Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
So Mswahili: what is the issue here: huamini Mbowe kama anasoma Hull au una shaka na standing ya Hull as a credible university?

Wacha: Una ushahidi au precedence yeyote ya Hull kuuza vyeti? Unatambua athari za statement yako kwa reputation ya Hull University? I am just curious if you have any backing in making such a bold statement!
 
I stand by my statement not yours. I say what I know. it seems you do not know what you are talking about
 
Fikiraduni.
wapi baba? umemsikia Sawaya wametajwa Bukoba university.

unafiki wenu hasikilizi, Mzumbe tunazidi kupepea, naomba majibu au uko busy na kubebeba maboksi huko majuu?
 
sijui China yuko wapi

jamani CHINGA RUDI

exam pale Hull zinaanza tarehe 16 sasa huu ni muda mzuri wa kudurusu
 
Mswahili toa ushahidi kwamba Mbowe hasomi bali anazulula Hai. Umekwisha jidhihirisha wewe ni mzushi, awali ulizusha kwamba Mnyika alipata Div III nilikubishia,Chinga nae akaja kupotosha, jj amejibu, nashangaa upo kimya, sema ulikosea au uliteleza, ikiwa una historia ya upotoshaji inakuwa rahisi kuamini unaendelea kufanya kazi yako ya upotoshaji ambayo haina msaada wowote kwa taifa.

Ingekuwa vyema ukashambulia kwa hoja kama wengine walivyo fanya kwenye chopper,ukabila na Conservatives lakini wewe ni majungu na uzushi tu! Ndio maana hoja zao zinajibiwa, wewe unaleta ngonjera na kebehi zenje vionjo vya taraab, kwenye mijadala mizito ya kulisadia taifa, haifai! Hata wanao kosoa CCM watakuwa wanakosea kama wanawasilisha majungu badala ya hoja, Taifa haliwezi kwenda namna hii.Jenga hoja ndugu

JJ, Hongera kwa kuchaguliwa na kutoa majibu murua kabisa. Kazi nzuri, unajitofautisha na wanasiasa wengi, si wote wenye ujasiri na uwezo kufanya mijadala kwenye forum ya mijadala mizito kama hii
 
Ogah,
Nakubaliana na wewe nami pia huvutiwa sana na sera ya majimbo, naamini ni sera muufaka.

Sioni ni kwa namna gani sera ya majimbo italigawa taifa! Kama majimbo yataligawa taifa kwani mikoa isifanye hivyo? Yote si ni mifumo ya kiutawala tu? Na hakuna ulazima wa wa kugeza mfumo wa majimbo wa nchi nyingine, yataundwa kwa matakwa na na mazingira ya Tanzania.

Majimbo ni suluhisho kwenye mgawanyo wa rasilimali na ushiriki wa wanachi katika kuongoza nchi yao.

Mfumo wa sasa unazipendelea baazi ya maeneo kufaidika na rasilimali zao na kuziacha nyingine. CHADEMA inasema sehemu ya mapato ya rasilimali yatabaki na sehemu itakwenda serekali kuu.

Halmashauri za wiliya ya Ilala na Kinondoni zinafaidika na sera majimbo sasa! Kwa kutumia municipal levy, zinakusanya makusanyo makubwa kwenye halmashauri zao, makapuni makubwa mengi yapo Ilala na kinondoni, rasilimali kuu za wilaya hizi ni biashara, sasa wilaya nyingine kama Kahama na geita rasilimali zao si dhahabu, itakuwa vyema nazo zikiweza kufaidika na sehemu ya mapato ya rasilimali zake.

Maana kwa wilaya za ilala na kinondoni zinabakisha sehemu ya mapato ya kampuni kwa ushuru na sehemu iliyobaki inachukuliwa na serekali kuu kupitia coprate Tax.

isitoshe, kuwa karibu na rasilimali ni gharama.Watu wanao kaa karibu na mbuga za wanyama wanashambuliwa na wanyama mara kwa mara na wakati mwingine mali zao kuharibiwa hio ni gharama ya kuwa karibu na rasilimali, wale walio karibu na milima wanapigwa baridi kali hio ni gharama ya wao kuwa na rasilimali walio karibu na madini ardhi yao itaharibiwa vibaya, mazingira huchafuliwa sana na shughuli za usafishaji wa madini pamoja na moshi. Ipo haja ya kubakisha sehemu ya mapato kuwawezesha hawa watu kukabili gharama za kuwa na rasilimali.

Kama ilivyo kwa kuwa karibu na viwanda. Sera ya majimbo ni jibu murua. Hapa tungetengeneza miji mizuri mingi kwa kufuata mgawanyo mzuri wa rasilimali.

Mfumo wa sasa wa utawala una hitilafu. Kuna msongamano mkubwa wa vyeo pasipo kuwa na sababu.

Chukulia mfano wilayani, Kuna mkuu wa wilaya(politician),Meya(Politician), Mkurugenzi wa Halmashauri(Technocrat),Distric Adminstrative Secretary-DAS(Technocrat). Mkuu wa wilaya anateuliwa na Raisi na ana nguvu zaidi ya meya anaechaguliwa na wawakilishi wa wananchi(madiwani). Kuna haja ya kuwa na utitiri huu wa viongozi?

Sera ya majimbo itafuta ututitiri wa viongozi wa kuteuliwa na kurudisha madaraka kwa wananchi kwa kuchagua viongozi watakao wajibika moja kwa moja kwa wananchi.
 
Eric
Really, this Majimbo thing make a lot of sense than mfumo uliopo wa sasa
 
Ni woga wa mabadiliko ndio unafanya watu waogopa majimbo. Fear of unknown.
 
Kwa mtu anayefahamu, naona hili liliwahi kuulizwa lakini sijaliona naomba anyefahamu shahada anayesomea Mbowe pale Hull inaitwaje?
 
inabidi waheshimiwa muyabadilishe hayo mazungumzo kwanini mh mbowe amekosamtu wa kumfananisha naye?au basi afande sharp
 
Ongara na Ogah maneno yenu mazito,maandiko hayo si ya kusomwa tu, yanahitaji pia kufanyiwa kazi.Ninafarijika mno ninapoona watu wanajadili issues na sio MTU.

Kama binadamu kila mtu ana mapungufu yake!Tuangalie zaidi nini mchango wa muhusika ktk maendeleo ya wananchi, na sio kupoteza muda kubishana kuhusu exams grade za watu.Sipo hapa kufagilia watu,lakini ni ukweli usiopingika kuwa kijana kama Mnyika ni hazina kubwa kwa Taifa letu,ni mtu wa kujitolea, kujituma na kukubali kukosolewa, tusimkatishe tamaa kwa kejeli na maneno yasiyo na maana.

Tujadili issues zaidi,kwa sababu sasa forum imekuwa work Guide ya baadhi ya wakubwa waliopo serikalini, wanapata mengi na ya kweli kutoka humu.

Wale wenye datas tupeni mawe ili kijiwe kiendelee kuvuma!!
 
Ogah na Eric,
Swala la majimbo, Mimi na Sam tulimuuliza Mnyika kule bsctimes akashindwa kuja na jibu.
Freeman pia, sera hii ilitumiwa na CCM kama bakora kumnyanyasa na pengine kuzoa kura za watu wengi.

Hii sera ya majimbo haina kichwa wala miguu kwa sababu tatizo kubwa letu hasa ni la KIUCHUMI. Na RUSHWA (grand Corruption) ndilo gonjwa lenyewe kwa hiyo dawa ya gonjwa hili sio kubadilisha madakari na kupangua vituo vya afya.

Tumekwisha wapeni kwa undani zaidi nini kitaweza kujitokeza,tena kwa maelezo marefu zaidi ya mapendekezo ya Chadema na sera nzima.

Mnapozungumzia viongozi waliopo sasa hivi kuwaondoa mbona hamtuonyeshi huo utawala wa majimbo utakuwa na viongozi wa nama gani?

Kumbukeni tu majimbo sio mikoa wala wilaya...je, mnataka kutuambia mtawaondoa viongozi wa wilaya na mikoa?.. je, ktk sera ya majimbo ni wapi inaposema Mbunge atakuwa na sauti kuliko DC ama RC. Je, kila jimbo litakuwa na bunge?.. na what about bunge la taifa!.. sioni upungufu wa viongozi hata kidogo hali gonjwa letu ni rushwa... rushwa ndio adui wetu na njia zipi zitumike kuondoa rushwa otherwise Tanzania tunao utajiri wa kuliendeleza taifa zima.

Mimi napinga sera ya majimbo kwa sababu rahisi kabisa! Hakuna maendeleo yoyote ambayo hupatikana baada ya watu kuvunja ndoa!..wala hakuna maendeleo ya kifamilia ikiwa mke na mume kila mmoja wao ana maisha yake!

Pia urithi uliogawanywa kati ya watoto hauwezi kuongeza maendeleo ya watoto wote. Kati yao wapo ambao hawakubalikiwa kuwa na kipaji cha biashara!.hii ni mifano midogo sana ambayo sote tumewahi kuiona ama kuisikia.

Nitarudia kusema kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni kupenda kuiga sera za nchi za magharibi bila kuzingatia mazingira yetu..
Hii sera ya majimbo haina tofauti na kuacha swala la elimu kuwa mikononi mwa wahubiri wa dini!..wakati wenzetu Ulaya, shule inaweza kuitwa St Joseph lakini shule hiyo hairuhusiwi kabisa kufundisha dini ama hata kuendesha misa ama sala wakati wa masomo. Mbali na hapo hawa wenzetu dini sio moja ya matatizo ya jamii zao, nchi zao ama uhuru wao umepatikana kwa kupitia dini hizi.

Ni upumbavu mkubwa kutegemnea eti shule ya waislaam Tanzania inakayoitwa Al. Jazeera kutofundisha dini ama kuwatendea haki watu wa madhehebu mengine. Na ni ujinga zaidi kufikiria kuwa maendeleo ya watu kwa kutumia dini zao ni bora kuliko maendeleo ya wananchi wote kwa pamoja bila kujali dini ama rangi zao.
 
Maalim Mkandara.

ndio maana Chinga alikuwa anahoji uhalali wa hawa Chadema kushirikiana na Conservative kutokana na sera zao kuwa za ajabu sana na mara nyingi hazina maslahi kwa weusi.ila ndio mambo ya kuiga tena. mtu mzima akiona Chifupa katoa pesa kwa yatima nae atapeleka kanisani.
 
Bob,

Swali lako na sam nalikumbuka sana tangu kule bcstimes.

Mfano wako wa Seminari ni inapproprate, bse its a very small entity ndani ya mfumo mzima wa majimbo nilivyouelewa mimi.

Swali la msingi kabisa "a valid challenge", uliloleta ni
".............Kumbukeni tu majimbo sio mikoa wala wilaya...je, mnataka kutuambia mtawaondoa viongozi wa wilaya na mikoa?.. je, ktk sera ya majimbo ni wapi inaposema Mbunge atakuwa na sauti kuliko DC ama RC. Je, kila jimbo litakuwa na bunge?.. na what about bunge la taifa!..........." watu wengi tunajiuliza sana kuhusu hili, however the logic is simple and at the same time the project implementation is a big challenge and for those in favour should table the solution + myself

to me, this is a project on its own i.e to come up with structure ya majimbo. Sijui CHADEMA wameweka vipi (structural wise) kuhusiana na hii issue ya majimbo. Kama CHADEMA wanayo sioni ni kwa sababu gani walishindwa kukujibu wewe na sam kule bcstimes enzi zile. it would have been an easy question to respond, if they have/had everything in order.

Nikiangalia jinsi nchi yetu ilivyo, with 45 years old ktk system tuliyonayo, im afraid sehemu kama Mtwara, Lindi, Rukwa, Shinyanga and the like zitabaki duni kwa kila kitu mpaka Mesiah arudi!!

Nahisi, majimbo yatatufanya wananchi wengi tuuone uhuru na matunda yake ya kweli, na sio mazingaombwe ya kofia, tisheti, khanga na pilau yalivyo sasa

Kumbuka, mimi hapa najaribu ku "explore the reality" as you always put it.
 
Ogah,
Kwanza swala la shule umelielewa vibaya.. sikuzungumzia seminari bali mfumo wa kuweka elimu chini ya wawekeshaji ambao hakuna ukweli zaidi ya kusema chini ya wahubiri wa kidini.

That is a naked truth na sielewi serikali ilitegemea kitu gani inapotokea kuwa dini zinachukua nafasi ya mafunzo na elimu dunia nchini.

Kwa hiyo unapoweka majimbo lazima pia ukumbuke kuwa nia yako ni kuiendeleza Mtwara, Lindi, Rukwa na sijui wapi kwa sababu sehemu hizi zina rasilimali kubwa. Kwa kufanya hivyo lazima Mtwara wasimamishe maendeleo ya mkoa fulani tuseme Dar. Mtwara watasema hakuna sababu ya gas kwenda hadi Dar wala usafiri wa south kupitia Dar.

Pengine hata ushuru mdogo wa bandari kuliko Dar.. na kumbuka Mtwara ina makabila yake, dar pia Mzaramo na Mndengeleko atasema aaah! basi toka sasa mtu wa kusini lazima aingie Dar kwa visa (natania). Hao Dodoma na Singida ndio hata sijui niwaweke wapi ktk mapambano haya ya kiuchumi kwani hawana kitu kabisaaa!

Anyway my point ni kuwa kila mkoa utakuja na sheria zake. Kama unakumbuka wakati wa Nyerere madaraka mikoani tu tulifanya makosa kibao!.. Huwezi kuvuka na mahindi toka mkoa wa Iringa bila kibali maalum. Kila mpaka wa mkoa ama wilaya waliweka mageti n.k..Ilikuwa adha kubwa sana kwa wananchi.

Hapa kinachojitokeza wazi ni UONGOZI hatuna! Chini ya kiongozi kama Freeman ambaye ameweka malengo yake wazi kabisa ni rahisi zaidi kupata mabadiliko nchini chini ya system hii. Yaani tukimpata mtu kama Freeman anavyosema ina maana ni rahisi kwake kugawa utajiri wa nchi. Kuweka watu pale anapoona pana hitajika na rahisi kwake ama chama kuondoa RUSHWA.

The boss has said! bahati mbaya hatujampata KIONGOZI hadi sasa ktk system hii ya Udikteta,(naomba mnielewe hapa tafadhali).

Chini ya majimbo, Kilimanjaro wakiiba ama kupendelewa hakuna hakimu maadam wanalipa fungu la taifana mbunge ama kiranja ni Mchagga. Haya Marangu na Machame unajua tena, visa vitaanza kujitokeza... kwa sababu maliasili fulani iko wilaya fulani kwa nini huyu Mchagga wa.. anapeleka mali kwao?. From majimbo tutaanza kuangalia mikoa na mwisho Wilaya kujitegemea!

Nchi zote zilizojigawa zilianza hivi hivi kwa kutumia mapungufu ktk Uchumi wao kuwa sababu ya kuweka Utawala mpya.. hali solution ilikuwa ni kuukataa uongozi mbaya wa kiuchumi (RUSHWA) unaotenga watu ama kuwaibia watu.
 
Bob,

Majimbo ni mfumo wa Utawala.

Umesema
"................Chini ya majimbo, Kilimanjaro wakiiba ama kupendelewa hakuna hakimu maadam wanalipa fungu la taifana mbunge ama kiranja ni Mchagga. Haya Marangu na Machame unajua tena, visa vitaanza kujitokeza... kwa sababu maliasili fulani iko wilaya fulani kwa nini huyu Mchagga wa.. anapeleka mali kwao?. From majimbo tutaanza kuangalia mikoa na mwisho Wilaya kujitegemea!..........."

na Si lazima uwe na majimbo ndio hayo uyasemayo yatokee!!. mapinduzi ya kiserikali ktk nchi kadha wa kadha yametokea na hawakuwa na majimbo. the point is, kuwa na majimbo hakuashirii mgawanyiko kama wengi wanavyofikiri.

Nielewavyo mimi, majimbo yatajumuisha mikoa kadhaa ku-form Jimbo, ambalo litakuwa na utawala wake, as for the structure ya uongozi na za kiuchumi ndio la kujadiliwa na kuwekwa sawa.
nakumbuka madaraka mikoani, wakati ule wa mazao kutovushwa kutoka mkoa hadi mkoa, the idea was brilliant!!, implementation ndio ilikuwa tatizo letu, kama ilivyokuwa maduka ya ushirika, na hata kwenye sera zetu nyingine nzuri tu leo hii tatizo limwkuwa ktk implementation.

Kuhusu Singida na Dodoma kuwa hawana kitu................sasa basi ktk mfumo uliopo sasa ndio kabisaa maendeleo watayasikia ktk bomba, kwa sababu "strategically" hakuna atayekubali ku-invest sehemu isiyo na matumaini ya return. ngoja nikupe mfano mdogo tu. Juzi juzi Magufuli alirudisha/alichukua pesa za maendeleo ya mji wa Mbeya kwa kuwa hawakuzitumia, suprisingly wananchi wa Mbeya sijui wamelala au sijui vipi (labda shibe ya viazi na maharage). let say mgao huo ndio ungekuwa wa kuwaletea maji kuulee kijijini Singida/Dodoma halafu urudishwe kama ilivyotokea Mbeya, i bet you viongozi watakoma kuzaliwa!!

In Nigeria for instance
Maana najua mtu atajiuliza kinachoendele huko "Majimbo". Nimeishi huko, naelewa kilicho, kinacho na kitacho endelea. Its a long story and the problems is not majimbo at all. MATATIZO MAKUBWA kwa uzito wake ni kama ifuatavyo....(Muulize Mnigeria yeyote atakubaliana nami)

1.RUSHWA
2.UKABILA
3.UDINI

majimbo sio tatizo!!

Tanzania yetu:
1.RUSHWA ipo sana
2.Ukabila - Hakuna
3.Udini - Hakuna

Kinachotakiwa ni UONGOZI THABITI (ambacho tunamiss) katika majimbo na serikali kuu na usio na mawaa hayo hapo juu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom