Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

..ungeeleweka kama chadema ndio wangekuwa wamechukua silaha na kuuwa wananchi mtwara, arusha, na kwingineko.

..ungekuwa sahihi kama aquilina angekuwa ameuwawa na watu wa chadema, au walioamrishwa na chadema.

..mikutano haina madhara. Wenye madhara ni wahusika wanaoamrisha mauaji na dhuluma dhidi ya Watz wenzetu.
Vyombo vya usalama/ulinzi vina namna ya kutuliza ghasia kama wanaghasia hawatii sheria,hivyo walikuwa wanatekeleza majukumu,LAKINI yasingetokea hayo bila chadema kwenda kuwafitinisha
 
Hawa jamaa wameshaanza sarakasi zao Mama itakubidi ukorome kidogo la sivyo watakutawala.
Akorome KWA lipi Sasa, wakati kinachaodaiwa ni haki ya wananchi, hivi nyie mnaona tanzania ni kisiwa ,msione kwamba mwendazake aliweza ilikua swala la mda ati ipo siku angeshangaa Sana, leta katiba ,maana hakuna wakuizuia katiba,
 
Msimuendeshe kama mlikuwa mpo desperate hivi mngefanya kweli enzi za UKUTA alipowaambia msinijaribu ...mkaufyata, mmemkuta Mama hana makuu mnaanza kuzingua sawa tusubirie tuone.
 
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.

"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe

====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”

Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.

Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.

Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.
Asipotokeleza matakwa yako mzee mbowe utafanya nini ?mshukuruni saaana mama yetu kwa angalau kuwapa ahueni mnaweza hata kutoa mawazo kwa uhuru hata kama hayo mawazo ni ya hovyo
 
Sasa ndio muache ukaidi wakati dunia inapambana na Uviko 19 nyie mpo busy kuhamasisha maandamano.

Na Mwenyekiti wa kudumu janja janja sana achelewi kubadili gear angani huyu.
Mbowe acha pupa aisee,unachotaka kulazamisha kamwe hutokipata ,mama kaonyesha saana kuwa tayari kwa majadilianonila inasikitisha saana unapompa ultimatum ,wewe ni nani?
 
Naunga mkono hoja,
This time hatutakubali.

Katiba mpya ni ya lazima.
Ila Kwa mnayemwita mwendazake mliufyata sasa mmeona hayupo mnatafuta sababu ya kumchafua aliyepo, kaizima JK mkakauka kisa alikuwa akiwaita mnakunywa naye chai, Kaja JPM hakutaka kusikia katiba wala wapinzani mkaimba kuingia barabarani hatukuwaona, ATI this time hatukubali
 
Ndio Hatutakubali iwe Asubuhi iwe Jioni Katiba mpya Itadaiwa kwa Uchungu na Wivu Mkubwa.
Nchi haiwezi kuwa under one man show.
 
Akiamua kuwa dikteta kwa sababu watu wanadai haki, na awe. Hatuna cha kupoteza, zaidi ya kongwa zetu za kuonewa na kunyanyaswa.

Marehemu alikuwa dikteta, aliwapoteza baadhi uetu, aliwaua, aliwabbikia kesi, aliwateka, lakini hakutumaliza wote. Hata huyu, japo hatutarajii awe hivyo, akiamua kuwaonea watu wanaodai haki, hatawamaliza. Marehemu hakuwamaliza, naye akawafuata aliowatanguliza.

Duniani ni kituo wakati tukiwa safarini. Tenda wema, itumikie haki, usitumikie chama wala magenge ya waonezi.
Kwa hiyo hasira zenu Kwa.Magu mnataka kuzimalizia Kwa Mama Samia, Kwa hizo papara zenu mtasubiri sana
 
MBOWE NAE ANAMTISHIA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA. MKUU WA DOLA NA BOSI WA NCHI HII.
KUMBE JPM ALIKUWA SAHIHI SANA KUWANYOOSHA HAWA MAPIMBI.
 
neno MKATILI ni relative sana kwani linaweza kuchanganya kusimaia sheria za nchi (ambazo ni za kimabavu naturally) na kuonea raia (ambalo ndyo watu hatutaki). kwani Golda Meir alipokuwa anawapiga na kuwaua waarabu, au Margareth Thatcher alipokuwa akiwabana Labour party kisiasa walikuwa MAKATILI?

..huenda Golda Meir aliungwa mkono kwasababu alikuwa akiua Waarabu na sio Wayahudi wenzake.

..Unadhani Mama Samia anaweza kuwa maarufu na akajijengea heshima kwa kuwa mkatili dhidi ya Watanzania wenzake?

..Binafsi naamini Mama Samia atajiharibia ikiwa atatawala kwa mkono wa chuma kama alivyotawala Magufuli.

..Kama kuna jambo la awamu ya 5 ambalo Watanzania hawataki Mama Samia aliendeleze ktk awamu ya 6 ni tabia za kikatili dhidi ya viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
 
Mkuu wewe ni miongoni mwa members ambao kwa kweli wakini-quote huwa nawaheshimu sana. Heshima yangu kwako ipo juu sana mkuu.

Unajua kinachopelekea haya mambo yatokee.

Hivi Mheshimiwa Mbowe kama kiongozi mkubwa tu, anaongeaje maneno aliyoyaongea kumjibu Rais wa nchi??? Ndio kweli tukae kimya tu????
Fikra zake kwamba Mama atakubali kuingilia muhimili wa Bunge na kuwaondoa wakina Halima Mdee na kitendo kuchelewa kupewa jibu la kukaribishwa ikulu limewafanya CHADEMA wapaniki.
 
Msimuendeshe kama mlikuwa mpo desperate hivi mngefanya kweli enzi za UKUTA alipowaambia msinijaribu ...mkaufyata, mmemkuta Mama hana makuu mnaanza kuzingua sawa tusubirie tuone.
Hivi kua rais ndo kua na Hati miliki ya TAIFA , yote aya ni tokana na Katiba mbovu , Yani mtu anakua kiongozi mnamjaza utukufu kuliko mungu, MPAKA mnakufuru, iko ivi siku zote haki ushinda maovu, anaweza fanya lolote KWA sababu ni Rais ila mwisho wake usiwe mzuri , kwani atafikisha miaka mia akiwa rais
 
Vyombo vya usalama/ulinzi vina namna ya kutuliza ghasia kama wanaghasia hawatii sheria,hivyo walikuwa wanatekeleza majukumu,LAKINI yasingetokea hayo bila chadema kwenda kuwafitinisha

..Yote hayo yalitokea kwasababu ya kulazimisha ushindi wa CCM.

..Badala ya kuua watu, kuwatia ulemavu, na kuwafunga wengine, CCM ingeweza kubadili sheria ili wabunge waweze kuhama vyama bila kulazimisha uchaguzi kurudiwa.
 
Hivi kua rais ndo kua na Hati miliki ya TAIFA , yote aya ni tokana na Katiba mbovu , Yani mtu anakua kiongozi mnamjaza utukufu kuliko mungu, MPAKA mnakufuru, iko ivi siku zote haki ushinda maovu, anaweza fanya lolote KWA sababu ni Rais ila mwisho wake usiwe mzuri , kwani atafikisha miaka mia akiwa rais
Tuonesheni mfano kwa kumuambia Mwenyekiti wa kudumu kupisha na wengine pia waongoze dooh!!!
 
Kama Mbowe alisumbuliwa tu na DC Sabaya....ataweza kumsumbua mh.Rais na CCM yake ?!!!

Jamaa BOYA SANA HUYU.....
Upeo wako ni mdogo kiasi kwamba Huwezi kuona hata chembe yaliyokuwa nyuma ya pazia mpaka Sabaya kafika hapo alipo, Halafi unamsifu Sabaya kwa Ouvu wake.
 
..Kama kuna jambo la awamu ya 5 ambalo Watanzania hawataki Mama Samia aliendeleze ktk awamu ya 6 ni tabia za kikatili dhidi ya viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
Hilo la "tabia za kikatili" ni hisia ambazo hazijanishawisi; kusimamia sheria kunahitaji matumizi ya mabavu nandiyo nature ya utendaji wa serikali. Sasa ukivunja sheria halafu serikali ikakupiga rungu usiseme huo ni ukatili, ndivyo serikali inavyofanya kazi.
 
Huyu Mbowe naona Sasa anatafuta kurudi Dubai! Hamjui Mama,asimuone mpole vile,anaweza akawa Mkali zaidi ya Magu hasa ukiingia mwenyewe kwenye angaa zake! Mama alisha sema "Ukinizinguwa,tunazinguwana'!!
Ngoja tuone mahali "venom" yake ilipo.
 
Tuonesheni mfano kwa kumuambia Mwenyekiti wa kudumu kupisha na wengine pia waongoze dooh!!!
Kwani Kuna popote Ssh rais amekataliwa asiongoze ! Au Katiba inamzuia asiongoze? Yeye ata akiongoza KWA miaka 100 no one care,ilihali amechaguliwa Katika uchaguzi huru na haki , mbona akuna shida, Sasa mnaogopa Katiba MPYA kisa nini?

Maana ccm mkisikia Katiba mnachanganyikiwa tatizo nini
 
Back
Top Bottom