Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 12
Ndugu Mkandara,
Si kweli kwamba sera ya majimbo ilichangia CCM kuzoa kura au kupata " matokeo walioyapata". Kama ungekuwa unakumbuka vizuri mapambano ya hoja wakati wa kampeni, basi CHADEMA walikuwa wawaburuza vibaya CCM, propaganda zote za CCM zilijibiwa kwa ufundi sana na Freeman kwenye mikutano yake ya kampeni.
Hoja ya kwamba Sera ya majimbo italigwa taifa ilijibiwa vizuri kabisa na CHADEMA.Mbowe alohoji kwa kutengeneza jimbo mfano la kanda ya ziwa, ambapo ataonganisha mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera anaonganisha makabila mangapi? Akajibu kwa kusema wanaoligawa taifa ni CCM kwa kuendelea kugawa wilaya kwa misingi ya kisisa na kikabilia! Mfano jimbo la hai waligawa kwa misingi ya CCM na CHADEMA, jimbo la Tarime hivyo hivyo na pia sasa wameweka mstari upande wa wajaluo na wakurya! Nani analigwa taifa?
Taifa linaendelea kugawanyika kwa ubinafsi wa viongozi, maamuzi mabaya ambayo yanaongeza nyufa kati ya maskini na tajiri hapa ndio yanaligawa taifa! Angal;ia Zanzibar walipunguza majimbo ya pemba na kuongeza ya unguja kwa misingi ya kunufaika kisiasa!Kwa hiyo mfumo wa sasa ndio unaligwa taifa. CCM walishindwa kujibu hoja, walizidiwa, wakaanza kushambulia helkopta na baadae Mzee kingunge akaja na kituko kwamba Mbowe asimnukuu Nyerere, eti kwa hoja kwamba Nyerere ni mali ya CCM! Hivyo Mbowe na Nyerere ni vitu viwili tofauti!
Kama tungekuwa tunaamua kwa kutumia hoja,CCM walipaswa kuwa wanne! Nyuma ya CHADEMA,CUF na NCCR! Propaganda zote dhidi ya sera ya majimbo zilijibiwa kwa ufasaha kabisa kwenye mikutano yake.CCM walizidiwa na kujawa na hofo.
Hata UDSM ilionekana kumkubali na kumuelewa mno Mbowe, ikumbukwe Mbowe alikwenda Nkurumah kwenye maazimisho ya siku ya mwalimu Nyererena na kuteka wanaafunzi kutokana hoja zake nzito, pia uwepo na mvuto wa Mnyika alie kuwa anaogombea jimbo la ubungo uliasiadia kuleta hamasa kubwa chuo kikuu.
Kouna hivyo, CCM ilizidi kuwa na hofu, ndipo wakaandaa mkutano wao pale Diamond, wakahonga wanafunzi na waliwaletea mabasi kuja kuawachukua wanafunzi kuwapeleka Diamond, JK hakuwa na ujasiri wa kusimama Nkurumah kama ambavyo walikimbia mdahalo wa wagombea uraisi ulioandaliwa na channel TEN. Ni katika mkutano ule wa diamond ndipo JK alipo ahidi kuongeza mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kuongeza idadi yawanaopata mikopo, aliropoka kwamba wangetoa mikopo kwa wanafunzi 30,000, hii alilenga tu kuwateka wanafunzi, kwa maana sasa hivi ameshindwa kabisa kutekeleza ahadi yake hii kwa kupunguza idadi ya watu wanao pata mikopo kwa kuongeza kigezo cha Daraja la kwanza kwa wavulana na daraja la kwanza na la pili kwa wasischana, haya yanafanyika wakati takwamu zinaonyesha jumla ya wanafunzi waliopata Daraja la kwanza mpaka la tatu kwa mwaka jana ni 21,000 tu! Hivyo kama angeishi ahadi yake ya 30,000 wanafunzi wote waliofaulu wangepata mikopo!
Na katika kipindiki hiki hata Profesa Rweitama alijenga hoja kuunga mkono hoja ya majimbo katika maadhimisho ya siku ya uhuru.Watu walielewa hoja ya majimbo, propaganda za CCM hazikufanya kazi, ndio maana wameyapika matokeo ili kumkatisha tamaa Mbowe ambao kwa vyovyote vile wanamhofia sana!
Turudi kwenye suala Uchumi, umesema kwamba tatizo letu sasa hivi ni uchumi ni kweli lakini linasababishwa na nini? Uongozi mbovu usiowajibika wala kuwajibishwa.Katiaka Mikutano ya Kampeni, Mbowe alijenga hoja kwa kumnuku ya Nyerere kwamba ili nchi iendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
Alifafanua kwamba watu tanao, wengi tu na tuna arhi nzuri na yenye utajiri mkubwa tatizo kuu ni siasa safi na uongozi bora ambao umeshindwa kutumia vyema rasilimali watu na ardhi yenye utajiri mkubwa kuleta maendeleo!
Sera ya majimbo inasisitiza mgawanyo wa rasilimali na kuwapa mamalaka zaidi wananchi kwa kuchagua viongozi na kupunguza idadi ya viongozi wakuteuliwa, kwa kufanya hivyo tutakuwa na uongozi unawajibikla zaidi na kuchochea maendeleo.
Kuhusu wilayani, hoja ya majimbo haisemi tutakuwa na wabunge wenye nguvu zaidi ya wakuu wa wilaya. Nilipo andika nilitaka kuonyesha utitiri wa viongozi wilayani amabo wanagongana kimajukumu,na kuwa mzigo kwa taifa na pia nilionyesha nguvu ya viongozi wa kuteuliwa dhidi ya wale wa kuchaguliwa.
Sera ya majimbo itafuta mikoa, wilaya zitabaki. Ila viongozi wote wa kuteuliwa wataondoka! Kuanzia mkuu wa wilaya, kiongozi wa juu atakuwa ni meya ambae anachaguliwa na kuwajibika moja kwa moja kwa wanachi, badada ya wilaya ni serakali ya jimbo chini ya gavana(au kwa jina lolote litakalo pendekezwa) ambae atakuwa anachaguliwa. Sera ya .majimbo inaainisha mabo yatakayo kuwa chini ya serekali kuu na sekali za majimbo!
Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeondokana na miungu watu wanaoteuliwa, ambao hawana mipanago yoyote ya mandeleo kwa maneo husika wala hawajibiki kwa wananchi, pia vyeo vya kuteuliwa vimekuwa vikitumika vibaya,marafiki, nyumba ndogo za viongozi na wapinzani wanaonunuliwa wamekuwa wakizawadiwa vyeo hivi pasipo kuanagalia uwezo wao au wana mipanago na maono gani ya kimandeleo kwenye maeneo husika.
Siamini kama sera hii inagezwa, imesema itaendana mazingira ya Tanzania. Watu wanababaika na jina jimbo, tunaweza kutumia neno kanda. Ikumbukwe hata mahakama na taasisi nyingine kama TRA zinafanya kazi kikanda! Haya ndio majimbo yenyewe!
Na isitoshe, CHADEMA wanaendelea kusema kwamba, sera ya majimbo haitachomekwa tu watakapo chukua nchi, hapana. Moja wataitisha mjadala wa kitaifa juu ya mabadiliko ya kikatiba pili mabadiliko ya kimfumo wa utawala amabapo serekali ya CHADEMA itapendekeza sera ya majimbo na hoja zake.
wananchi watajadili na kuamua na pia wanaweza kuikarabati watakavyo ona inafaa kukidhi mahitaji ya nchi na kuondoa hofu za watu. Na kuonyeaha kuwa wana maanisha wanachosema, mwaka jana CHADEMA wamefanya mabadiliko ya katiba yao ambapo wameamua kuishi sera ya majimbo! Imingizwa kwenye muundo wa chama, wanaifanyia kazi sera yao baada ya mika mitano watakuwa na uzoefu na sera wanayoisimamia hivi ndivyo chama mbadala kinavyopaswa kuwa.
Kwenye mgawanyo wa rasilimali, nimeeleza mantiki ya kubakiza sehemu ya rasilimali kwenye maeneo husika, katika mchango wangu wa mwisho, rejea suala la gharama za kuwa karibu na rasilimali na pia umuhimu wa wananchi wa maeneo husika kufaidika na rasiliamali, pia rejea mfano wa manispaa za wilaya za kinondoni na Ilala. CHADEMA inasema sehemu ya mapato ya railsimali ndio yatabakishwa na sehemu nyingine kupelekwa serekali kuu.
Naomba ulete hapa hoja zako za kijiwe cha zamani mlizo muhoji Mnyika kwa manufaa ya mjadala huu na kwetu sisi ambao hatukubahatika kuwepo huko.
Tujadili