Mbowe: Ununuzi wa ndege siyo kipaumbele sahihi kwa nchi yetu zaidi ya Elimu, Afya na Miundombinu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,965
141,968
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kununua ndege siyo kipaumbele sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu ukilinganisha na Elimu, Afya na Miundombinu.

Mbowe amesema uwekezaji kwenye ATCL unahitaji mtaji mkubwa, utaalamu uliotukuka kwa watu wetu na mbinu za kisasa kuhimili ushindani wa soko.

Hata hivyo msemaji wa serikali Dr Abbas amesema serikali kuwekeza katika ndege haimaanishi kuwa imeacha kuwekeza katika maeneo mengine.

Source BBC Dira ya Dunia

My take: Naona Mbowe ana hoja na Dr Abbas ameipangua kiufasaha.

Maendeleo hayana vyama!
 
M
Tulipaswa kuwekeza ndege ndogo kwa soko la ndani na ukanda EA.Ila kwa root nje midege mikubwa haikuwa uamuzi sahihi.
Moja Tu ya Kuanza kulitangaza Shirika sio mbaya au hata 3 za nje sio mbaya

Shirika la Ndege lina manufaa sana kaka hasa safari za Nje
 
Na Huu ndio Umasikini wa Fikra ulitaka ndege ya Biashara iwe Nauli za daladala?

Wakati Mwingine mambo ya msingi msitoe mawazo kama haya ni aibu kwenu.

Marekani wana ndege 1200 za shirika lao ila wapo watu hawana hata sehemu ya kulala

Mtanzania anayeishi chini ya Dola 1 ya Tsh 2300 kwa siku ambao ni wengi anawezaje kumudu ticket ya ndege ya 230k hadi 300k ?
 
Miundo mbinu ya usafiri wa anga ni ununuzi wa ndege, ujenzi wa viwanja vya ndege na ununuzi wa radar. Miundo mbinu ya usafiri wa majini ni ununuzi wa meli na ujenzi wa bandari.

Miundo mbinu ya usafiri wa nchi kavu ni ujenzi wa barabara, reli na ununuzi wa treni za umeme Miundo mbinu ya huduma za afya ni ujenzi wa vituo vya kutolea huduma hiyo na ununuzi wa madawa na vifaa tiba.

Miundo mbinu ya elimu ni ujenzi na ukarabati wa mashule/ vyuo na ununuzi wa vifaa vya kufundishia. Miundo mbinu ya maji ni ujenzi ujenzi wa wa matenki ya maji, kutandaza mabomba ya kusafirisha maji na ununuzi wa pampu za kusukuma maji.

Sasa kipi hapo Mbowe anaona si muundo mbinu? Miundo mbinu ya chama cha siasa ni kujenga majengo ya ofisi za chama ngazi zote. Jee yeye ameshajenga miundo mbinu ya chama cake?
 
Ununuzi wa midege toka nchi za mabeberu ni zigo la hasara kwa walipakodi wa Tanzania.

Ukiacha Ethiopia, hakuna shirika la ndege la nchi za Afrika linaloendeshwa kwa faida.

Na Ethiopia wameweza kwasababu walianzisha shirika lao zamani kabla biashara ya usafiri wa anga haijawa biashara kichaa.

JPM alisema Kagame ndio mshauri wake ktk ununuzi wa midege, lakini Kagame ameingia hasara kubwa na amelazimika kuomba ubia na Qatar Airways.
 
Na Huu ndio Umasikini wa Fikra ulitaka ndege ya Biashara iwe Nauli za daladala?..
Muwe mnafuatilia vitu, Marekani kama Marekani hawana ndege hata moja inayomilikiwa na serikali angalau kwa asilimia moja tu, zote wameyapa makampuni na mashirika binafsi yaendeshe kama biashara, wenyewe wanachukua kodi.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kununua ndege siyo kipaumbele sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu ukilinganisha na Elimu, Afya na Miundombinu...
Mbowe ni mfanyabiadhsra anajua anachokisema ambacho ni ukweli mtupu, huyo Msemaji wa Serikali anafanya kazi yake ya kusema tu kama ilivyo kwa wote wa Awamu hii ya maneno bila vitendo. Mfanyabiadhara kwa kuangalia mahitaji anaamua alete bidhaa gani, wakati gani na kwa ajili ya wateja gani na bidhaa ikishapokewa haifungiwi stoo, kama yale madege yamepark pale miaka na miaka yakingoja wateja, bali atawapelekea wateja wake ambao watamlipa fedha yake ya kuleta bidhaa tena.

Musukuma Bus Service akiona kuna haja ya kuongeza Bus jingine, kabla hata ya kuagiza, ataanza kulitafutia ruti yenye abiria wengi na ni wakati gani abiria ni wengi na hiyo ndo itampa ishara lini Bus lifike na la ukubwa gani ili likifika tu linaingia kazini. Wenye PhD wanajua watu husafiri kwa ndege kwa hiyo zinanunuliwa nyingi tu, zikipokelewa kwa mbwembwe na kujisifu, wanaanza kuunda Kampuni ya Ndege lakini inagundulika kutahitajika Uwanja wa nyumbani kwa hiyo unaanza kujengwa huku juhudi za kutafuta ruti zenye abiria wengi zinaanza na zinaendelea hadi leo. Musukuma Bus Service inachanja mbuga bila wasiwasi, madege yakiwa yamepark tu, mengine yakisubiriwa!
 
Naona Mbowe sasa akili imerudi anaongelea maendeleo ya vitu

njia ya mwongo fupi.Sasa kampeni za uchaguzi 2020 kwa nini walipinga maendeleo ya vitu?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kununua ndege siyo kipaumbele sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu ukilinganisha na Elimu, Afya na Miundombinu.

Mbowe amesema uwekezaji kwenye ATCL unahitaji mtaji mkubwa, utaalamu uliotukuka kwa watu wetu na mbinu za kisasa kuhimili ushindani wa soko.

Hata hivyo msemaji wa serikali Dr Abbas amesema serikali kuwekeza katika ndege haimaanishi kuwa imeacha kuwekeza katika maeneo mengine.

Source BBC Dira ya Dunia

My take: Naona Mbowe ana hoja na Dr Abbas ameipangua kiufasaha.

Maendeleo hayana vyama!
Mandege yenyewe maboooooooooovu. Airbus iligoma kuruka Mwanza, wakaanza kuikorokochoa
 
Bwashee hapo kwenye mbinu za kisasa kuhimili ushindani wa soko amejibu nini cha maana?

Acheni kukimbia kimbia kama watoto.
 
Back
Top Bottom