GT, nadhani ni vizuri utupe data za kisomo cha Freeman kushindwa kwake kwa sababu hizo nyingine mbili umedata kinoma.
Mimi nimefanya kazi na Freeman ambaye kwa kiasi kikubwa naweza kumlaumu kwa mengi sana lakini baada ya kufahamu ukweli zaidi nimemsamehe...
Mimi ndiye mwanzilishi wa Space 1900 mwaka 1980 pale YMCA baada ya sisi kuondoka Keys Hotel..Na tulifanya mkataba na Freeman wakati huo baba yake yupo hai na Freeman akiwa bado akisoma shule nadhani wakati huo ndio kwanza alikuwa akiingia kidato cha nne au tano..Alifahamu uwezo tuliokuwa nao sisi laa sivyo asingekubali hata kidogo - at age naweza sema pengine 18.
Tuliendelea kupiga pale Mbowe tukafunika mji mzima na Freeman alipomaliza masomo yake alikuja kuendeleza biashara ya baba yake. Binafsi nilikuwa namwona mshamba tu hawezi kuingia mjini na speed alokuja nayo lakini kumbe jamaa alikuwa akisoma nyakati...
Kufikia mwaka 1984 Freeman alikuwa tayari akisukuma BMW 5 series, kijana wa miaka 20 enzi ya mwalimu. Katika hesabu zake aliona hakuna haja ya kukodisha watu hivyo akatupiga mtama Space 1900 tukahamia New Africa..Baada ya hapo Space ilikwisha na kuvurugika kabisa jambo ambalo binafsi nilimwona mnyama lakini kusema kweli hata mimi mwenyewe ningefanya hivyo kama ningekuwa nafasi yake...
Baada ya kuchuka madaraka yote mwenyewe akaweza kutumia umaarufu ambao tayari tulikwisha ujenga kuingia mageuzi mapya ya starehe hii. Freeman alifungua RSVP kashusha vitu vya kisawasawa vinavyokwenda na wakati kwa biashara hiyo..RSVP ikavuma na kila hatua ilivyozidi kuvuta watu aliweza kwenda na wakati kuweka mabadiliko ya biashara hiyo hadi kufikia kufungua Bilcanas, Hardrock cafe na juu kuongezea Much Moore hizi zote ni biashara ambazo zinaingiza fedha kuliko unavyofikiria...roughly mkuu alikuwa akiingiza kitu kama dollar 2000 hadi 3000 kwa siku za weekend tu.. kumbuka tu disco lilikuwa likipigwa seven days a week hata kama siku za kukosa aliingiza robo ya fedha hizo....bnado hujaweka hesabu za vinywaji..
Kwa hiyo unaweza sema kaanguka kibiashara leo hii kwa sababu unachoona wewe ni kufungwa kwa sehemu kutokana na Ukarabati mpya unaofanyika wakati Freeman amekuwa akifanya hivi toka achuikue madaraka ya kuiendesha Mbowe..
Ukarabati ni utamaduni ambao sisi waafrika hatuna kabisa na kama kuna kiongozi anayeweza kuonyesha tamaduni wa maintanance ktk maisha yake mwenyewe, hii ni dalili kubwa kwamba yupo ktk msitari unaonyooka ktk tamaduni za kuboresha biashara sio CCM kina Mkapa & co wanaokwenda na Punda aliyechoka kuendesha shughuli zao kiasi kwamba inabidi waibe fedha serikalini kuinua mitaji yao... Hawa wanakula hata mbegu za kupandikiza uchumi wa nchi nzima..
Tukianza kuhesabu waheshimiwa waliojaribu biashara na wameshindwa nadhani Tanzania nzima tutakuja achana na wanasiasa tuwaweke kina Bakhresa, Mengi, Mama Mkapa na pengine hata kina Patel kuongoza nchi maanake hawa ndio wameweza kufanikiwa shuleni, biashara na hata kuingia ktk Politics za Ikulu kupata umaarufu ktk biashara zao. Wabongo wanasema MWIZI SIO MWIZI HADI HAPO ATAKAPO KAMATWA..ndio hawa unaotaka kuwasifia hapa.
Ni imani ambayo imewapa nguvu sana kina Mkapa, Yona, Lowassa na Karamagi na kundi zima kuvuta mabillioni hadi siku watakayo/waliyo kamatwa tumejikuta it's Too Late kwa serikali na wananchi kufanya kitu kwa sababu wameisha jenga mizizi ama ngome kimafia kutokana na fedha walizokwisha iba..
Freeman is the Businessman na Politician ambaye huwezi kumhesabu mafanikio ama umaarufu wake ktk Politics na mfanyabiashara mwingine yeyote yule anayejaribu kujiingiza ktk siasa... He is above them all kwa sababu he is the ONLY businessman aliyewahi kusimama fainali za kugombea Urais nchini!
Je, Mbowe ana mapungufu?.. hili halinga pingamizi maadam yeye ni binadamu aliyeumbwa na tamaa unaweza kuyakuta mengi ya kibinadamu lakini hajavunja sheria.. hakuna hata kesi moja inayoweza kumfunga Freeman Mbowe kama FISADI... hakuna lakini chukua mtu mdogo sana ktk tawala za CCM hata katibu kata utakuta mlolongo wa malalamishi ya wananchi katika uongozi wake..
Freeman is tough na amekua kisiasa kiasi kwamba leo hii ni anaonekana kuwa tishio kubwa la chama kizima cha CCM...
Na ajabu kubwa ni kwamba hawa Chadema watu wake wachache tu wanaweza kuitetemesha CCM nzima.. Mtazame Dr. Slaa ama Zitto hawa watu watatu tu wamekuwa pingamizi kubwa la chama kizima cha CCM chenye wasomi waliobobea kisiasa.
GT, usitake kuleta za kuleta wakati humjui Freeman..binafsi leo hii naweza sema simjui kabisa kwa sababu yale mazuri na mabaya aloyafanya enzi za ujana wetu yanaweza kuwa nje ya siasa kabisa na siwezi kumhukumu Freeman kutokana na mashindano ya Ujana wetu.. Ni wakati tofauti na watu tumekuwa kiumri hata yeye mwenyewe sii ajabu atashangaa kusikia Mkandara huyu ndiye yule alokuwa Space1900...