Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mwanasiasa, umejitahidi sana kuitetea Chadema, na nina hakika kama kweli wewe ni mwanachama wa Chadema utaanza pia kujiuliza kukoje huko kwenye chama!! Yaani sielewi, "Priority" list - huyu kijana Mnyika hakustahili kuwemo kwenye hiyo list? Na wale wazee ambao miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakiwatoa akina Mongela na Msekwa jasho hawakustahili? Au hii priority ilikuwa ni kwa wanawake tu? Tuseme kweli hakuna wanawake wenye sifa na uzoefu zaidi ya hawa? Maneno ya Chinga yanazidi kuwa na uzito zaidi.

Tusisahau, ruzuku za vyama na mishahara ya waheshiwa bungeni ni jasho la walala hoi. Kama kweli 'Discussion Boards' kama hii zitakuwa na maana yoyote kwa Mlala Hoi, aina ya uozo kama huu ndio unaofaa kupigiwa kelele hadi mabadiliko ya kweli yapatikane. Hiyo CCM yenyewe muda wake wa kuvunjika vipande vipande umewadia sasa; lakini naona hakuna chama cha ukombozi kilicho tayari kuchukua utawala!
 
Mzee Mwanasiasa,

Point yangu ni kwamba, siasa ni mchezo mchafu sana na unachezwa siku zote na watu wachafu sana, kwa mantiki hiyo, ninasema kama CCM inayajua yote haya maovu yenu yanayosemwa hapa, basi katika kampeni za uchaguzi huwa kuna kutoa uchafu wa upande wa pili, ambao hukusanywa kwa juhudi zote hata kama ni kuua mtu, yes!

Sasa ukishakusanywa huwa unapimwa, upi unafaa kuutoa publicly na upi haufai, but, huu usiofaa huwa unafanyiwa kazi rasmi, na hapo ndipo Mzee Nchimbi anapoingia kazini, yaani kuusambaza kwa kichini chini, kwa kugonga nyumba moja hadi nyingine kwenye nyumba kumi kumi, na kuutoa uchafu huo, sasa CCm haiwezi kusema hadharani kuwa huko kwenu kuna uongozi wa kifamilia, badala yake wataenda nyumba kwa nyumba, na ndiyo iliyokuwa kazi ya Nchimbi katika uchaguzi uliopita, sasa I do not care about this guy na mapunguf yake kisiasa au kiuongozi, but my brother it worked,

Na huu ndio mchezo alioufanya Bush, mwaka 2000, walipita nyumba hadi nyumba huko South, na kuwaambia wananchi kuwa Joe Liberman, ni Myahudi sasa atakuwaje makamu wa rais, maana akiwa Mossad itakuja kumuuua Gore, ili Liberman awe rais, na hawa Wayahuddi watawale vizuri nchi yetu, si mnajua kuwa huwa wanatawala Hollywood, na ulipokuja uchaguzi wa mwisho wakarudia tena kuwa Kerry, anataka kuidhinisha ndoa za mashoga, sasa ndugu yangu inasadikiwa watu wote huko South walienda kupiga kura kwa Bush kwa kuogopa hayo matisho, sasa huu uchafu Bush hakuutoa hadharani maana ingekuwa politically incorrect, ndio mchezo aliotumia Nchimbi huu sasa mimi nilifikiri ilikuwa sio haki, kumbe ni kweli mnao huu uozo ndani ya chama chenu, Nchimbi na jamaa zake alipita nyumba hadi nyumba kutoa huu uozo huko vijijini ambako mpaka leo wananchi hawajui kuwa Mwalimu hayupo, wakaamini,

Maana ndugu yangu mahesabu yote yalikuwa yanaonyesha kuwa JK hawezi kupita Kaskazini, sasa what happened? Ninategemea unanilelewa ndugu yangu, nina heshima nyingi na Freeman, kwa sababu angweza kukaa nyumbani na kula hela zake, badala yake akaingia kwenye huu mchezo mchafu, lakini kumbe na yeye ni another CCM, yaani manpena uongozi mtoto wa Ndesamburo, mahawara, yaani mnatia aibu, angalau CCM Makamba hajaingiza kimada chake, yaani puh! kisiasa mnanuka kuliko CCM!

Posting ya tafit mpaka leo bado mnahangaika nayo, na sasa inaoenkana Chinga alikuwa na hoja nzito na nilisema toika mwanzoni kuwa kuna hoja za kujibiwa, yaani mpaka mahawara wa Kabwe nao wanapata ubunge, Mwanasiasa mnanuka kuliko CUF na udini wao!
 
Nungwi,

Nilisema kama JJ alikuwa kwenye "team" anayo haki. Unatakiwa ujue kitu kimoja, leo hii Bill Gates akija kama consultant wa serikali kuhusu software developments for govt offices use, utasema safi na sawa huyu jamaa anafaa, swali je anayo hata degree moja?!?, hapo ndio nasemaga sometimes afadhali unyamaze, Jasusi amekuuliza je akija mtafiti kutoka india kutafiti dawa za kienyeji kule Ukerewe, je mganga wa jadi anayempa maelezo anaitwa nani hapo? sio Consultant?!?

Ndugu kabla ya kutoa maoni humu tunafikiria kete ya kusogeza baadaye, hatuwi tumetawaliwa na ubinafsi na sifa zisikuwepo.

BTW naona umeme unakutesa sana ndugu yangu mara upo mara haupo🙂 nipe CV nikuvute mshkaji hahahhahahah, tuma hapa:

FDreal@gmail.com

FD
 
Jasusi' Fikiraduni

Nafikiri hapa hamjadili nini hasa maana ya consultant bali ni ku-justfy kuwa JM alikuwa ni consultant kwa sababu alilipwa dola 100 kwa siku. Swali ni je kiasi ambacho mtu analipwa ni kipimo cha kuwa consultant. Jibu lake ni hapana.

Kumfananisha na mtu ambaye ana utaalamu wa miti ni tofauti kidogo kama mtaalamu kutoka mars akija na ana utaalamu wa kuandika hiyo report na kukubalika na wataalamu wengine anaweza kumtumia huyu mtu aliyebobea kuhusu miti lakini hawezi kuyaweka masuala yake kwa nyenzo zinazokubalika hivyo ataweza kuajiriwa ili mawazo yake yakubalike kitaaluma hivyo huyu mbobeaji hawezi kuwa consultant ataitwa msaidizi wa consultant kwani anamsaidia mtu ambaye ataweka mawazo yake katika upeo unaokubalika katika jamii kama consultant.

JM alifanya kazi kama msaidizi wa consultant kwa maoni yangu na hakuwa consultant labda kama yeye mwenyewe akitueleza alifanya nini hasa, mfano kama yeye ndiye aliandika hayo maripoti kitaaluma n.k.

Nafikiri tuache hilo hadi mwenyewe atuambie lifanya nini hasa bila kuendelea na justification ambazo hazina msingi na kudharau taaluma ya ma-consultant au la vinginevyo ni jina tu lilitumika ili kuweza kulipwa chochote.
 
Mchumba wa Zito mbona anajulikana? Na juzi tu, mwezi huu, amejifungua mtoto wa kiume, akapewa jina Chachage. Acheni hizo. Mchumba wa Mhonga mbona yupo? Msiwachafue watu bila sababu...
 
Jamani mi sidhani kama Mtu anayetakiwa kuiendesha nchi ni lazima awe na madegree na mashahada juu, kwani kuongoza nchi ni swala la mtu kuelewa ukweli wa mambo mfano kujua matatizo ya jamii unaiyoiongoza.

Hivyo basi kusema Mbowe na Amina CV zao hazijashiba sidhani kama inaleta mantiki yoyote when it comes to kuongoza nchi.
 
...hata CCM pia inageuka kuwa family business. Tumeshuhudia familia za kina Mwinyi,Kawawa,Karume,Malecela etc nao pia wamejaza watoto wao ktk chama.

sioni ubaya wowote ule wa viongozi wa chadema kuamua kuchumbiana. jambo hilo siyo geni, na mara yangu ya kwanza kulisikia ilikuwa ni CCM.

vilevile, kutokana na wingi wa wabunge wa CCM, basi tatizo la wabunge "kuchukuana" ni kubwa zaidi ndani ya CCM kuliko Chadema.
 
Mzee Joka kuu,

Heshima mbele, the issue hapa ni Chadema na family business, sio CCM maana hiyo tunaipiga mwe hapa kila siku, ila at moment ni Chadema ndiyo iko mahakamni hapa!
 
Mzee ES,
inawezekana Chadema wameiga toka chama tawala. hii tabia ya ngono miongoni mwa viongozi/wabunge haikuanza leo, imeanza na waasisi wa CCM na inaendelea mpaka leo ktk chama.

tuwape muda chadema wajijenge. kwa jinsi ccm ilivyo na mabavu upinzani Tanzania Bara lazima uanzie kilimanjaro na kusambaa mikoa mingine.

mimi naamini kilimanjaro ni kati ya mikoa michache tanzania bara ambako wananchi wanaelewa thamani ya kura yao wakati wa uchaguzi. kilimanjaro mbunge usipo-deliver basi uchaguzi unaofuatia hawakupi kura. wananchi wa tanzania nzima wangekuwa na jeuri kama kilimanjaro CCM isingekuwa imebweteka kiasi hiki.

Mramba,Yona,Mbowe,Ngalai, ni kati ya vigogo waliopata kupigwa chini kilimanjaro. hata Mzee Msuya, pamoja na uzito wake, alishindwa kumpitisha mtu aliyemtaka ktk kura ya maoni ya ccm jimbo la mwanga.

kwa kweli monopoly ya CCM katika siasa za Tanzania haitusaidii. badala ya kuwakejeli na kuwaponda chadema, mimi nawaomba tuwape ushauri nasaha. upinzani makini na wenye nguvu utaleta neema kwa tanzania nzima.

Kama tunataka kulisaidia taifa ni vizuri tukajiuliza maswali yafuatayo:
1.Kwanini CCM ina shinda kirahisi ktk maeneo[kusini...] ambayo sera[vijiji vya ujamaa] zake zimewaumiza zaidi wananchi? mikoa iliyoko nyuma zaidi kimaendeleo?
2.Kwanini, pamoja na uoza wote wa CCM, bado chama kinaendelea ku-attract wagombea wenye elimu,upeo, na uzoefu? Hapa nazungumzia watu kama Balozi.Swedi Kagasheki,Dr.Migiro,Prof.Wangwe,Dr.Kawambwa,Prof.Mwakyusa etc. Wanasiasa wengi huharibika/huoza baada ya kujiunga CCM.
 
Joka kuu,
Haya maneno!... lakini kitu kimoja. Utamshauri vipi mtu usiyemfahamu roho yake! Nikiwa na maana Chadema hawakuja hapa kutafuta ushauri wetu bali nafikiri ni kutuvuta sisi na urembo wao.

tatizo linakuja kuwa Chadema kweli anavutia sanaa ila kuna hizi sifa mbaya ambazo zinatakiwa zifutwe ama twe na hakika nazo - Ni KWELI sio KWELI, kisha mvuto utakuja kwa mtu yeyote yule anayejali uzuri wa mtu ni roho yake sio maumbile.

Mwanasiasa na Mnyika wametuvuta toka mbali sana. Kuna maswali ambayo hayawezi kurudiwa tena na sisi tutaweza kuyatumia huko mbele lakini hili wingu bado halijaisha.
 
jana kwenye kikao cha NEC amina katolewa nishai na katibu mkuu makamba tena na tv ilikua ikionyesha live ,,alienda kukaa kwenye kiti ambacho slitsakiwa kukaa naibu katibu mkuu makamba alifoka" wewe amina toka hapo ,sio sehemu yako ,,kwakae kulee nyuma ,hapo ankaa msaidizi wangu mimi makamba ,katibu mkuu"

sasa kweli huyu hata protokali hajui,au alitaka tu akae karibu na jk kikaoni ,kama anakaa nae sehemu nyingine nyingine angemsubiri huko huko ,sasa kweli huyu ndio mnataka kumpima na mh mbwe ,,si halali bora mbowe mngempima na nchimbi[dr feki]
 
Phillemon,

Nikumbushe, kumbe Amina Chifupa ni mjumbe wa NEC?!, sikua nikijua hilo

FD
 
fikiraduni ,
la ujumbe wa nec wa amina ,sijui ila jana wajumbe wa nec pamoja na makada wa juu wa chama chini ya mwenyekiti,rais ,waliandaa mkutano wa wazi pale dodoma kuzindua kampeni za wajumbe wa nec kupita mikoani kuimarisha chama.. amina pia naye alihudhuria na mkutano ule umeonyeshwa kwenye tv jana mchana saa tisa .
 
Wapendwa,

Leo tena nimepita hapa kuzungumza nanyi machache. Nimekuwa kimya kwa siku chache, siku chache baada ya kuandika majibu yangu ya mwisho niliondoka tena DSM. Nimetoka kidogo kwa shughuli zangu binafsi. Na mnajua tena nchi yetu, ukitoka tu nje ya mjini internet inakuwa almasi!

Bado niko mkoani na nafurahi nikiwa huku niligongana na mjumbe mmoja wa hii mitandao. Nadhani baadaye nitapata wasaa wa kukutana naye na pengine nikirejea naweza kuwapa salamu zake.

Leo nitazungumzia kuhusu helikopta- na kilichonisukuma kuzungumzia helikopta kabla ya hoja ya family bussinness ni simu ambayo nimepigiwa na mmoja wa watanzania akinieleza kwamba CCM imefanya mkutano wa kupokea viongozi wa upinzani. Na kwamba viongozi hao walipotoka wameponda helikopta kwelikweli.

Nilijiuliza maswali mawili:

Mosi, hivi kwanini helikopta imekuwa suala kweli? Nikajijibu-ukiona mpinzani wako anazungumza hoja moja kila siku kuhusu wewe ujue aidha amekuoana dhaifu katika hoja hiyo au anakuogopa kupindukia. Ukifika mwisho wa ujumbe wangu utaamua mwenyewe kati ya haya mawili.

Pili, nikajiuliza tena-hivi kwa nini CCM badala ya kuchambua kwa kina imewafanyia nini watanzania inaanza kwa kuzindua ‘viongozi wa upinzani’ iliowapokea? Is dealing with opposition number one enemy of the nation?. Nikakumbuka mjadala wa CCM kumbomoa Mbowe( kwa ambaye hajausoma autazame hapa………..)

Anyway, leo sijaja kuzungumzia haya. Nitazungumzia hili baada ya kujua kwa kina nini hasa kilijiri katika mkutano wa CCM.

Kabla sijaeleza kuhusu helikopta niweke suala suala moja ambalo limezua mjadala kutokana na mchango wangu wa mwisho. Suala la mimi kuwa consultant!

Natambua mchango wa wote mliochangia hoja hii hususani Mwanasiasa, Jasusi, Ogah, Mkandara, Fikiraduni na wengineo. Hoja ambayo imeanzishwa nadhani na Mtalii baada ya majibu yangu. Technically and traditionally neno hili limekuwa likitumika kurejea mfumo wa wa watu au taasisi kuwafuata au kuchukua mtu au taasisi kwa ajili ya kupata ushauri fulani. Root ikiwa neno ‘to consult’. Sina kamusi hapa nilipo wala nyaraka yenye ufafanuzi wa formal kuhusu neno hili.Lakini wakati huo dhana hii ilikuwa inabeba maana ‘ushauri’.

Lakini niseme tu kwamba neno hili siku hizi(na utamaduni huu umeanzia Marekani) limeanza kutumika pale ambapo taasisi inapofanya outsourcing ya utalaamu au nguvu kazi ya aina fulani. Na maneno ambayo hutumika ni aidha consultant au independent contractor.

Kwa hiyo consultancy by itself sio taaluma wala sio utaalamu. Ila ni mfumo tu wa kutumia utaalamu na haishii kwenye ushauri pekee, siku hizi ni mpaka vitendo vya kufanya kazi yenyewe.

Kwa upande wangu tu niseme nimewahi kuwa consultant katika kazi mbalimbali. Lakini kwa kesi ya mradi wa bunge mimi nilikuwa rapportuer(mnukuzi). Binafsi naamini kazi hii haisomewi-ingawa katika baadhi ya shahada uandishi wa ripoti upo ndani yake kwenye CL ama communication skills.

Kwa hiyo taasisi inapotaka rapportuer inaangalia kati ya vitu viwili : Ngazi ya elimu ama mifano ya kazi ambazo muhusika ameshazifanya. Mimi nina-track record ya unukuzi katika mashirika ya kitaifa na kimataifa. Kabla ya kazi unawasilisha kitu kinachoitwa bio data-na kwa wale ambao wamefanya kazi na mashirika ya kimataifa wanajua ni process gani inapitiwa. Baada ya approval rate inapangwa kwa kuzingatia past works, past payment, experience na elimu.

Mimi rate yangu kwa sasa ipo kati ya dola 70 na 150 kwa kutegemea taasisi. Lakini nakiri kwamba suala la elimu ni kigezo muhimu. Huwa nasikitika sana kwamba kuna madaktari na maprofesa wanafanyakazi mbovu za kulipua lakini wanalipwa kuliko mimi kwa sababu tu wanavyeti vikubwa zaidi kuliko mimi. Na kazi tunayofanya ni ileile. Siku zote nimekuwa nikifanya kazi kama freelance. Lakini sasa kutokana na kutingwa nashughuli za kisiasa na kwa nia ya kuruka hili suala la kuwa rated low nadhani in future ni vyema vijana wenye opportunity kama yangu wakaanzisha consultancy company. Tuwe rated as a institution.

Mzee Es: umeuliza kuwajengea uwezo wabunge maana yake ni nini? Nilichoandika ni jina la Mradi: Mradi wa kuwajengea uwezo wabunge, nilichofanya ni kutafsiri tu kwa tafsiri isiyo rasmi jina la mradi unaoitwa “The Center for International Development of the State University of New York (SUNY/TANZANIA) technical assistance programme for the strengthening of Tanzania’s Union National Assembly/Parliament”. Mradi huu kumsingi unajengea uwezo bunge na wabunge. Lazima nikiri, kuna vitu huwa siandiki kwa kina hususani zinazohusiana na taasisi nyingine ambazo hazina uhusiano wowote na mijadala yetu ya hapa ya kitaifa. Ni kuziingiza katika mijadala isiyowahusu!

Mtalii: Ulianzisha hoja hii lakini pamoja na majibu ya baadhi ya watu naona ulikuwa bado hujaridhika, baada ya maelezo haya ni matumaini yangu sasa utaliweka hili akilini na tutandelea na mijadala mingine. Lakini katika maelezo yako kuna facts tatu umezipotosha sana: Mosi, kwamba sikuzungumzia kuhusu elimu yangu ya kidato cha
 
sita-wachangiaji wengine wameshakujibu. Pili, umesema kwamba CHADEMA ndio wananiita consultant na ukatumia mifano ya Maji Marefu na wengineo na kwamba taasisi za kimataifa haziwezi kumuita mtu kama mimi consultant. Ukweli ni kwamba CHADEMA mimi ni mtendaji hivyo siwezi kuwa consultant kama ni kutoa ushauri kwenye chama ni sehemu tu ya wajibu wangu.

Ukweli pia ni kwamba neno consultant limetumiwa na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ambazo nimezifanya nao kazi, na hii iko katika mkataba wa assignments walizonipa ikiwemo kwenye mradi wa kuwajengea uwezo wabunge na bunge.

Tatu, umesema na nakunukuu, " Ukabila na ukanda upo.mwaka huu MBOWE alipeleka wenyeviti wake watatu London kuwapongeza kwa ushindi na kati hayo watatu wote ni wachaga na wanatoka Kilimanjaro,
cha kujiuliza hakukuwa ma mwenyekiti toka Mara au Kigoma au Mpanda ambako nako kulipatikana viti." Ukweli ni kuwa hakuna wenyeviti watatu waliopelekwa London kwa ajili ya kuwapongeza kwa ushindi.

Sasa kinyume cha kusema ukweli ni nini?Jibu ndicho ulichosema. La kujiuliza ni kwanini umesema maneno haya?Je, umepotoshwa au umeamua kupotosha?

Anyway, niaachane na hili kwa kuwa ni la binafsi sana, halina maslahi mapana kwa watanzania kwa ujumla.

Back to chopper issue:

Chinga alitoa mahesabu yafuatayo kuhusu CHOPPER, kwenye mjadala wa Mbowe na Chifupa namnukuu:


"Tufanye hesabu kidogo: Kuikodi Helikopta hii
kunawagharimu dola 1,200 kwa saa. Na watakuwa nayo kwa
siku 23, kila siku ina masaa 24.
Kwa hiyo jumla ni 23 x 24 x 1,200 = USD 662,400.00
Exchange rate ni about TShs 1300, kwa hiyo hizi ni
662,400 x 1300 = Tshs 861,120,000 Yaani takriban
Milioni mia tisa zinaunguzwa hivi hivi, na hapo
hatujaangalia gharama za mafuta, per diem na gharama
nyinginezo za mikutano! Hiki kweli ndio chama mbadala
au ndio hiyo NGO flani.... and the guy wants to be a
president. What a joke?"!"

Chinga amemalizia kwa kusema what a joke-nadhani alijua kabisa kuwa alikuwa akizungumza mzaha. Na mtu akisema mzaha. Watu hucheka na kupuuza.

Zifuatazo ni hoja zinasosemwa kupinga matumizi ya helikopta:

1. Helikopta inafika maeneo machache
2. Helikopta ni ghali kupindukia
3. Helikopta inabeba watu wachache hivyo viongozi wengi hawapati fursa ya kupanda
4. Badala ya kutumia helikopta pesa zingeelekezwa katika matumizi mengine.
5. Helikopta ni ishara ya anasa na ‘ubepari'
6. Tanzania haujafikia bado ngazi ya kutumia helikopta
7. Helikopta ni mkakati wa Mbowe kujikweza ambao unakataliwa na viongozi wengine
8. Helikopta inatoa muda kidogo sana wa kuhutubia kwa hiyo muhutubiaji huondoka na helikopta yake bila ujumbe kubaki.
9. Watu wanakuja tu kushangaa helikopta, hakuna athari yoyote kwa maamuzi yao.
10. Wagombea na viongozi wanajitoa kwa sababu ya Mbowe kutumia helikopta
11. Helikopta inapingwa na watu wengi

Nianze sasa kujibu hoja moja baada ya nyingine na kutoa sababu 10 kwa nini CHADEMA ilitumia na imepanga kuendelea kutumia helikopta:

(i) Helikopta inafika maeneo mengi hata yale yasiyofikika kirahisi
Katika uchaguzi uliopita CHADEMA ilitumia magari katika awamu ya kwanza ya kampeni. Tukapata uzoefu wa kutumia magari katika kampeni za urais. Kumbuka hii ilikuwa ni mara ya kwanza kusimamisha mgombea urais. Katika awamu ya pili na kuendelea CHADEMA ilitumia helikopta.

Mosi, Baada ya kuanza kutumia helikopta CHADEMA ilikuwa na uwezo wa kufanya wastani wa mikutano 8 kwa siku. Hii ilifanya Mbowe awe mgombea aliyefanya mikutano mingi kuliko mgombea mwingine yoyote tena katika maeneo yenye utofauti mkubwa wa umbali. Pili, CCM ni wajanja, siku za kampeni(kabla ya muda kuongezwa ni around 70) wakati ambapo nchi ina wilaya zaidi ya 130 na majimbo zaidi ya 230.

Mgombea urais anayetumia magari kufanya mkutano mmoja kila wilaya kwa siku hawezi kumaliza nchi nzima katika kipindi hiki kifupi cha kampeni. CCM inatumia advantage ya kuwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa etc kuziba mapengo na kuwa na competitive edge. Njia moja ya kuwazidi kete ni kutumia helikopta kwenda maeneo tofauti kwa haraka. Tatu, CCM imeshindwa katika miaka zaidi ya 45 ya utawala wake imeshindwa kuweka mtandao mzuri wa barabara mpaka vijijini kabisa.

Hiki ni kikwazo cha wagombea wa uraisi kufika kila mahali. Yapo maeneo ambayo mpaka sasa wanadhani Nyerere bado ni rais. Hapafikiki kirahisi. Helikopta ilikuwa na makawa na jenerata ndogo. Ipo mikutano ambayo ilifanyika vijijini kabisa ambapo ingekuwa ngumu kufika kwa magari katika wakati mwafaka.

Huku ni kuwafikishia ujumbe wa mabadiliko wananchi waliopembezoni kabisa!. Sasa tutaitumia tena kueleza mwaka mmoja wa kushindwa kwa serikali ya CCM na haja ya watanzania kukumbatia ‘TUMAINI JIPYA'. CHADEMA,chama mbadala! Hii ni kwa manufaa kwa Taifa zaidi ya vyama..


(ii) Helikopta ni nafuu kuliko magari na ndege-

Najua wengi mtashangaa!. Huu ndio ukweli. Nianze kwa kusema kwamba mahesabu ya Chinga ameamua kupotosha, sijui kwa makusudi au kwa kutokujua. Kitu kimoja amesema kweli-kwamba helikopta hukodishwa kwa dola 1200 kwa saa. Helikopta nyingi duniani zinakodishwa kati ya dola 1000 na dola 2000 kutegemea aina nk. Uchaguzi 2005 CHADEMA ilikodi helikopta ya dola 1200 kwa saa. Kwa kampeni zote zilizoratibiwa na makao makuu ya chama, CHADEMA ilitumia jumla ya Tsh milioni 700 na ushee. Kati ya hizo ni sh milioni 200 tu zilitumika kwenye helikopta. Na si bilioni 3 kama baadhi wanavyosema, na pesa hizi zilitoka katika vyanzo vya ndani. Nitazungumza zaidi hoja hii nitakapozungumza fedha, conservatives etc!.

Lakini kwa sasa, hebu ipongezeni CHADEMA kwa kuwa wazi kusema imetumia shs ngapi na kuvitaka vyama vingine navyo viseme. Tuliviambia vyama vingine navyo viseme toka May sasa ni December.Kimya!!!Bado wanaandaa mahesabu toka December mwaka jana uchaguzi ulipokwisha!.
 
Back to chopper!. Asichojua Chinga na wengine ni kuwa helikopta, tofauti na vyombo vingi vya usafiri gharama zake za kukodi zinahesabiwa kwa muda ambao helikopta inakuwa hewani. Helikopta ikiwa chini hailipiwi gharama za kukodi. Wanachofanya tu ni kukupa minimum flying time per day(which in most cases is 1hr) na minimum days you can hirre(which is most firms is one week). CHADEMA katika uchaguzi uliopita ilikuwa inatumia between 1 to 2 hours a day!. Si zaidi ya hapo.

Sasa tuchukue kadirio la juu- 2 hours a day, hii inafanya gharama kuwa dola 2,400 kwa siku. Mafuta ya ndege ni kati ya tsh 900 na 1200 kwa lita. Ila by experience mafuta ya masaa mawili ni takribani asilimia 10 ya gharama za kukodi kwa hiyo ni dola 240. Jumla kwa siku ni around dola 2640, tufanya 2700. Tukigeuza kwenda fedha za kibongo hii ni sawa na takribani 2,800,000 kwa kiwango changu cha kubadili fedha.

Kwa hiyo helikopta kwa siku ni shillingi hata tukimbandisha kupindukia milioni 3.

Ukifanya mikutano 8 kwa siku hii ni sawa na wastani wa kadirio la juu wa shilingi laki nne kwa mkutano mmoja. Laki nne kwa mkutano mmoja wa mgombea urais. Hii ni peanut jamani.

Mkutano uliofura watu(tazama picha kwenye www.chadema.net) ambao wamekuja wenyewe bila kubebwa na FUSO wala mabasi wala kuletwa kulipwa posho wala kuja kwa kupewa fulana na kofia. Wanakuja kwa ridhaa yao. Hii ni kuwa very cost effective!

Naambiwa mkutano mmoja wa kikwete wa Jangwani uligharimu tsh milioni 20. Hii ni sawa na mikutano mingapi ya helikopta?


Gharama za kukodi ‘shangingi' moja kwa siku ni dola 200. Hii ni sawa na 1/6 ya kukodi helikopta!. Kikwete alikuwa na msafara wa mashangingi mangapi? (Mtaniambia aliyanunua- sawa sasa tuyahesabu katika rate ya kukodishwa!). No wonder katika maeneo walikuwa wakitumia mashangingi ya serikali. Msafara wa magari mengi unahitaji man power kiasi gani? Kama kila mmoja akilipwa posho ya kati ya 20 na 30 jumla ya gharama kwa siku ni kiasi gani?

Watafiti, tupeni majibu. Chinga,toa uchambuzi wa kifedha wa suala hili pia!

Kikwete na Shein walikuwa wavuki kwa magari pekee mkoa hadi mkoa. Walikuwa wakitumia ndege ya serikali. Eti walikuwa wanaikodi. Ndege ya serikali kukodi ni bei gani kwa safari? Inatofauti gani na helikopta? Lakini je, ndege inaweza kutua kijijini na kufanya mikutano kama nilivyosema? Nataka majibu ya kweli!


(iii) Helikopta inabeba zaidi ya kiongozi mmoja na viongozi wengine wananjia ya kuwepo

Si kweli kwamba helikopta ilimbeba Mbowe pekee. Helikopta inategemea ukubwa. Ile tuliyokodi katika uchaguzi 2005 ilikuwa na capacity ya kubeba abiria 3 na rubani. Kwa hiyo kupanga ni kuchagua, unaamua tu kuchagua ni viongozi wangapi wapande. Kwa hiyo alikuwa akipanda Mbowe, mratibu wa ziara ya helikopta ambaye humsaidia pia pilot kutambua maeneo na nafasi ya kiongozi mmoja. Hapa ilitegemea mahali. Yapo maeneo ambayo alipanda mgombea mwenza, yapo maeneo ambayo mgombea wa eneo husika wa ubunge alipanda na yapo maeneo ambayo kiongozi wa chama wa eneo husika alipanda. Kwa hiyo ilifanyika kutokana na situation. Binafsi nilipanda helikopta ilipokuja Ubungo- tulitua Kimara, Mbezi, Mabibo, Urafiki etc. Nilipanda kama mgombea ubunge. Kwa hiyo wagombea wanaosema helikopta ni ya Mbowe pekee ni wazushi. Tatizo ni kuwa ilikuwa ukitaka kupanda helikopta lazima uache jimbo lako uende kuipandia katika jimbo ambalo mkutano wa mwisho unafanyika kabla ya kufika kwako. Kwa hiyo wapo waliamua kubaki jimboni kwao waisubiri ije wampokee mgombea urais. It was a matter of choice. But what on hell is kupanda helikopta mpaka watu wagombanie? Kiongozi wa chama wa eneo husika anapaswa kuwa uwanjani akimsubiri mgombea wake wa urais afike ampokee, hizo ndizo itifaki. Zilitekelezwa katika maeneo yaliyofikika. So inawezekana viongozi kuwako katika maeneo mengi, it's a matter of choice hususani katika maeneo ambayo magari yanafika!.

(iv) Pesa zinaelekezwa pia katika matumizi mengine, kupanga ni kuchagua

Pesa zilingepelekwa katika maeneo mengine. I tell you today. Hizo milioni 200 zilizopelekwa katika helikopta zisingeleta impact kama ambayo imeletwa na helikopta. Kupanga ni kuchagua. Besides, kama ni kupelekwa maeneo mengine tsh 500 zilipelekwa katika maeneo mengine mabango, vipeperushi, vyombo vya habari, kusaidia wagombea katika red seats the list is long!. Nieleze ni mambo gani hayo mengine ambayo hayakupewa enough attention ambayo yangezidi hizo faida nilizofafanua hapo juu za helikopta?

(v) Helikopta ni suluba, helikopta ni kazi

Kwa yoyote aliyewahi kupanda helikopta ya polisi ambayo inashabihiana na ile iliyotumiwa na CHADEMA anajua kuwa kupanda helikopta ni kuweka roho rehani kama sio hewani. Helikopta inaleta suluba ya kuongeza idadi ya mikutano, binafsi nampa pole Freeman kwa kuhutubia mikutano mingi namna hiyo kwa siku. Huyu jamaa angekuwa kimeo angeanguka siku nyingi sana! Lakini the guy ame-survive all over. Sijasikia ameanguka jukwaani. Helikopta ni chombo cha kazi. Helikopta tunayotumia haina AC kama mashangingi, haina viti vinavyofanana na masofa kama mashangingi. Haina raha kama ndege ya serikali wala haina anasa kama ndege ya rais. Hakuna hostosess na juices mule. Kuna harufu ya moshi na vumbi la upepo mkali unaposhuka. Ni symbol ya mapambano na harakati!. Ni symbol ya vita dhidi ya mfumo mbovu wa utawala unaopenda anasa!

(vi) Tanzania imefikia ngazi ya kutumia helikopta

Wait a minute! Huku ni kujidharau. Wakenya jirani zetu hapo wanatumia helikopta mpaka kukagua mashamba. Ile helikopta tuliyokodi pamoja na kurudi kufanyiwa mapendekezo ilitumiwa pia na watu wa mashindano ya magari. Ni helikopta ilitumika kuhamasisha wananchi kwenye vuguvugu la chungwa(ODM) kuhusu katiba Kenya. Lazima tuwe na viongozi wenye kuona mbali na kujua nini tunastahili kwa raslimali tulizonazo!. Hatuwezi kuwa na chama kinachoona jembe la mkono ndio halali yetu tukipanda kidogo eti tutumie plau na mikokoteni ya kukokotwa na ng'ombe. Napenda utamaduni wetu...
 
(vii) Helikopta ni mkakati wa CHADEMA sio wa Mbowe
Uamuzi wa kutumia helikopta ulifanywa na baraza kuu la chama na kuridhiwa kwa kauli moja na mkutano mkuu wa CHADEMA. Sio uamuzi wa Mbowe ule. Hata baada ya uchaguzi, baraza kuu lilikaa tena kutathmini na kwa kauli moja walipongeza matumizi ya helikopta na kupitisha azimio la kuendelea kutumia helikopta.(soma tamko kwenye. Kwa hiyo helikopta ni mkakati na utamaduni wa CHADEMA. Tegemeeni helikopta kwenye TUMAINI JIPYA. Lakini helikopta ni njia moja tu inayotumiwa na viongozi wa kitaifa kwa kipindi fulani kwa nia fulani ya kisiasa!Kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi na ujumbe mahususi. Tunaomkakati mwingine, huu sasa tunauita CHADEMA ni Msingi, kama ni jeshi basi huu ni mkakati wa infantry. Wa chini kwa chini!. Huu unahusisha kutuma vikosi vya makada kufanya mikutano midogo ya hadhara katika kijiji na mitaa na kuingia mikutano ya ndani kutoa mafunzo na kujenga netweki au oganizesheni ya chama nganzi ya chini kabisa!. Huu utaanza mara baada ya helikopta kulipua mabomu ngazi ya juu. Hii ni sayansi ya vita vya kisiasa....hii ndiyo CHADEMA,chama mbadala.

(viii) Ujumbe umeleta hamasa, Helikopta yaweza kutoa muda mrefu wa kuhutubia
Ukitaka kujua kuwa ujumbe wa helikopta ulileta hamasa angalia jinsi ambavyo wagombea walikuwa wakiweweseka baada ya helikopta kupita maeneo yao. Utakuwa huwatendei haki watu wa Tarime kwa mfano kuwaambia kwamba baada ya Helikoptav kupita na Mbowe kumwaga maneno alipoondoka walisahau kila kitu. Ingawa nakubali kuwa kuna baadhi ya maeneo tulimwaga mbegu katika jangwa na pengine katika magugu. Ni hadithi ya mpanzi! Ndio maana sasa tumeamua kujikita katika kusuka vizuri na upya uongozi wa chama ngazi ya chini. Tunaanza uchaguzi kuanzia msingi, tawi na kuendelea mpaka taifa kuanzia uchaguzi wa mwakani. Tegemeeni chama kuongeza nguvu. Na wote wanaotaka kugombea tunawakaribisha. Tunachotaka ni nguvu na mamlaka ya umma.

Tume-take note suala la muda wa kuzungumza. Kwa hiyo katika awamu ya sasa tutazungumza kwa saa si chini ya moja kwa kila mkutano. Kwa maneno mengine sasa badala ya mikutano nane na zaidi kwa siku tutafanya kati ya mikutano minne na mitano tu kwa siku. Watoto wa kijiweni husema, huu utakuwa ni wakati wa makamuzi ya kufa mtu!. Hakuna kulala mpaka Kieleweke...

(ix) Watu hawaji tu kushangaa helikopta!

Guess, mpaka sasa unajibu la swali hili; unaweza kuja kushangaa ndevu za shekhe ama padri lakini kwa dakika tano unazomsilikiliza ukaona TUMAINI JIPYA. Hivi jamani, tunawafanya watanzania washamba kiasi hiki kiasi kwamba hawajui kuchagua jema na baya.....wapo washangaaji-nakubali, lakini wapo waamuaji..tutafika.......

(x) Viongozi na wagombea wachache wanaojitoa wanafanya hivyo kwa sababu zao binafsi

Mbaazi zikikosa maua husingizia jua!....unajisikiaje unaposikia mtu mzima akisimama mbele ya luninga pembeni ya katibu mkuu wa CCM akisema nimejitoa CHADEMA kwa sababu Mbowe anatumia helikopta.......what comes in your mind quickly kuhusu mtu kama huyu baada ya ufafanuzi nilioutoa?..aidha ametumwa, au amekata tamaa au hajui chochote kinachoendelea katika chama chake........tunapaswa kumsamehe na kumwombea!(with a light touch)....Niliwahi kuandika kuhusu wanaojitoa...soma kwenye mjadala wa CCM kumbomoa Mbowe........
(xi) Helikopta inapendwa na watu wengi, inapingwa na watu wachache ama kwa kutojua undani wake au kwa kuamua kupotosha kwa makusudi

Ukweli ubaki pale kwamba helikopta ina wapenzi na washabiki wengi. Inapondwa zaidi na top leadership ya CCM, ni strategy ya kuichafua CHADEMA na kuchochea migogoro. Mpaka leo Kikwete na wenzake bado wanaiota helikopta, nadhani wangetumia muda zaidi kugombana na Darwin kuliko helikopta-because this is not a nightmere, its a real thing!

Sasa mpo hapa wachambuzi wachache mnaoiponda helikopta. Najua hamna nia mbaya ila mlikuwa haujapata upande wa pili wa shilingi kuhusu helikopta. Baada ya maelezo yangu nategemea sasa mtasimama katika ukweli.

Lila na fila havitangamani asilani….

HOJA YANGU KUU: HELIKOPTA NI CHOMBO KINACHOMWEZESHA MWANASIASA WA KITAIFA KUFIKA MAENEO MENGI NA YASIYOFIKIKA KWA MUDA MFUPI NA KWA GHARAMA NAFUU.HELIKOPTA NI UBUNIFU NA NI ISHARA KWAMBA CHADEMA INGEKUWA MADARAKANI INGETUMIA UBUNIFU, HATA KATIKA UMEME CHADEMA ISINGEKUJA NA ‘UBUNIFU' WA KULETA ‘RICH-MONDULI':

Natabaruku:

Coming soon, is CHADEMA a family business, what was behind special sets nomination? Is CHADEMA a Christian and Chaga party?Stay tuned.

JJ

Ps: Waandishi wa nyumbani, hapa nimewawekea facts zote. Nategemea mtaandika makala katika magazeti ya kuhusu helikopta, nia ni kuondoa upotofu kwa maslahi ya taifa.
 
JJ kazi yako ya Uconsultant wa kulipwa doa 100 kwa siku na chadema siy mbaya...i hope your TAX RECORDS are in order
 
JJ,

Well done! ninasubiri ya family business, hope utakuja soon kabla ES naye hajaondoka na dukuduku.

FD
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom