Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
wanabodi,
Jamani maswali mlouliza magumu sana, wala sii jambo la kurukia likaja tafsrika vibaya. Kumbukeni linaloandikwa humu ni rekodi ambayo watu mtakuja wasuta kesho.

Shukran za dhati kwa Chinga kwani katupa vitu ambavyo sasa vinawasumbua vichwa Chadema na ndivyo inavyotakiwa sio kuuliza maswali rahisi ambayo mtu anaweza kuyajibu bila kupitiwa na wazee!

Tuwapeni Muda watakuja tu hawawezi kuzama moja kwa moja kwani hili sasa hivi ni donda kwao!
 
Mtalii,

Sasa naanza kushawishika na waliosema wewe ndiye Chinga. Kama hivyo ndivyo karibu sana ndugu yangu. Naona hujatia neno katika hoja nilizitoa kuhusu chopper. Nadhani sasa naweza kuendelea na hoja zingine.

Ila umeendelea kusisitiza uwongo(huwa sipendi kutumia neno hili) kwamba Mbowe alikuwepo Moshi kutoa misaada. Nimekwambia Mbowe hakuwepo Moshi wakati ule, misaada ilitolewa kwa niaba ya Grace Kiwelu(MB), gazeti liliripoti vibaya. Sasa kukanusha au kutokanusha hilo ni suala lingine na hasa ukizingatia habari imepita muda kidogo. Unaweza kuwasiliana na muandishi wa habari hiyo Ali Sonda 0784 329429 kwa ufafunuzi au wasiliana na gazeti husika.

Mbowe amerudi Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya ziara zinazoanza kesho. Raha ya mijadala ni watu kukubali ukweli sio kuendelea kung'ang'ania uwongo la sivyo maana ya majadiliano inapotea!

Mkandara na DrWHO

Maswali yaliyoulizwa si magumu ila ni mengi yanayohitaji muda kuyajadili. Sasa kuna mambo mawili yamenishika mkono: Mosi, tuko kwenye hekaheka za maandalizi ya ziara mikoani. Infact viongozi wengi sasa wako field. Kwa hiyo kuna mambo mengi yapo mikononi mwangu kwa sasa. Pili, hii ni Xmas, nawakatikia heri mjazwa upendo, jitihada, mafanikio na furaha. Mara baada ya mapumziko nitaendelea na mjadala. Lakini kwa sasa kwa kuwa hoja zilikuwa nyingi na naona wapo wanaotaka nianze na family bussiness wengine uhusioano wa CHADEMA na conservative(na chagizo za DrWHO kuhusu realism!). Ipi nianze nayo?

Lakini fahamuni kuwa mpaka sasa hakuna hoja ambayo CHADEMA kama CHADEMA tumeifanyia kikao cha kuijadili kati ya hoja zilizosemwa humu. Bado hoja za humu ni maoni yangu binafsi. Ikitokea siku tukaamua kutoa tamko rasmi kabisa kujibu hoja nitawajulisha.

But nakubaliana na wewe Mkandara-walatini wanasema Scriptura maneti(kama bado nakumbuka spellings) kwamba 'maandishi hubaki'. Hivyo lazima niwe makini kiasi katika kuchangia hoja.

Na hii ni tofauti yangu kati Mtalii, DrWho na wengine. Mnaouwezo wa kuandika chochote,vyovyote,popote wakati wowote.

Mimi Mwenyekiti wangu yuko hapa(in a light touch) na wapinzani wangu wamejaa tele....Teh teh teh teh...

Once again, Happy holidays!

JJ
 
Its almost two months since i asked you two simple questions but looks like you cant cme up with a straight answer!

anyways

i will be more than happy if you would confirm if your Chairman is a realist

then asnswer in depth about the relationship between CHADEMA and CONSERVATIVES


Its my hope you will be back soon
 
Mnyika.

Naomba ujibu hoja kila siku unaleta dharura ili hali wewe ni mtoto wa kiume mara kuna kikao mara kuna nini, ni wewe uliyeahidi kujibu hoja zote tarehe 5 hadi leo imekuwa hadithi tu.

kunilinganisha mimi na Mwanaume Chinga boy aliyewatoa kamasi chadema kwa kweli nafarijika sana umenipa cheo kikubwa sana, ningekasirika kunifananisha na mtoro wa shule au kuniita mwanachadema.

tunaomba namba ya Grace Kiwelu hapa tu confirm kama mwenyekiti Mbowe alitoroka shule, huyu Sonda mmeshamuweka sawa tunalijua hilo.

vipi biashara ya dhahabu mbona una kwepa?
 
Kwa maneno ya Mzee ES "Siasa.....Kaaaaaaaaaaazzzzzzzziiiiiii Kwellllllllliiiiiiiiiiiiiiii
 
Hivi mtalii, wewe ni mwalimu wa primary school au? Kutoroka shule katika chuo kikuu ni kitu gani hasa hicho?

Yaani wewe ndo kina Goliati wasioamini hadi waguse? Mbowe alikuwepo chuoni ndugu yangu, achana na hii hoja. Twende mbele.

JJ achana na kutoa ahadi kuwa utajibu hoja tarehe fulani; ukipata nafasi teremka. Kwa nini ujifunge kwa ahadi?
 
Mwanasiasa.

Mbowe ni kiongozi na kuwa mtoro iwe primary au university ni noma. huo ni ushuhuda kuwa chama chenu elimu haina umuhimu.

hushangai hata kufuata deadline mnashindwa?

Mnyika anadai nitajibu siku fulani anaingia mitini kwa vile hafanyi kwenye chama kama taasisi yuko kwenye NGO hana deadline jee mtaweza kutuongoza? hoja za Chinga zina miezi sasa muda wa kujibu haupo. chadema kina majimbo mawili tu ya uchaguzi hakina muda wa kujibu vipi mkipewa nchi?
hapo mnajichanganya na kutupa faida sisi kujua hamko serious ni wasanii tu wa mjini.
 
wewe umeshaambiwa zaidi ya mara kumi na zaidi ya watu watano kuwa Mbowe alikuwepo chuo, hicho unachong'ang'ania hasa ni kipi?
 
Mwanasiasa.

Naomba niambie hao watu watano walioniambia kuwa Mbowe yuko shule.

Chinga aliweka namba za chuo na tulipiga na kuambiwa hayupo na hakuna aliyekuja na jibu. leo chuo kimefungwa unadai alikuwepo chuoni.

Mwanasiasa usiwe na siasa za jazba kiasi hiki unahaki hadi kwenye kuandika?
uta jazbika sana utakapokuja kujua uko kwenye NGO.
KUMBE ndio maana Chinga alituambia ulipitia vyama vingi sana hii kutokana na jazba ulizo nazo.
Noma ndugu yangu kuwa na kiongozi mtoro hamuoni Sumaye pamoja na wizi wake kaamua kula kitabu.
 
unajua kupata hii info kama Mbowe alikuwa Chuo aha hakuwa huo ni rahisi sana

ni kiasi tu cha kujua kama aliattend seminar katika tarehe hizo then ukweli utajulikana na uwongo utajitenga

na kupata info hiii si kazi kabisa








MR MNYIKA


I am still waiting for my answer and i wonder whats taking you this long
 
Haswaaa DR.Who
hawa hawajui attendance ni sehemu ya kusoma.
tunakushukuru kwa kutuwekea timetable ya Hull university iliyoonesha Mbowe kakacha vipindi.
 
basi usipate tabu sasa lete tarehe ambazo unawasi wasi kuwa bwana Mbowe hakuwa shule


mimi naweza kupata info zaidi ili kuliweka hili sandukuni
 
Kwani akiondoka shule lazima aage jamani?! Sidhani kama kuna mambo kama hayo kwenye asasi za elimu ya juu.

Kwani kama alikuwepo shule lakini siku hiyo hakuingia darasani?!
 
kolosig.png
 
Kwani akiondoka shule lazima aage jamani?! Sidhani kama kuna mambo kama hayo kwenye asasi za elimu ya juu.

Kwani kama alikuwepo shule lakini siku hiyo hakuingia darasani?!

Jamani huku majuu unapokuwa kwenye sehemu yoyote iwe ofisi, taasisi ya elimu, bungeni lazima ieleweke upo wapi na wewe ni nani.

Sababu ni moja tu ajali ikitokea au moto ni lazima wote mjulikane mpo wapi ndio sababu kama hukutokea i.e. chuoni itaonyesha hukuwepo pale hivyo sio kitu ambacho ni cha ubabaishaji.

Kuna wale wanaolipua mabomu bila taarifa hivyo roll call ni kawaida.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom