Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mbowe na Mnyika ni wasanii tu.
Huo umakamu mwenyekiti ni wa NGO hicho chama hakina maana yeyote ni ulaji tu.tizama Mnyika akazungumzia mambo ya Ukimwi kila tapeli sikuhizi anatumia mgongo wa Ukimwi.
Mwanasiasa.
Uko kimya hivyo? nauliza mwenyekiti anasomea librarian? au French na Germany? kweli mwanafunzi atakuwa na muda wakati huu kuhutubia mikutano? mnunulieni cheti mchezo uishe.usomaji Mbowe hana.
 
Chinga et al:

You have highlighted an important issue of priority with our leadership at home.

Saying thank you to voters is a very good idea and shows maturity in politics. But how one goes about doing it, in a poor country like Tanzania, is another question, bearing in mind what the incumbent leadership is doing when we see expensive presidential jet which can only land on about 6 places in the whole country, radar, MPs remunerations, etc.

Whenever an opportunity allows, I always tend to encourage people to adapt one way of discussing issues of the day. Try and separate issues from personality and this will inevitably save the issue under discussion justice as it will get the attention it so deserve. The minute you indulge into personal attacks and such innuendos, one just becomes part of the whole mess and the points that needs addressing gets muddled up and no one gains out of this other the those wishing the status quo to remain unchanged forever.

To that end, it will be helpful if this thread were to first

(a) Substantiate the facts given
(b) Debate on the rationale behind such expenditure
(c) Agree / Disagree with reasons given
(d) Propose alternatives that would have served well than what has been done.

From the outset, assuming all is true as reported, some of us know what we would want to see our leadership doing. I think they have lost the plot and most actions are simply inclined to corrupt practises, greed and selfishness. Our public doesn't even help when we behave in ways that we expect our leaders to be corrupt and shower them with full praises at a time when actually they deserve a slap!

Do your math as Chinga suggested (have used online tools to calculate the figures):

Duration calculation results
From and including: Wednesday, 29 November 2006, 00:00:00
To, but not including: Friday, 22 December 2006, 00:00:00

The duration is 23 days, 0 hours, 0 minutes and 0 seconds

Note: This calculator does not take time zones, daylight saving time or leap seconds into account.

Alternative time units

23 days, 0 hours, 0 minutes and 0 seconds can be converted to one of these units:
1,987,200 seconds
33,120 minutes
552 hours
3 weeks (rounded down)


Thursday, December 28, 2006

662,400 US Dollar = 863,391,323 Tanzanian Shilling
This means:
You buy 662,400 US Dollar : 863,391,323 Tanzanian Shilling

What about using 863,391,323 Tanzanian Shilling to build a Primary School in each and every say, region or district or any level but with such publicity and what will be actual gain? How much benefit will be to the people and the Chadema as a party?

If we have economic planners here, they can give us educated estimates of what that sum could achieve in actual development projects which have direct impact to people’s daily lives.

Regards,

Taasisi.
 
JJ et al mna kazi kubwa ya kuendelea kutueleza mambo yanavyokwenda... (wakati mwingine hudhani kama tunamuonea JJ kwa maswali (na vijembe?) lakini kwa vile kajitolea kwa dhati kwenye chama basi ataendelea kukidhi mshawasha wetu bila wahaka kama kawaida yake).

CCM nao wanataka kuonekana wako makini katika kuiga vita rushwa! Kazi kwelikweli!

Tarime Chadema leaders defect to CCM

SOSTHENES MWITAin Dodoma
Daily News; Thursday,December 28, 2006

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Secretary General Yussuf Makamba on Tuesday received 11 new CCM members who defected from two opposition parties.

Three of the defectors were Tarime district’s Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) top leaders. The party has 17 councillors and an MP in the constituency.

The remaining eight defectors were from Tanzania Labour Party (TLP) in Dodoma region. The Tarime defectors included Mr Laurent Yohanes Marwa, the chairman of Chadema in the district.

Mr Marwa said he rejoined CCM because Chadema had lost its course and was heading for political doom. He prophesied Chadema’s demise saying, “It will no longer be in existence by the year 2010.”

Mr Marwa rejoined the ruling party along with Tarime district Chadema secretary, Mr Chacha Daniel Okong’o, who said Chadema was so poor that it did not own neither a regional nor a district office.

Mr Okong’o condemned Chadema Chairman Freeman Mbowe for using a helicopter during his presidential campaign last year, saying he made the party bankrupt. He was pessimistic about Chadema’s ability to retain its members in future.


Another defector, Mr George Chacha Mtetya, who was Tarime’s Chadema publicity secretary in the district said he would demolish his former party in the district.

Meanwhile, Mr Makamba has announced that CCM members will hold a countrywide meeting on January 14, next year, to discuss and draw strategies on how to fight corruption during the party’s general elections in July, next year.
 
Mwanasiasa..

Toka niahidi kujibu Disemba 5 na kuchelewa kwa siku kadhaa kujibu na nikaja kutimiza ahadi yangu nikajibu kuhusu elimu na chopper sijawahi kuahidi tena tarehe. Na kweli nimeacha sasa kutoa tarehe. Sasa najibu kwa kadiri ratiba inavyoniruhusu. Hivyo namshangaa ndugu yangu Mtalii kuendelea kusema tarehe 5. Sijui ni ipi hiyo!

Wote..

Sasa nimebanwa na shughuli kama mjuavyo tuko kwenye mshikemshike wa ziara. Pindi nikipata wasaa nitakuja kujibu hoja za family business na uhusiano wa CHADEMA na conservative etc. DrWHO umeendelea kusisitiza swali la Mbowe kama ni realist au la. Sitaki kujibu ndio au hapana. Nitakuja kujibu ndio au hapana na kusema kwa nini!. Kwa mtazamo wa nje hili swali linaonekana dogo. Lakini hili swali ni ideological!. Nitalijibu kwa muktadha wa uhusioano wa kiitikadi. Vuta subira ndugu yangu,.musuala ya pragmatism, idealism, realism, materialism etc sio ya kuyajibu kwa mstari mmoja.

Ila kwa sasa siwaachi hivi hivi, nilikuwa napita archive yangu nikakauta Makala ya Mzee Mtei aliyoiandika mwaka mmoja aliopita ambayo inajibu baadhi ya maswali mliyoyauliza. Naiweka muijadili then nitakuja baada ya kuwa imeshajadiliwa kutoa mtazamo wangu sasa. Yapo ambayo sikubaliani na Mzee Mtei katika makala yake, Nitayagusia.


Kuhusu IYDU>

Nawashukuru wote kwa pongezi. Nitazungumzia hili kwenye mjadala kuhusu conservative. Ila ndugu yangu mtalii amesema nimezungumzia UKIMWI tu, si kweli. Hicho ndicho mwandishi ameona habari! Soma press statement kamili hapa…http://www.chadema.net/habari/2006/habari5.php.Na ukweli ni kuwa nilisema mengi katika hotuba yangu ya dakika tano ya kuomba kura. Nitaiweka hotuba kamili kwenye blogu yangu ili uweze kuirejea.

Kwaherini kwa sasa, ngoja nikaendelee na mambo ya ziara. Hakuna kulala, Mpaka Kieleweke

kuhusu Mbowe>

Amekuja Tanzania siku chache kabla ya Xmas na anamaliza ziara tarehe 5 Januari na kurudi masomoni kujiandaa na mitihani. Atarudi tena likizo ijayo kumalizia ziara mikoa iliyobaki. Wakati huo huo chama kitandelea na mkakati wa CHADEMA ni msingi kujenga chama chini kabisa. Kama nilivyosema, ziara za sasa za mwenyekiti ni za kushukuru na kufanya mashambulizi ya juu!


JJ
 
Makala ya Mzee Mtei....


CHADEMA NI NINI NA NI NANI


Nikiwa Muasisi na Mwenyekiti (Taifa) Mstaafu wa Kwanza wa CHADEMA naona ninawajibika kujibu makala ilioandikwa na H. Nesario iliyokuwa na kichwa cha habari kama hapo juu, na kuchapishwa katika Toleo la Mtanzania Jumapili tarehe 4 Desemba, 2005.

Kuanzishwa kwa Chadema
Ni kweli kwamba wastaafu kadhaa walikuwa miongoni mwa watu waliojiunga nasi kuanzisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka wa 1992. Lakini kulikuwa na wananchi wa kila rika, taaluma na kazi. Kulikuwa na wanasiasa kama Mheshimiwa Edward Barongo ambaye aliungana na mimi hata kutia saini katika Fomu ya Maombi ya kusajiliwa kwa awali na Mama Mary Kabigi, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam. Wafanya biashara kama Bwana Medard Mutungi na Kanali Mstaafu Geofrey Marealle walituunga mkono. Wana-ushirika kama Brown Ngwilulupi walijiunga siku zile za mwanzo. Mameneja wa makampuni kama Victor Kimesera, Michael Shang'a na Alphonse Maskini. Vijana kama Freeman Mbowe pamoja na kundi kubwa la wanazuoni kama Lenny Kassoga walishiriki kubuni katiba ya awali. Wanasheria pia walikuwepo, mmoja wao akiwa Bob Makani ambaye alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza na Mwanaidi Majaar ambaye alikuwa mmoja wa wadhamini wa mwanzo. Wakulima na wafanyakazi, wake kwa waume, walituunga mkono mara tu ilipojulikana kwamba tulikuwa na mpango wa kuanzisha Chama kipya cha siasa sheria itakaporuhusu. Kwa hiyo si kweli kwamba CHADEMA kilianzishwa tu na wastaafu.

Asili ya Misimamo ya Chama
Ni sahihi pia kwamba mimi binafsi nilibahatika kushika nyadhifa za kiserikali kuanzia wakati tulipopata Uhuru, zikiwepo Chief Establishment Officer, mwaka wa 1962, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha 1964, Gavana mwanzilishi wa Benki Kuu, 1966, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1974 na mwishowe, Waziri wa Fedha na Mipango. Wadhifa wa uwaziri niliushika mara baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki 1977, nikaendelea hadi wakati wa vita dhidi nduli Idi Amin wa Uganda.

Baada ya vita nilikuwa na msimamo tofauti na ule wa bosi wangu, Rais Mwalimu Julius Nyerere. Tofauti hizi zilihusiana na mikakati ya kufufua uchumi ambao uliathirika sana wakati wa (na hasa kutokana na) harakati za kumfukuza adui kutoka nchi yetu. Uchumi ulidorora pia kutokana na miradi na mashirika mengi ya umma kuanzishwa kisiasa bila uchambuzi yakinifu na kuendeshwa kwa hasara na kutegemea ruzuku kutoka Hazina. Kwa maoni yangu haya yote yalihitaji kurekebishwa kimuundo na kimenejimenti.

Kutokana na mlipuko mkubwa wa bei uliosababishwa na sera zetu za kuendesha serikali na mashirika ya umma, na uzalishaji duni wa bidhaa, thamani ya sarafu ya Tanzania ilikuwa imeshuka sana. Nilikubaliana na ushauri wa I.M.F. na Benki ya Dunia wakati huo kuwa tulihitaji kurekebisha thamani hiyo, pamoja na kutathmini uendeshaji wa miradi na mashirika kadhaa ya umma. Rais Nyerere alikataa kata kata kwamba hawezi kukubali ushauri huo na hata akaamuru ujumbe wa I.M.F. uliokuwa nchini ufukuzwe. Kwa vile niliona msimamo wa bosi wangu ulitokana na watu waliokuwa wanapotosha mambo na haungesaidia kutatua matatizo yaliyokuwa yanakabili taifa letu, nilimwandikia kumuomba ateuwe Mtanzania mwingine ambaye angeweza kuendesha naye uchumi wa nchi yetu. Rais alikubali kujiuzulu kwangu na ndipo nikaacha uwaziri, nikahamia Arusha kuwa mkulima kuanzia 1980.

Kwa hiyo ni hisia za Bwana H. Nesario tu kwamba eti mimi nilikuwa natetea au kusimamia haki za wenye mitaji, ambapo Mwalimu alikuwa anatetea haki za Watanzania masikini. Najiuliza kuendelea kuyapa ruzuku kutoka Hazina mashirika muflisi ni kutetea haki za Watanzania masikini? Huko ni kutoelewa menejimenti fanisi au uchumi! Nesario anahitaji kufunzwa uchumi na menejimenti yenye tija, licha ya kwamba alifanya kazi serikalini mpaka akastaafu. Alikuwa na cheo gani alipostaafu?

Historia ya nchi yetu kuanzia wakati nilipojiuzulu, mwisho wa 1979 imedhihirisha kwamba kama ushauri wangu ungekubaliwa, mambo yangeendelea kwa unafuu zaidi. Nimkumbushe Nesario na wengine wanaoonekana kusahau, kwamba kuanzia mwanzo wa 1980 bidhaa muhimu kwa matumizi ya wananchi wa kawaida zilikuwa adimu sana na Watanzania hasa wa kipato cha kawaida na cha chini, waliteseka sana. Ni wale wakubwa tu waliosafiri nje ya nchi ndiyo walioweza kuleta na kukidhi mahitaji yao.

Sijui Bwana Nesario alikuwa anaishi wapi wakati huu, lakini sabuni, sukari, mafuta ya kupikia, nguo, viatu, karatasi, unga wa sembe na wa ngano, mchele, mafuta ya taa na karibu kila aina ya bidhaa ilikuwa inauzwa kwa kibali au kwa bei ya juu sana. Hata baadhi ya wananchi mashambani walilazimika kuvaa mifuko mitupu ya saruji au ya mbolea! Ilifikia mtu akitoka nyumbani akaona foleni ya watu mbele ya duka alikuwa anajiunga nayo akitarajia mwisho wake angeweza kununua chochote kilichokuwa kinauzwa. Wenye magari hawakuwa wanaruhusiwa kuendesha Jumapili jioni, na petroli ilikuwa inauzwa kwa kibali na kwa bei ya kuruka. Nahisi Nesario alikuwa nje ya Tanzania ndiyo maana anajizungumzia tu bila kuona adha au taabu tuliokuwa tunapata.

Fursa ya kuunda chama mbadala kwa Chama cha Mapinduzi ilitulazimisha tubuni filosofia na sera ambazo zingeepusha taifa kurudia makosa ya zama za ujamaa zenye sera zisizo na tija na uendeshaji wa kiimla. Wananchi ni lazima waweze kuamua mambo yahusuyo maendeleo ya taifa lao kwa uhuru kamilifu, ujasiri na bila ya woga na kuepuka utawala wa kiimla. Rasilimali za nchi ni lazima zitumike kunufaisha wananchi. Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira yanayowezesha mitaji kuingia nchini. Uhuru wa soko ndiyo njia endelevu ya kuvutia mitaji ili raslimali za nchi ziweze kutumika kikamilifu, lakini papo hapo lazima umma wote ufaidike na mazingira yawekwe kuhakikisha wananchi wanajituma kwa kadri iwezekanavyo kupata kipato chao wenyewe. Wasiojiweza na ambao hawakupata ajira watadhaminiwa na umma. Miundombinu ya kiuchumi na ya kijamii itamilikiwa na umma na kuendeshwa kisayansi, kuhakikisha ni endelevu na ina tija. Miradi ya umma itabuniwa na kuendeshwa bila pupa za kisiasa. Misimamo kama hii ni ya social democrats na ilitangazwa mapema na CHADEMA. Kama Bwana Nesario aliisoma au kuisikia hangeweza kusema eti kwamba chama hiki kinasimamia mabepari na wenye mitaji. Najisikia mshindi kwamba licha ya CCM kujidai eti ni chama cha ujamaa, wameiga sana misimamo ya CHADEMA kama tulivyoitangaza hapo awali.

Itakumbukwa kwamba licha ya matamshi ya Mwalimu Nyerere wakati wa kukataa ushauri wangu (na wa I.M.F) kwamba hatageuka kutazama nyuma kwani angekuwa "jiwe la chumvi kama mke wa Loti", sisi CHADEMA tulimpelekea kijitabu cha Sera na Misimamo yetu mwanzoni mwa mwaka 1994. Mwalimu alizisoma na baadaye alitamka hadharani alipokuwa huko Mbeya kwamba sera zetu zilikuwa safi na zingeweza kuwaondolea Watanzania kero zao. Maneno ya Mwalimu yalikuwa "Heri Mtei, Bwana"! Hizo ndizo sera za CHADEMA kimsingi.
 
Makala ya Mzee Mtei ya Mwaka jana....


Viongozi ni Wanafamilia?

Kuhusu madai ya Bw. Nesario kwamba CHADEMA ni kikundi cha familia ya viongozi, naweza kusema ni uzushi mtupu usiokuwa na msingi wowote. Kama kulikuwa na watu walioniunga mkono ambao wana uhusiano wa karibu na mimi, hii ni kutokana na kwamba wananifahamu kwa kina na walielewa mapema umakini wangu katika upendo wa nchi yetu na uzalendo wangu. Si ajabu kwamba wanaweza kuwa wa karibu kijamii. Hata Baba wa Taifa, ndugu zake wa karibu kama mdogo wake, Joseph Nyerere aliongoza TANU Youth League, shemeji yake, Lawrence Gama alikuwa Katibu Mkuu wa CCM. Kuna ajabu gani kama ndugu wa karibu anaafikiana na kiongozi na kujiunga na Chama chake? Nesario anafahamu kwamba Rais wa sasa wa Zanzibar alilelewa na Hayati Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar? Mbona hata mwanae Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ni kiongozi katika serikali ya CCM?

Jambo la msingi na muhimu la kuzingatia kama kiongozi ananuia kwa dhati kuwa na chama cha kitaifa kweli kweli, ni lazima ahakikishe uongozi una mtandao wa kitaifa na kwamba yeyote anayechaguliwa au kuteuliwa awe ni yule mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake. Kama ni uchaguzi uwe ni wa uwazi na wa kidemokrasia. Naweza kujivunia kwamba viongozi wakuu wa CHADEMA wakati nikiwa Mwenyekiti walitoka kona zote za Tanzania Bara: Makamu wangu akiwa Brown Ngwilulupi toka Mbeya, Katibu Mkuu, Bob Makani akitoka Shinyanga, Makamu wake akitokea Mtwara na Mkuu wa Kitengo cha Wanawake akitokea Mbeya. Mwenyekiti wa Vijana alikuwa Freeman Mbowe. Kamati Kuu ilikuwa na wajumbe kutoka mikoa yote. Nasisitiza kwamba kiongozi makini hawezi kubagua watu wenye uwezo na kuwazuia wasichaguliwe eti kwa vile wana uhusiano naye wa karibu.

Mapato ya Chama
Miongoni mwa viongozi wakuu wa Chama kulikuwa na waliokuwa na uwezo kifedha ambao walikifadhili. Mmoja wa hawa ni Bwana Philemon Ndesamburo ambaye sio tu alisaidia sana Mkoa wa Kilimanjaro kama Mwenyekiti, bali hata Dar es Salaam aliweza kutupa ofisi tuliotumia kama Makao Makuu kwa miaka ya mwanzo. Mimi mwenyewe nilikaa Dar es Salaam kwa miaka yote sita nikiwa Mwenye Kiti, bila kulipwa hata senti moja kama mshahara, au kulipiwa kodi ya nyumba. Mara nyingi nilitumia magari yangu binafsi kwa mashughuli ya Chama nikinunua petroli au dizeli bila CHADEMA kunirudishia.

Viongozi karibu wote walijitolea magari yao kwa ajili ya safari za Chama mikoani, mara nyingi bila hata Chama kulipia gharama za petroli. Samani za awali ofisini zilitolewa kama zawadi na wanachama, na hata magari ya kwanza, mengi yakiwa sio mapya yalitolewa kama zawadi na wapenzi wa Chama, miongoni mwao wakiwa ndugu zangu wa karibu. Kama Makao Makuu yalionekana kwamba yanaendeshwa kwa kubana matumizi sana ni lazima ieleweke kwamba mapato yalikuwa finyu kwa vile ada za uanachama hazingeweza kukidhi mahitaji, hasa kwa vile tulitarajia kukua kwa kasi. Pale mwanzo ilikuwa ni lazima kila mwisho wa nwezi kukutanisha Wajumbe wa Kamati Kuu ili kutoa michango kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Chama ambao hawakuwa na kipato kingine.

Licha ya kwamba CHADEMA kimeweza kupata ruzuku kidogo miaka hii ya karibuni, mapato mengi ya Chama yameendelea kuja kutokana na wanachama kujitolea kibinafsi kwa vile ada za uanachama ni kidogo. Kwa hiyo ni lazima kudhibiti matumizi ili wafadhili wa ndani na wa nje waendelee kuwa na imani kwetu. Bwana Nesario anasema kuendesha Chama namna hiyo ni kukiendesha kama kampuni binafsi. Kama kudhibiti matumizi ni kuendesha Chama kama kampuni, basi hilo lilikuwa lengo letu. Anayetaka pesa za dezo na takrima abaki au aende CCM. Tunahitaji wazalendo walio tayari kujitolea kujenga chama mbadala kwa CCM.

Kueneza Chama Nchini
Licha ya unyonge wetu, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 1995, tuliweza kuwa na matawi katika kila wilaya, na mimi nikiwa Mwenyekiti niliweza kutembelea wilaya zote Tanzania Bara isipokuwa Ukerewe, Ngara na Makete. Itakumbukwa pia kwamba, kabla ya Bwana Augustine Mrema kuingia upinzani, CHADEMA kilikuwa ndicho Chama cha upinzani kilichoongoza kwa ukubwa na wingi wa wanachama. Itakumbukwa pia kwamba CHADEMA kilishindwa tu kuchukua kiti cha Ubunge cha Kigoma-Ujiji katika uchaguzi mdogo wa 1994 kutokana na mbinu chafu za CCM. Mahakama ya Rufaa ilibatilisha uchaguzi wa Azim Premji wa CCM na jimbo hilo lilibaki wazi mpaka Mhe Aman Walid Kabourou wa CHADEMA alipochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 1995.

Uamuzi ambao uliathiri mtandao wa CHADEMA kitaifa ni ule wa kumuunga mkono Augustine Mrema wa NCCR-Mageuzi mwaka 1995 na kumpigia debe ili awe Rais. Makubaliano baina ya CHADEMA na NCCR-Mageuzi ya kuachiana majimbo yalipuuzwa na Mrema na alifanya kampeni nchi nzima akisema yeye alikuwa "shoka" na NCCR-Mageuzi walikuwa "mpini", kwa hiyo Mbunge wake lazima awe mwana-NCCR-Mageuzi. Matokeo yake wana-Chadema waliopania sana kuwa wabunge walihamia NCCR katika dakika za mwisho wakitazamia kwamba kimbunga cha Mrema kingewavusha. Baadhi yao waliweza kuwa Wabunge, lakini kwa tiketi ya NCCR.

Wale tulioamini katika misimamo ya CHADEMA tulipania kukiimarisha baada ya ule Uchaguzi ambao ulitutupa katika nafasi ya tatu. Kuna rafiki yangu ameniambia kwamba kosa langu kuu la kisiasa ni lile la kumuunga Augustine Lyatonga Mrema mkono mwaka wa 1995. Nakubaliana na huyu rafiki, lakini pia mimi ni mtu ninayeheshimu maamuzi ya wengi, na ni CHADEMA waliamua kwa kura nyingi kidemokrasia na kwa uwazi kumuunga mkono Mrema.

Mrema hakudumu NCCR-Mageuzi, na baadhi ya wana-CHADEMA waliohamia NCCR walirejea chamani kwetu na wengine wakamfuata T.L.P. Hao wataangamia naye kisiasa kwa vile mahali alipo Mrema mihadi haiheshimiwi. Uchambuzi wa Bwana H.Nesario kuhusu chaguzi za 1995 na 2000, na waliochaguliwa Rombo, Vunjo, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Hai, Siha n.k. haukugusia uvurugaji wa mtandao wetu wa viongozi kutokana na Mrema kutojali makubaliano. Hata hivyo, naamini kwamba wazalendo walio makini wamejiunga sasa na CHADEMA na kwamba wanasiasa wengi wazalendo wa kweli wanaonuia kwa dhati kuboresha maendeleo ya nchi yetu, wataendelea kuimarisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika safari yake ya kuwa Chama tawala.

Kuimarisha mtandao wa CHADEMA nchi nzima ulianza tena kwa ari mpya mwaka 2004, hasa baada ya Bwana Freeman Mbowe kuchaguliwa Mwenyekiti na Dkt. Willibroad Slaa kuwa Katibu Mkuu. Wakishirikiana na Wabunge wengine wa CHADEMA wameweza kuweka mtandao imara na tumeweza kuweka wagombea wengi katika majimbo ya ubunge na udiwani kuliko wakati wote wa historia yetu pamoja na Freema Mbowe mwenyewe kama Mgombea wa kiti cha Urais.
 
Makala ya Mtei ya mwaka jana.....

Kuhusu Mgombea Mwenza

Kukerwa kwa Bw. Nesario na uteuzi wa Mama Anna Komu kuwa Mgombea Mwenza kwa maoni yangu kunaonyesha mawazo ya Mfumo Dume wa kizamani na uliopitwa na wakati. Hakuna mtu anayeweza kusema Mama Komu si mzaliwa wa Zanzibar. Kwa hiyo kisheria na kikatiba ana haki ya kugombea. Eti kwa vile ameolewa na mwananchi wa Tanzania Bara, basi anyimwe haki yake. Mbona hata Bwana Salmin Amour alioana na mwanamke wa Bara? Kuna mtu ameweza hata kutaja kwamba hakustahili kuwa Rais wa Zanzibar? Mbona Mama Magimbi aliyekuwa kiongozi wa Upinzani kati ya 1995 na 2000 alikuwa mzaliwa wa Zanzibar lakini ameolewa na Mtanzania wa Bara? Kuna yeyote isipokuwa Nesario ambaye angeweza kusema eti Mama Maghimbi hangestahili kuwa Makamu wa Rais endapo chama chake kingemteua na kikashinda? Mantiki za akina Nesario ni za ufinyu.

Uwakilishi wa Wanawake

Sio kweli kwamba ni mtu mmoja alichagua na kuandaa orodha ya Wakina mama wa CHADEMA watakaoingia Bungeni kwa uwiano wa kura. Mimi niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa jopo la wanachana waliochambua sifa za kila aliyeomba na tulitumia vigezo vya kisayansi kufikia orodha hiyo. Sijui huyu Nesario alipata wapi uvumi huo kuwa ni mtu mmoja alitayarisha hiyo orodha.

Kuhusu Kampeni za Sasa

Nafajirika sana na jinsi kampeni za sasa zilivyoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu na kwa uchambuzi wa kina wa matatizo yanayolikabili taifa letu. Hii iliwakera wakina Nesario mpaka wakalaumu Mtei na Ndesamburo kwa kuchangia. Nesario hata kaota ndoto kwamba ninaye mwanangu huko Marekani ambaye anasaidia kukusanya misaada na kuipelekea CHADEMA. Kwa wale watu wanaofadhaika na kukosa usingizi kutokana na CHADEMA kuwa tishio kwa CCM, mimi sina mtoto anayeishi Marekani. Wanangu niliowaacha Marekani kumalizia masomo baada ya kazi yangu kama Mkurugenzi wa I.M.F. wamerudi nyumbani; wa mwisho akiwa amerudi miaka saba iliyopita. Swali la kujiuliza ni kwa nini Nesario ameamua kuwa mzushi?


Edwin I. M. Mtei
P.O. Box 967
ARUSHA


Ps> huu ni mtazamo wa mzee mtei alioutua mwaka jana. Sehemu kubwa ya mambo aliyoyasema ni ya muhimu sana kwa mjadala wetu wa leo zaidi kuliko hata alipoyatoa wakati huo. Tuyajadili. Yapo mengi ambayo binafsi nayaunga mkono. Yapo ambayo nina mtazamo tofauti, mtausoma katika michango yangu kwani kuna developments nyingi toka yeye alipoandika makala mwaka mmoja uliopita mpaka sasa. Lakini pia yeye ni muasisi wa chama, yapo ambayo ulikuwa ni mtazamo wao wa wakati huo na kizazi kipya cha CHADEMA kinayo ya ziada pia. Nawatakia heri ya mwaka mpya

JJ
 
JJ Mnyika,

kwanza hongera kwa kuchaguliwa kwako na asante sana kwa mada za Mtei kumjibu Nesario

Pili naona hapa panahitaji ufafanuzi zaidi katika sehemu hii ya mada ya Mtei


"...................Uwakilishi wa Wanawake

Sio kweli kwamba ni mtu mmoja alichagua na kuandaa orodha ya Wakina mama wa CHADEMA watakaoingia Bungeni kwa uwiano wa kura. Mimi niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa jopo la wanachana waliochambua sifa za kila aliyeomba na tulitumia vigezo vya kisayansi kufikia orodha hiyo. Sijui huyu Nesario alipata wapi uvumi huo kuwa ni mtu mmoja alitayarisha hiyo orodha........................"


1.Mzee Mtei aliteuliwa...............
2.Ni akina nani walikuwemo ktk Jopo
3.Ni vigezo vipi hivyo vya kisayansi?

I like this para most

".......................Fursa ya kuunda chama mbadala kwa Chama cha Mapinduzi ilitulazimisha tubuni filosofia na sera ambazo zingeepusha taifa kurudia makosa ya zama za ujamaa zenye sera zisizo na tija na uendeshaji wa kiimla. Wananchi ni lazima waweze kuamua mambo yahusuyo maendeleo ya taifa lao kwa uhuru kamilifu, ujasiri na bila ya woga na kuepuka utawala wa kiimla. Rasilimali za nchi ni lazima zitumike kunufaisha wananchi. Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira yanayowezesha mitaji kuingia nchini. Uhuru wa soko ndiyo njia endelevu ya kuvutia mitaji ili raslimali za nchi ziweze kutumika kikamilifu, lakini papo hapo lazima umma wote ufaidike na mazingira yawekwe kuhakikisha wananchi wanajituma kwa kadri iwezekanavyo kupata kipato chao wenyewe. Wasiojiweza na ambao hawakupata ajira watadhaminiwa na umma. Miundombinu ya kiuchumi na ya kijamii itamilikiwa na umma na kuendeshwa kisayansi, kuhakikisha ni endelevu na ina tija. Miradi ya umma itabuniwa na kuendeshwa bila pupa za kisiasa..................................."

Though its not a mada here naomba niseme kidogo kuhusu Sera ya majimbo:
Juzi juzi nilipata taarifa za kuwa Mh Magufuli kurudisha wizarani pesa za maendeleo ya mradi wa viwanja huko Mbeya, sababu kubwa ni kuwa walishindwa kuzitumia (I liked his action). Najiuliza Je Magufuli anatumia sera za MAJIMBO kiaina kuonyesha accountability ya viongozi wetu? Nilitegemea wananchi wa Mbeya wangeandamana kutaka wahusika wafutwe kazi.

Nilikuwa Nigeria, na pia India, kusema ukweli nashawishika na sera za majimbo, kwani nimeshuhudia ACCOUNTABILITY kwa sana
 
I hope this answers some of Chinga's or Mtalii's questions.
Congrats kijana JJ.
 
wanabodi,
Mzee mtei kichwa safi sanaaaa!.. Na kweli Ogah kipande hicho hapo juu kinachotangulia na - Fursa ya kuunda chama mbadala!..

Kipande hiki ndiho nachokizungumzia kila siku. kila kukicha na ndicho pekee kinachonipa tumaini.
Isipokuwa Ogah hili swala la majimbo mshikaji, kwa nini bado hamuelewi tofauti kati yetu na hizi nchi nyingine mnazozitolea mfano?..
Je, Unajua kwamba Nigeria na India ni mataifa mapya yaliyoundwa baada ya kuyaunganisha majimbo yao?... Tanzania haikuwa formed kwa njia hiyo kwa nini leo sisi tuanze kuigawa nchi ambayo haikuwa na matatizo kama yao!. India na Nigeria walikuwa na matatizo ya Ukabila la tena India Kabila kwao ni DINI.. sasa wewe nambie kama kuna njia bora zaidi ya kulyaweka majimbo pamoja bila ya kukubali tofauti zao. Na unaona vita vyao haviishi kila siku!.. Pakistan, sriLanka na Bangladesh was part of India before!.. Unakumbuka?
Kifupi majimbo ya nchi hizi ni makubaliano ya tofauti zao, kwanza kisha maendeleo ya nchi nzima inafuatia...Na utakuta kila jimbo lina historia yake ya Kiutawala na hata baadhi ya sikukuu zao!... Do we want to go there?

Kitu kimoja tu ambacho kinajitokeza hapa ni kwamba Mtei ameshindwa kuyaona makosa ya Chadema ktk swala la familia ikiwa CCM nao wanafanya hivyo!...Pili, kuwa mwanachama na kushika madaraka ya juu kwa kuteuliwa (kifamilia) ni vitu viwili tofauti kabisa na viongozi waliochaguliwa hata kama wanatoka familia moja.
 
Fikiraduni.

Asante sana kwa offer yako, Umeme tunao wa kumwaga hivi sasa.
hata kama kusingekuwa na umeme nisingeondoka nchi yangu, vyeti vyangu vinaniruhusu kupata kazi sehemu nyingi na huwa nashinda interview zote za kazi, mimi sio kama wewe na wasomi wa Udsm mkikosa kazi hapa nyumbani mnakimbilia majuu, inajulikana kila interview mkiingia na vijana wa Mzumbe mnaambulia patupu.

Jawabu si kukimbia nchi ila mkiimarishe chuo chenu na sasa mmeingia kwenye biashara kwani masomo yamekushindeni. Bwana FD naomba nafasi ya banda hapo kwenye Mall yenu niuze maji ya baridi? kodi nitalipa ya miaka mitatu.

Mnyika.

Mitihani inaanza january 8 na Mbowe anamaliza ziara tarehe 5 january hapo kuna tatizo unless Tutor wake awe ni Fikiraduni.
 
David Cameron ametoa salamu za mwaka mpya na kusema chama chake anataka kiwe cha working class na si matajiri kama kilivyo. Chadema mnasemaje?
 
Fikiraduni uko wapi?
Soma makala ya Padri Karugendo- ufidhuli wa Marekani, poleni sana vijana wa Udsm huko ughaibuni.
Eid Mubaraka na nakutakia kheri ya mwaka mpya na wanabodi wote.
 
Tunaomba Katibu wa comission ya universities Tanzania-Wiliam Sabaya atufahamishe na degree ya Mbowe kama inakubalika?
 
Mbowe hajamaliza hiyo degree bado. Labda tuulize kama Hull ni chuo kinachotambuliwa na hiyo tume ya Sabaya. Ninavyojua ni kuwa Hull University is in good standing as an institution of higher learning in the UK.
 
Wacha.
Mbowe hasomi atanunua cheti tu. lakini anazuga yuko UK. na mara nyingi anajichimbia Hai atatumia ujanja huo kwa miaka mitatu halafu aje na cheti.
Hull hawawezi kuwa na mwanafunzi bomu na mtoro kiasi hiki.
 
Atapata cheti cha mwisho kwamba walimwona, hawawezi kumuumbua mzee mzima baada ya kulipa hizo £8000 na ushee kwa mwaka. watampa kitu.
 
.............
(b) Mbowe anajifua sasa hivi kupata shahada 2,
zilizoandaliwa maalum kwa ajili yake, within 3 years,
semi part time, kutoka vyuo vitatu tofauti, vilivyo
katika mabara matatu tofauti.
(Damn! doesn't this qualify as an entry in Guinness
book of record?)

By the way, mbona inatajwa Hull tu, hivyo vyuo vya
marekani na japan mbona havitajwi majina? au ni
mazabe?
.....

Mbali na Hull inayotajwa, vyuo vya marekani na Japan ni vipi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom