Wapendwa,
Naona bado mjadala wa chopper unaendelea, mpaka tuamua kuuweka pembeni mjadala huu kwa muda ndio nitaingia mjadala wa family business na mingine.
DrWHO,
Nimeshindwa kukuelewa. Soma post yangu vizuri. Hakuna sehemu yoyote niliyosema mimi nafanya consultancy CHADEMA na kulipwa dola mia kwa siku. Consultancy ni kazi zangu za binafsi, si za CHADEMA wala si kwa CHADEMA. Soma vizuri tafadhali
Mvuvi,
Nashukuru kwa mchango wako, but I am afraid if a respond to every issues you have raised we will derail the trend of the current discussion. Ila suala moja. Si kweli kwamba Mbowe aliingia gharama kubwa kuwa na mikakati ya wazi ya kuwakomboa watanzania!. Kwanza tuondoe dhana ya Mbowe kwa kuwa unakuwa huvitendei haki vikao vya chama. Uamuzi wa kutumia helikopta ulifanywa na vikao vya chama kuanzia sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu ambao naamini wengi wenu mliona kupitia kipindi maalum tulichokirusha kwenye TV.
Kwa hiyo CHADEMA iliamua kutumia milioni 200 kwenye helikopta, ambayo haikuwa inatumiwa na mgombea urais peke yake. Mathalani, Badala ya kupewa laki 4 za kunisadia kwenye kampeni kitendo cha kuelekeza pesa hizo kwenye chopper kilisaidia kuvuta kundi kubwa la watu Mbowe alipokuja Ubungo lakini pia image ya chama kwa ujumla ilikua. Lakini kwa upande mwingine Chadema iliamua milioni 500 zitumike katika mikakati mingine wakati wa kampeni ambayo kwa kiasi kikubwa ilielekezwa wa wabunge.
Ukweli ni kuwa chama kilifanya realistic evaluation kabla na wakati wa kampeni na kugundua majimbo ambayo tulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda, haya tuliyaita red na yalipewa raslimali zaidi ikiwemo mabango kwa wagombea na hata sehemu kiasi ya pesa. Na targeting yetu ililipa kwa kuwa haya ni majimbo yanayochangia zaidi hata katika ruzuku ya chama kwa sasa.
Mkandara.
Umerudia tena swali lako la siku zote| Kwa nini CHADEMA haikuchukua dola pamoja na heka heka zote hizo?Kwanini CHADEMA ilishika nafasi ya pili nyuma ya CUF? Hili ni swali pana, unaniruhusu nitulie nikufanyie uchambuzi kabla kujibu suala la family business?
Lakini nikueleze kwa ufupi tu]
Mosi, nakubaliana na Ongara kwamba matokeo ya 2005 hayakuwasilisha hali halisi ya ridhaa ya watanzania. Na mimi ni mhanga wa hili katika jimbo la Ubungo. Soma tamko la CHADEMA kuhusu uchaguzi(
www.chadema.net) litakupa picha ya nini kilitokea. Ukitaka kujua kama hawa jamaa hawakushinda kwa kishindo kama ilivyosemwa angalia mshangao wa kikwete kuhusu matokeo lakini angalia pia jitihada wanazofanya kuua upinzani. Hiki kama wangekuwa ni chaguo la wananchi kwa asilimia zaidi ya 80 wangehangaika kiasi hiki kuvunja upinzani badala ya kutimiza ahadi zao kwa wananchi?
Pili, CHADEMA ilipata mafanikio katika kura. Na si kwa sababu ya chopper tu, ni chopper na mikakati mbalimbal. Na mafanikio hayo yamekuwa kwenye kura, ruzuku etc kama ifuatavyo..
CHADEMA imezidi kupanda Kisiasa: CHADEMA kiliendesha kampeni zenye ufanisi zaidi ukilinganisha na miaka mingine. Ongezeko la wagombea wazuri, ubunifu wa kutumia helikopta katika kampeni na utamaduni wa kuendesha siasa safi zinajozikita katika ajenda/hoja vilipandisha chama kisiasa. CHADEMA ilijitofautisha kwa kiasi kikubwa na vyama vingine kisera kwa kutilia mkazo sera ya mabadiliko ya mfumo wa utawala ikiwemo uundaji wa serikali ya majimbo. Chama kimepata mtaji mzuri wa kisiasa kutokana na uchaguzi mkuu 2005 mathalani kufahamika kote nchini, wapenzi na wanachama wapya, wagombea nk.
Pamoja na kushindwa sanjari na kupata matokeo ambayo hayakulingana na jitihada na kukubalika kwa chama, CHADEMA imekua zaidi kisiasa katika uchaguzi mkuu 2005. Chama kimeongeza idadi ya wabunge wa kuchaguliwa kutoka 4 mpaka 5 na kuongeza idadi ya kura za ujumla za ubunge kutoka asilimia 4.23 mpaka 8.2. Hili ni ngezeko la takribani asilimia 100.
Hii imepelekea chama kuwa na wabunge wa viti maalum 6 kutoka 1 na kufanya jumla ya wabunge wa chama kuwa 11 kutoka 5 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 110. Ruzuku ya chama imeongezeka kutoka milioni 5.6 kwa mwezi mpaka milioni 35.5 na hivyo kutoa nguvu nyingine ya chama kuweza kujijenga kisiasa. CHADEMA ilisimamisha mgombea Urais kwa mara ya kwanza na kushika nafasi ya tatu. Jumla ya madiwani imeongezeka kutoka 64 mwaka 2000 mpaka 99 katika uchaguzi 2005.
Kwa upande wa Zanzibar chama kimeweza kusimamisha wagombea wengi zaidi kuliko chaguzi zingine na kushika nafasi ya tatu katika kura za ubunge katika majimbo mengi na kujitambulisha kama nguvu ya tatu katika siasa za visiwani. Matokeo haya mazuri yamepatikana kwa raslimali kidogo ambazo chama na wagombea wake walikuwa nazo katika uchaguzi. Kwa ujumla kampeni za CHADEMA zilitumia shilingi 753,786,505. Katika fedha hizi shilingi 223, 030,726 zilikuwa gharama za helikopta.
Hii ni ukiondoa gharama ambazo zilitumiwa na wagombea binafsi pamoja na wapenzi wa chama moja kwa moja katika maeneo yao
Tatu, umesema kwamba CUF hawakutumia nguvu yoyote lakini wameshika nafasi ya pili. Mimi si msemaji wa CUF, naomba vijana wa CUF waibuke hapa na kutoa takwimu ni pesa ngapi chama chao kilitumia. Nijuavyo mimi CHADEMA kilikuwa chama cha tatu kwa matumizi ya pesa, CCM kwanza, CUF pili. CUF ilitumia pesa nyingi zaidi sana ya CHADEMA. Ndio maana nasisitiza, CHADEMA imesema imetumia pesa ngapi, na vyama vingine viweke wazi basi matumizi yao. Nisingependa ninukuu kutoka habari za ndani kwako. Nataka itoke midomoni mwao.
Nne, umesema kitu gani kimeishusha CHADEMA wakati it was a name kabla ya chopper. Hii nayo sikubaliani nawe,hata ripoti za waangalizi wa uchaguzi zinataja chopper kama baadhi ya mambo makuu yaliyompandisha chati kiasi kikubwa Mbowe na CHADEMA.
Tano, linapokuja suala la kuzidiwa idadi wa wabunge katika bunge la muungano hapa kichofanya CHADEMA izidiwe ni Pemba factor. Otherwise CHADEMA ndio ingekuwa official opposition!
Sita, your basic question remains, if all that kwa nini CHADEMA imeshika nafasi ya tatu? Soma tamko la CHADEMA utapata baadhi ya majibu
http://www.chadema.net/uchaguzi/ripoti1.php Tatizo ni kuwa watanzania walioipenda CHADEMA waliipenda weeee mpaka wakawa na matarajio yaliyozidi mipaka.
Mimi nikupe mtazamo wangu
1. Historia, tazama 1995, 2000 vyama vipi vilikuwa vya kwanza,pili, tatu na nne? Ukweli ni kwamba kabla ya 2005 CHADEMA haikuwa na nguvu ilizokuwa nazo 2005. Hii inamaanisha ni nini, CUF ilisha invest kwenye uchaguzi wa 2005 kabla ya mwaka huo hususani mara baada ya uchaguzi 2000. Hii iliwafanya wawe na mtandao maeneo mengi na kuokoteza kura country wide,hivyo pamoja na kukosa mbunge hata mmoja kwa nadharia ya haba na haba ni wazi kwamba wangeweza kuizidi kura CHADEMA ambayo haikuwa na wagombea kila mahali katika nchi hii. Na ushahidi mwingine, wa mtaji huo ni matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2004. Infact investment na mtadao wa CUF haulingani kabisa na matokeo waliyoyapata. Hivyo historia hii imeshaanza kubadilika watch 2009 na 2010.
2. hii inazaa sababu ya pili, mapungufu ya CHADEMA katika baadhi ya maeneo. Ukweli ni kuwa the new CHADEMA ni product ya kazi iliyaonzwa kufanywa na ziara za wabunge 2003 na kuzaa mabadiliko ya uongozi yaliyowaingiza wakina Freeman kwenye uongozi mwaka 2004 tu. Wengine tumeingia CHADEMA mwaka 2005. Kwa hiyo tulikuwa na less than a year ya kujiandaa. Kwa kipindi hicho kufupi tu cha maandalizi tumefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya tatu na kufanikiwa kiasi ambacho nimedokeza hapo juu. Sasa tunamiaka mitano ya kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi ujao tukiwa na raslimali nyingi zaidi unategemea matokeo yatakuwaje? Unategemea CHADEMA itashika tena namba tatu?
3. Ukweli unabaki pale kuwa CHADEMA ndio chama pekee kikubwa cha upinzani kilichokuwa. Kwa hiyo ni chama kinachokuwa wakati upinzani kwa ujumla wake unashuka. Changamoto ni kuziba hii vacuum na kubaki kuwa na strong opposition kwa maslahi ya taifa na hatimaye kuweka madarakani alternative government.
4. Ni chama kipi cha upinzani kinachoonyesha matumaini ya kuwa alternative party Tanzania? Mashambulizi ya dola sasa yanaelekezwa wapi kwa upande wa bara?
Hii ni changamoto kwako na kwangu..
JJ
Ps. Mnaniruhusu sasa niingie kwenye hoja ya family business?stay tuned!