Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Inawezekana mbowe ni threat katika sisa za Tanzania kwa sasa.

Mara kila siku naona watu wanajaribu hata kuweka info zisizokuwa na kichwa, yaani ni viwiliwili tu nina wasiwasi baadhi ya watu baada ya kuwa mafisadi na kugundua kuwa kila mtu amewajua sasa wameamua kutufanya wajinga kwa kudhalilisha kila mtu ili aonekane FISADI/hafai.

Najua cha kujua zaidi ni kwamba watanzania wa sasa wamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Usishangae hata muungwana wakati anahutubia wananchi wa Butiama(kama atahamua kufanya hivyo) akaulizwa atoe msomamo wake katika jambo zima la ufisadi.

Kwa hiyo haina haja ya kumushambulia Mtu sijui FISADI, Mkabila, Sijui nani la muhimu kama Kuna mkereketwa jaribu kuangalia wapi umekosea na jirekebishe watu tutakupigia makofi.
 
Kati ya Wabunge wote wa Viti Maalum wa Chadema ni mmoja tu asiyetoka Kilimanjaro na huyo ni Mhonga Saidi Luhwanya ambaye hata hivyo, yeye pia anatoka Kigoma ambako aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Uchaguzi, Zitto Kabwe anatoka pia.

Shida ninayo iona hapa ni uelewa wa Kanuni, Taratibu na Sheria. Wabunge viti maalum ni asilimia ya wabunge wa kuchaguliwa. kwa hiyo huwezi kuwa na wabunge wa Kuchaguliwa toka Iringa kumi na ukateuwa viti maalum toka Kagera. Maana hawa wote wanajumuika katika mabaraza ya miji na Halmashauri za wilaya.

kwa hiyo kama CHADEMA Kigoma imetoa Wabunge wawili wa kuchaguliwa na kupitia hilo CHADEMA hawawezi kutoa mbunge viti maalum Iringa, kisiasa itakuwa ni faulo. Mkoa wa kilimanjaro una wabunge wa upinzani wengi wa kuchaguliwa kwa hiyo kulinda masilahi ya vyama hivyo katika kambi zao hizo wanazopigiwa kura ni lazima kutoa wabunge na madiwani viti maalum kwa wingi toka huko huko Kilimnanjaro.
Kama ni suala la kutokipenda chama au kiongozi wake basi itafutwe hoja itakayokuwa na tija kumshitaki.
 
Tofauti na hali ilivyokuwa wakati Bob Makani alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kwa miaka mitano kuanzia mwaka 1999 hadi 2004 alipoamua kustaafu, Mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe ameonyesha jinsi anavyonuka uozo wa Uchagga kwa kukijazia chama hicho Wabunge wa Viti Maalum kutoka Kilimanjaro, mkoa ambako mwenyewe anatoka.

Kati ya Wabunge wote wa Viti Maalum wa Chadema ni mmoja tu asiyetoka Kilimanjaro na huyo ni Mhonga Saidi Luhwanya ambaye hata hivyo, yeye pia anatoka Kigoma ambako aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Uchaguzi, Zitto Kabwe anatoka pia.

Nafahamu kuwa hata jambazi anayeiba na kuua watu kwa mapanga au risasi hawezi kukosa kabisa wendawazimu wa kumtetea uovu wake, hivyo hata uchafu huu wa Mbowe alioifanyia Chadema mwaka 2005 hauwezi kukosa mabingwa wa utetezi wake.

Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema wanaotoka Kilimanjaro ni pamoja na Halima Mdee na Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa huo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Wengine ni aliyekuwa mke wa ndoa wa mtoto wa Ndesamburo, Grace Kiwelu na Anna Komu, mgombea mwenza wa Mbowe katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2005 ambaye ingawaje ni Mzanzibari, lakini ameolewa Moshi na ndiyo maana anatumia jina la Kichagga ambalo ni la mumewe, akabadili dini kutoka Uislamu anakoitwa Maulida na kuwa Mkristu.

Nashawishika kusema kuwa Mbowe aligombea Uenyekiti wa Taifa wa Chadema ili atumie nafasi hiyo kwa faida zake mwenyewe na kupanda Uchagga katika chama hicho hata kama ni kifisadi. Ndiyo maana hata Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho hivi sasa naye ni Mchagga kutoka wilaya ya Moshi Vijijini, Anthony Komu.

Huu ni ushetani wa kisiasa ambao ninashangaa kuona watu wanaojifanya wana macho makali ya kuona maovu yote yaliyomo ndani ya CCM kama akina Chacha Wangwe, Dk. Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Msafiri Mtemelwa, Erasto Tumbo, Ali Chitanda na Kafulila hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi angalau siku moja tu kuusema hadharani ama kuupinga kwa namna yoyote.

Wanachofanya siku zote ni unafiki wa kuusema chinichini ili Mbowe asisikie, lakini akiwepo mbele yao wote wanaywea.

Zephania; kwa hili natofautiana nawe. Mwaka 2006 nilifanya mahojiano na Bwana Mnyika kuhusu hili suala la ukabila CHADEMA. Nikaandika habari hii. Hata hivyo mhariri alihariri na kutoa sehemu ndogo sana ya habari hii. Nakuletea hapa habari yenyewe kama ilivyo. Hii ilikuwa ni miaka michache iliyopita

MNYIKA: CHADEMA SI CHAMA CHA WACHAGA
• Asema wachaga wako mpaka serikalini
• Atoa rai kwa watanzania kuwakanya wanachochea ukabila

Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), John Mnyika ameibuka na kuzungumzia tuhuma kwamba chama hicho ni cha wachaga. Mnyika ambaye katika uchaguzi uliopita alikuwa mgombea wa Ubunge katika jimbo la Ubungo mkoani Dar es salaam amezungumzia suala hili kutokana na hivi karibuni kujitokeza kwa wanachama wanaojitoa katika kambi ya upinzani na kuingia Chama cha Mapinduzi(CCM) ambao pamoja na mambo mengine kutoa shutuma kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga.

Hivi karibuni, magazeti kadhaa ya kila siku(si gazeti hili) yamemnukuu aliyekuwa kiongozi wa chama cha wananchi CUF akiwa amezunguka vyama vya UMD, UDP, NCCR-Mageuzi, CHADEMA , na kuanzisha chama cha ULIMO bila mafanikio,Aman Nzugile Jidulamabambasi( maarufu kama Jidula ama Jidu), alirejea CCM, akitokea chama cha wananchi CUF ambapo alikuwa mgombea ubunge huku akitoa shutuma za hali ya juu kuhusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari(MAELEZO).

Itakumbukwa kuwa baada ya kurejea CCM, Jidulamabambasi alidai na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa vyama vya upinzani havina mwelekeo na kwamba vinaubaguzi , huku akisisitiza kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ni chama cha kikabila na kwamba kimejaa wachagga na kuongeza kuwa CHADEMA kilianzishwa kabla ya uhuru kwa maslahi ya wachagga ambapo kilikuwa na jina la Chagga Development Manifesto(CHADEMA).

“Kwa hulka na tabia ya Jidula tunayemfahamu, tunaamini kuwa maneno haya hata yeye mwenyewe anaamini si ya kweli na pengine alishinikizwa na CCM aseme hivyo kwani propaganda za namna hii zimekuwa zikitumiwa na CCM kwa muda mrefu dhidi ya CHADEMA, amesema Mnyika.

Aidha Mnyika alisisitiza, “Na kwa mtu kama Jidula mwenye hulka ya kutafuta uongozi kwa udi na uvumba, sio ajabu kutamka maneno ambayo hata mwenyewe ama hayaamini au hayajui. Kwa hiyo namtaka Jidula athibitishe kauli yake kuwa CHADEMA ni chama cha wachagga kilichikuwepo kabla ya uhuru wa Tanganyika, kwa upande mmoja. Lakini pia kupinga kauli hiyo ya upotoshaji ya Jidula kwa upande wa pili”.

Akizumgumzia shutuma kwamba CHADEMA ni chama si siasa kilichoanzishwa kabla ya uhuru kikiitwa Chaga Development Manifesto Mnyika alisema “ kwa mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa historia walau ya kiwango cha shule ya msingi, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA”

Kwa msomi wa kiwango cha Jidula kushindwa kung’amua vitu vidogo kama hivi, kunazua maswali mengi kuliko majibu hasa kuhusu uhalali na usahihi wa elimu yake kwa upande mmoja kama ni kweli amepotosha kwa kutojua. Lakini pia kunazua maswali kuhusu kiwango cha uzalendo wa Jidula anapokuwa anatafuta nafasi ya uongozi kama kweli alikuwa anajua lakini ameamua kuupotosha umma wa watanzania kwa malengo yake ya kisiasa katika chama hicho.

Kwa upande mwingine akijibu shutuma ya kwamba CHADEMA imejaa wa wachaga, Mnyika, “Pengine hatuna hakika na uwezo wa Jidula wa lugha ya kiswahili, labda pengine anatumia maneno asiyoyajua maana yake. Kwa mfano Jidulla anaposema CHADEMA imejaa wachagga maana yake nini?. Kwa akili za kawaida, maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Kama Jidula alikuwa na ujumbe huo!, Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?”

Akitoa takwimu kuhusu idadi ya wachaga katika CHADEMA Mnyika ameweka wazi kuwa, “Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Wazanzibari ni wengi zaidi kati ya hao viongozi sita. Kwa nini Jidula hakusema kwamba CHADEMA ni chama ambacho kimejaa wazanzibari?

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma kabila la Jidula ni watatu?. Kwa nini Jidula hakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa kamati kuu, kati yao hakuna na mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro? Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi. Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro? Je, Jidula anataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.

Zaidi ya hayo namshangaa Jidula akitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini namshangaa zaidi Jidula kwa kuwa hatukumsikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga wengi zaidi katika baraza la mawaziri. Je, kwa mantiki ya Jidula serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, Je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga? Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa mtu kama Jidula anaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Nimeamua kujibu shutuma hizo kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Naamini kauli za watu kama Jidula zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini.

Mwalimu Nyerere aliwahi tena kusema kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii ya Jidula.
 
Hana hamu maana amepara majibu mengi na mifano kibao nadhani anatafuta udaku zaidi .Kuanzia sasa acheni ku entertain udaku kaa hoja haina kichwa wala miguu na usahidi basi inaachwa hadi ife na yenye ushahidi unamwagwa kama hivi na hapo wataona aibu wenyewe .
 
Kuna hii mada ina mwanga mzuri wa ukabila Chadema.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=987

Mzee Kifimbo

Inaelekea wewe ni mtaalamu wa kurejea kweli. Basi tuletee ile ambayo Zitto aliweka bayana wabunge wa viti maalum walitueliwaje. Halafu tuwekee na ile ambayo Mnyika alieleza kiundani kabisa kuhusu viti maalum na kuvunja kabisa hoja ya ukabila. Halafu ndio tutajua ukweli wa maneno yako jamani

Asha
 
YA ZITTI kabwe sikuiona kuna nyingine zaidi ya hii uliyoweka ya Mnyika? tupatie kama unazo. hapa ni shuleni tunajifunza hatushindani kaka.
 
Nshakuwa kaka tena? Ipo, kati ya kwenye 'CHADEMA must reform' au 'Focus 2010', zipo pia za Mnyika alizungumza kwa kirefu. Ya Zitto ni ya zamani zaidi. Mi sijui kutafuta jamani

Asha
 
Mzee Kifimbo

Inaelekea wewe ni mtaalamu wa kurejea kweli. Basi tuletee ile ambayo Zitto aliweka bayana wabunge wa viti maalum walitueliwaje. Halafu tuwekee na ile ambayo Mnyika alieleza kiundani kabisa kuhusu viti maalum na kuvunja kabisa hoja ya ukabila. Halafu ndio tutajua ukweli wa maneno yako jamani

Asha

halafu wewe usijifanye mzuri wa kukimbia, ebu kajibu kule kwenye ile topic ya mbowe nilichokuuliza,lol ! seriously though !
 
according to think piece iliyokuwa dropped leo mchana mwandishi alisema hivi:

Freeman Mbowe – failed in school, failed in business, failed in politics, and all this after being born in the royal family, the House of Mbowe. And he still has the audacity to vie for Presidency. In the current political state of play, he is irrelevant, and, as a HIPC (Heavily Indebted Party Chairman) he is finished as a politician.[/

SOURCE hii hapa:
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13378

freeman_bowe_in_lndon.jpg

Discuss...
 
Umebadilika toka kwenye credibility umekuwa mkuuu wa majungu sasa .Unaogopwa kama ukoma kwa uzushi wako .Haya madai yako unaweza kuyasimamia ? Mbowe anarudi kumalizia shule baada ya kuomba time out kufanya siasa na biashara zake na inakubalika wewe unasemaje?
 
Let me grab a large drink and popcorns....The show is about to begin...

Alafu GT how far do you want people to go(iscuss) with this?
 
Ukichukua mkopo kwa madhumuni ya biashara na ukashindwa kuurejesha hadi ukaburuzwa mahakamani, that to me is a failure!

Hivi ni akili daraja gani hujadili watu katika style hii? Mnanyoosha vidole tu wengine humu mlipata division mduara kidato cha nne, halafu mnachonga.
 
Kana,
Freeman hajashindwa kulipa mkopo wake. Kinachofanyika ni njama za "watawala" kuonyesha kuwa mwenzetu kashindwa. Lakini with time kweli utajulikana tu. You can fool some of the people some of the time....
 
Let me grab a large drink and popcorns....The show is about to begin...

Alafu GT how far do you want people to go(iscuss) with this?

Hahahaha

Hii ya Mbowe nilipenda zaidi

watu tunaweza kureverse kwa kuanzia kuleee kwenye issue ya WAPUKI, mpaka kwenye tuhuma za kuuziwa magari ya wizi na akina Saleh Ziebi ( Range Rover Vogue new model) ili hali akijua kuwa ni la wizi huku London then atuambie kama kweli alideclare kiasi gani CHADEMA walipewa na Conservative (UK), kisha atuambie kwa nini anaona tabu kumsomesha JJ MNYIKA halafu tusisahau ule mkopo wa NSSF

this should be an interesting one...
 
Ukichukua mkopo kwa madhumuni ya biashara na ukashindwa kuurejesha hadi ukaburuzwa mahakamani, that to me is a failure!

Ni mahakama ipi hiyo aliyoburuzwa? Na huo mkopo alichukua kwa ajili ya biashara gani? Naomba unifahamishe, labda mi si Mtanzania wa Tanzania!!!
 
Think Big niko nawe wacha tuone majibu ya hawa jamaa .Unajua nadhani GT unapaswa sasa kupumzika kidogo .Umechoka umejawa na nongwa na umbeya .Unazusha na unageuza sasa hii serious forum kuwa kijiwe .You must avoided .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom