Tume ya Warioba ilitoa elimu ya katiba Wananchi wana uelewa waziri wa katiba asipotoshe

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau wenye AKILI KUBWA tulijua mapema sana kuwa Kitendo cha CCM kuvuruga ule MCHAKATO wa KATIBA MPYA ndani ya BUNGE la KATIBA ulikuwa wa Kukataa KATIBA MPYA.

Kuthibitisha hilo
1. Magufuli alipoingia Madarakani alisema KATIBA MPYA sio Kipau Mbele na pia Serikali yake HAINA BAJETI yake licha ya kuwa Ajenda ya KATIBA MPYA ilikuwa kwenye ILANI ya UCHAGUZI ya CHAMA Chake.

2. Rais Samia yeye hakukataa bali badala ya kuendeleza Tulipoishia kwenye BUNGE la KATIBA akaamua tuanze Upya kwa Kuunda KIKOSI KAZI.

3. Leo WAZIRI wa SHERIA anakuja na Hoja kuwa Wananchi hawaijui KATIBA Waziri anasahau kuwa Tume ya WARIOBA iliwaelimisha Wananchi kwa kuzunguka NCHI NZIMA na kupokea Maoni na Mapendekezo yao baada ya KUWAELIMISHWA.

CCM inajitahidi kuchelewesha MCHAKATO wa UPATIKANAJI wa KATIBA MPYA kwa Kuja na VIJISABABU visivyo na TIJA.

WANANCHI tunataka KATIBA MPYA kabla ya UCHAGUZI MKUU 2025.

20230829_171642.jpg
 
Back
Top Bottom