Kamati ya Miundombinu yasisitiza Wakandarasi wazawa kupewa kipaombele

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
IMG-20240316-WA0156(1).jpg
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeisisitiza Serikali kutoa kipaumbele kwa Wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa miradi na kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Wakandarasi hao ili kutoa fursa ya ushindani na Wakandarasi wa nje katika upatikanaji wa zabuni.

Hayo yameelezwa Mkoani Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso (Mb) wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vivuko vinavyojengwa na Mkandarasi Mzawa Songoro Marine na kuridhishishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

IMG-20240316-WA0162(1).jpg

"Hakikisheni mnawajali wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa miradi kwa kuwapatia malipo kwa wakati, mkimuwezesha Mkandarasi huyu ataenda kuwekeza katika Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika na kuleta ajira kwa wananchi wa maeneo husika”, amesema Kakoso.

Kuhusu utekelezaji wa vivuko, Kamati imesema bado kuna umuhimu wa kuongeza huduma za vivuko katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Mara, Geita, Mwanza na Kagera hivyo Serikali ione namna ya kusimamia utekelezaji wa miradi kwa haraka ili iweze kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.

IMG-20240316-WA0166(1).jpg

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiahidi Kamati kufuatilia malipo la Mkandarasi Mzawa Songoro Marine ili akamilishe ujenzi wa vivuko vipya vitano pamoja na ukarabati wa vivuko viwili.

"Nitahakikisha nafuatilia kwa ukaribu malipo haya Wizara ya Fedha (HAZINA), na naamini kuwa fedha zitapatikana na Mkandarasi ataendelea na utekelezaji wake kama ilivyopangwa", amesisitiza Bashungwa.

IMG-20240316-WA0154(1).jpg

Naye, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Bw. Lazaro Kilahala ameeleza kuwa Wakala huo
unaendelea kusimamia ujenzi na ukarabati wa vivuko hapa nchini ili kuongeza utoaji wa huduma za usafiri kwa wananchi.

Akitoa taaarifa ya ujenzi wa vivuko, Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro ameeleza kuwa katika Karakana ya Mwanza wanaendelea na ujenzi wa vivuko vipya vya Kisorya – Rugezi, Ijinga – Kahangala, Bwiro – Bukondo na Nyakaliro – Kome pamoja na ukarabati wa vivuko vya Mv. Nyerere na Mv. Kilombero II.

IMG-20240316-WA0152.jpg
 
Bora waendelee kupewa wachina tuu wabongo wengi wanafanya kazi za hovyo sana, barabara na majengo mengi yaliyo jengwa na wakandarasi wa kitanzania ni vichekesho na upotevu wa fedha za serikali tuu
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeisisitiza Serikali kutoa kipaumbele kwa Wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa miradi na kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Wakandarasi hao ili kutoa fursa ya ushindani na Wakandarasi wa nje katika upatikanaji wa zabuni.

Hayo yameelezwa Mkoani Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso (Mb) wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vivuko vinavyojengwa na Mkandarasi Mzawa Songoro Marine na kuridhishishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

"Hakikisheni mnawajali wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa miradi kwa kuwapatia malipo kwa wakati, mkimuwezesha Mkandarasi huyu ataenda kuwekeza katika Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika na kuleta ajira kwa wananchi wa maeneo husika”, amesema Kakoso.

Kuhusu utekelezaji wa vivuko, Kamati imesema bado kuna umuhimu wa kuongeza huduma za vivuko katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Mara, Geita, Mwanza na Kagera hivyo Serikali ione namna ya kusimamia utekelezaji wa miradi kwa haraka ili iweze kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiahidi Kamati kufuatilia malipo la Mkandarasi Mzawa Songoro Marine ili akamilishe ujenzi wa vivuko vipya vitano pamoja na ukarabati wa vivuko viwili.

"Nitahakikisha nafuatilia kwa ukaribu malipo haya Wizara ya Fedha (HAZINA), na naamini kuwa fedha zitapatikana na Mkandarasi ataendelea na utekelezaji wake kama ilivyopangwa", amesisitiza Bashungwa.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Bw. Lazaro Kilahala ameeleza kuwa Wakala huo
unaendelea kusimamia ujenzi na ukarabati wa vivuko hapa nchini ili kuongeza utoaji wa huduma za usafiri kwa wananchi.

Akitoa taaarifa ya ujenzi wa vivuko, Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro ameeleza kuwa katika Karakana ya Mwanza wanaendelea na ujenzi wa vivuko vipya vya Kisorya – Rugezi, Ijinga – Kahangala, Bwiro – Bukondo na Nyakaliro – Kome pamoja na ukarabati wa vivuko vya Mv. Nyerere na Mv. Kilombero II.

Sio swala la Kamati tuu,hii ni ajenda ya Rais Samia alishawapa Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Tamisemi na Waziri wa Fedha.

-Serikali imeongeza Wigo wa miradi exclusively ya wazawa Hadi bil.50
-Saizi inatunga muongozo ya mradi ambao atapata contractor wa Nje iwe lazima walaui 40% wafanye wazawa(subcontractor)
-Serikali imeanzisha Samia infrastructure bonds Kwa Ajili ya kuwezesha wakandarasi wadogo
-Serikali imewatambua wakandarasi wanawake,vikundi vya Vijana nk Ili kuwawezesha.
-Mwasho Kuna Maelekezo ya kutoa orodha ya wakandarasi 50 Kila Mkoa ambao wanatakiwa kuwezesha na Serikali

View: https://twitter.com/Hakingowi/status/1768607740362969496?t=GfdXglnhbg_IS8ELiOgKsQ&s=19
 
Sio swala la Kamati tuu,hii ni ajenda ya Rais Samia alishawapa Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Tamisemi na Waziri wa Fedha.

-Serikali imeongeza Wigo wa miradi exclusively ya wazawa Hadi bil.50
-Saizi inatunga muongozo ya mradi ambao atapata contractor wa Nje iwe lazima walaui 40% wafanye wazawa(subcontractor)
-Serikali imeanzisha Samia infrastructure bonds Kwa Ajili ya kuwezesha wakandarasi wadogo
-Serikali imewatambua wakandarasi wanawake,vikundi vya Vijana nk Ili kuwawezesha.
-Mwasho Kuna Maelekezo ya kutoa orodha ya wakandarasi 50 Kila Mkoa ambao wanatakiwa kuwezesha na Serikali
Hapo kwenye infrastructure bond kafanya jambo jema sana.
Watungasera wafanye fast ili 2025 iwe implemented
 
Mapendekeozo hayo yanatolewa ili vikampuni uchwara vya wabunge vipate tenda.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeisisitiza Serikali kutoa kipaumbele kwa Wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa miradi na kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Wakandarasi hao ili kutoa fursa ya ushindani na Wakandarasi wa nje katika upatikanaji wa zabuni.
Halafu wanakamati haohao wanazunguka kwenda kuomba mlungura kwa wakandarasi
Nchi ngumu sana hii
 
Hawa wakandarasi wazawa hawana vifaa vya kazi vya kisasa na vyenye nguvu. Wakapewa kujenga wanasuasua na kubabaisha, hawamalizi mradi kwa wakati. Wakajifunze kujenga vijijini wapate uzoefu ndio wapewe miradi mikubwa
 
Kwa taharifa yako hao unao walinganisha nao ni serikali ya uchina. Bila kuwawezesha hawawezi toboa
 
Back
Top Bottom