Mbowe ashikiliwa Central Police

Mbowe ashikiliwa Central Police

Hakuna aliye juu ya mahakama. Tusiwe vipofu wa sheria. Mbowe ni mtanzania kama wengine wote,, anapokiuka amri ya mahakama, sheria inachukua mkondo kama kawaida. Yeye ni nani aidharau mahakama? Mbowe yuko salama, na kila kitu kitafanyika kufuata sheria, wewe unayewashauri wenzako, utajikuta peke yako mahakamani. Watanzania si mbumbumbu wa sheria siku hizi.
Mahakama iko kwa ajiri ya nani?Wapinzani na walalahoi?Mifisadi iliojaa CCM pamoja na JK mwenyewe imefuja na inaendelea kufuja rasilimali zetu inaendelea kudunda na kutanua na hata huku ndani ya chama inafahamiana badala ya kuchuliwa hatua za kisheria inaendelea kutuimbia nyimbo za kujivua magamba huu ni wakati muafaka kwa nguvu ya umma kuchukua mkondo wake.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kama kuna uwezo wa kumkamata mtu Jumamosi basi na uwezekano uwepo wa kumuwekea dhamana hizo siku kama haiwezekani basi wasikamate watu siku zisizoweza kuwekewa dhamana kwani haki inatakiwa iwe sawa.

Hiyo kesi inakuwaje haiishi kwani kila kitu kipo wazi au ina maagizo kutoka juu???

Ndio sheria za nchi inayotawaliwa na mafisadi, sheria zinaruhusu mtu akamatwe Jumamosi lakini sheria hiyo hiyo hairuhusu mtu huyo kuwekewa dhamana mpaka baada mwisho wa wiki kwisha.
 
Pipozzzzzzzzzzz pawaaaaaaaar
Tunasubiri tamko la CDM tu,ttulio tayari kwa ukombozi tuzame street kwa ukombozi.kwani
"ni bora ufe ukipigania ukombozi,kwani hata usipojitokeza utakufa kinyonge kwa malaria,kipindupindu au ajali za barabarani"
kukubali kuishi chini ya magamba ni sawa kabisa na ku opt kifo,kwani watanzania wengi wameshakufa wakiwa hai kutokana na ufisadi na udhalimu wa magamba na taasisi zake kandamizi.
 
naona viashilia vya ccm kuondoka madarakani kwa nguvu yetu/nguvu ya umma,mh.mbowe kasema yuko tiyari kufa amesimama kuliko kuishi amepiga magoti,mimi pia nipo tiyari kufanae tukiwa tumesimama!!! Imetosha!! Sasa basi wajinga wakubwa hawa watawala,wanafiki majizi.mashetani!!! Hivi Mwalimu nyerere aliyajua haya shetani?
 
hali hii ya kuonewa itakomeshwa kama watu wataamua na kuungana pamoja na naomba wana-Arusha na wanaharakati popote mlipo mhakikishe mnamsaidia mwanaharakati mwenzetu ili watawala wajifunze vinginevyo ukombozi kwetu ni NDOTO

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WOTE WANAOPIGANIA HAKI.


Chombeza hiyo!!! Funga safari ukashiriki.
 
Acheni kuzungumza tu..CCM wanafanya hivi kuwapunguza makali CHADEMA..maana hali yao ni mbaya wako ICU kwa sasa..hata kama Mbowe angetoa taarifa za kuomba udhuru wa kutokuwepo mahakamani mara hamsini bado wangemkamata..kwani lengo lao ni kuwapunguza nguvu na kuwatisha CHADEMA...lakini hawajui idadi ya watanzania ambao wako tayari kufa wakipambana kuitafuta haki yao wanaongezeka kwa kadri wao wanavyoendelea kufanya upupu wao..Na ipo siku hawataamini yatakayotokea,na yaonekana wana uelewa mdogo..nyie mnaotetea hii serikali yenu ya magamba...kawaambieni ipo siku watakuja kufahamu hawana silaha za kutosha kuuangamiza umma wa watanzania wote waliochoshwa na maovu yao..na wakati huo ukifika tutakuwa tunawagonga nyundo kwenye macho yao,mapanga shoka na vinginevyo,kama nitakuwa nimekufa mimi yupo atakayekuwa hai..narudia tena
kawaambieni ipo siku watakuja kufahamu kuwa hawana silaha za kutosha kuuangamiza umma wa watanzania wote waliochoshwa na maovu yao

Huoni kama hii ni kununua umaarufu kwa Mbowe? Mbona wenziwe walienda baada ya kutishiwa kukamatwa? Ukweli wenyewe ni kuwa huko aliko sio keko lakini asingefanya mchezo huo. Mimi naona ni kutumia vitendo nyie wenye nguvu ya wananchi badala ya kuendeleza malumbano>
 
Kwa nini wasimkamate Ijumaa siku ya kazi? wamesubiri hadi Jumamosi wakijua fika kwamba kupata dhamana itakuwa nguvu- huu ndio ubabe= state intimidation!


Na kwanini hasa ashindane na mahakama kwani anaogopa nini wakati anajuwa hana makosa? Huku kuidharau mahakama hakuna maana na badala yake unajikuta kwenye matatizo bure. CHADEMA ina mahelkopta kwanini asiende alikoitwa kwa kutumia helkopta?
 
Ndio sheria za nchi inayotawaliwa na mafisadi, sheria zinaruhusu mtu akamatwe Jumamosi lakini sheria hiyo hiyo hairuhusu mtu huyo kuwekewa dhamana mpaka baada mwisho wa wiki kwisha.

Mimi najiuliza, Dhamana hiyo apewe na nani iwapo dhamana inatolewa mahakamani au polisi. Polisi wameshaamriwa wamkamate kwa kukiuka dhamana na mahakama haifanyi kazi siku hiyo, sijui lawama zinakujaje? Hapa kuna mambo mawili, moja ni sheria zetu tulizoziweka na la pili ni uamuzi wake mwenyewe Mbowe kuidharau mahakama kwa sababu anazozijuwa mwenyewe. Nafikiri ingekuwa busara tukangojea utetezi wake mahakamani kwani ni yeye anaeelewa kwanini alifanya alivyofanya.
 
mwandishi mwangulumbi alisha andika kuwa hawa jamaa ni mbwa wa watawala wanabweka pasipo na haja,wanabweka au kung'ata wakiambiwa kufanya hivo na wanaowafuga mbwa hao GP AND MK.sasa wamezunguka wanabweka,wanambwekea mh.mbowe,mapinduzi ya uhuru wa kweli yataanza naMBWA hao,then kwa wafuga mbwa! Kibaya zaid mengine majibwa koko!!
 
Hili nibaraza la vijanaa au Baraza la Vijana au Baraza la Vichaa(BAVICHA) Mbona wanapenda kukurupuka!Muda mfupi vijana na wadau wa CDM Wame2ma sms za kufurah kuwa Jk amepata ajal ilimradi 2 waonekane wanauchungu,cniupumbavu kuona kuwa Mboe anasukwa sukwa 2 tatizo je nae Wakiambiwa nae amekufa watafanyaje? Minawapoza 2 ila cku wakisema wanaingia knye target za Magamba 2 patachmbika.muwage wapole mcje mkadhani kuwa wa2 hawawasomi!watu wanaham na ninyi mlianzishe 2 wakubwa.msifanye tabu jamani eeeeh.

Wewe mazafanta acha vitisho vyako vya kijinga wewe,eti wanasoma na wanangoja tu,unadhani mtafanya hivyo mpaka lini??acha ujinga wako na fikra duni zisizo na mpango,kwa vile mmeshindwa kutetea points mnaamua kutumia nguvu au sio???sasa mtaweza???
 
Nimekatishwa tamaa na uamuzi wa Mbowe kujipeleka polisi mwenyewe. Najiuliza ni kwa nini amekiuka matamshi ya mdomo wake na maandiko ya chama chake yaliyotolewa na Lisu?
Hivi jamani naomba mnijuze ukweli kama alijipeleka mwenyewe au vipi..... kama ndivyo basi ana matatizo ya kutujengea imani upya juu yake. Ikiwa polisi walimkamata kwa nguvu basi anapaswa kusaidiwa na nguvu ya Umma ili kuionesha serikali kuwa mafisadi hawapaswi kuwa huru barabarani wakati mbowe akiwa Rumande.
 
HECHE AUNGURUMA KUKAMATWA KWA MHE MBOWE,BAVICHA WATOA SAA 48 AACHIWE HURU
Mwenyekiti wa baraza la chadema (BAVICHA) John Heche amekemea vikali na kulaani kitendo cha polisi kumkamata Mwenyekiti wa Chadema Mh mbowe kwani ni kinyume cha sheria.
Heche ametoa kauli hiyo wakati akiwa katika chuo cha sauti jijini Mwanza wakati alipokuwa akikabidhi vyeti kwa wahitimu 55 wa chadema chuoni hapa.
Amedai kuwa vitendo hivi vimezidi ambapo ndani ya miezi 3 karibu viongozi wote wa juu wa chadema na baadhi ya wabunge wameshakamatwa na kudhalilishwa,ametoa mfano wa viongozi waliokamatwa ni pamoja na Mbowe,slaa,Lema,Ndesamburo,Tindu Lissu,Esther Matiko na Zito Kabwe,pamoja na wafuasi wao wengi.
Amesema kwa sasa BAVICHA halipo tayari kuona viongozi wao wakidhalilishwa na kunyanyaswa,wametoa saa 48 Mh Mbowe aachiwe huru ambapo kesho BAVICHA watatoa kauli kuhusiana na unyanyasaji huo ambao amedai kuwa umeanza kuwa utamaduni,amesema sasa imetosha.
Ametoa mfano mbunge wa CCM (Busega) Dr Kamani alipotakiwa kuhojiwa na polisi ilibidi polisi waombe kibali kwa katibu wa bunge,amehoji kuna utofauti gani wa kisheria kati ya mbunge wa upinzani na CCM katika kukamatwa au kuhojiwa na polisi?.
Amesema Mh Mbowe licha ya kuwa ni mbunge ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo anasimama kama waziri mkuu kivuli,amewataka vijana wa Chadema kuwa tayari kwa tamko la kesho.

Wamepigia hesabu sawasawa kwani masaa 48 atakuwa mahakamani kuomba radhi ili aachiwe. Kama kweli hawa BAVICHWA hawajuwi hili danganya toto ya Mbowe wangetowa masaa7 tu atolewe na kama sivyo .......
 
Wanaharakati wa ukweli tupo tayari kwa lolote popote saa yoyote maana hii mizimu miwili ilioungana ya ccm na polisi haitosheki kuwaangamiza watanzania iwe kwa mtutu wa bunduki au ugumu wa maisha, tujipange kuulipua moto wa maandamano nchi nzima uzimwe na umoja wa mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani kama wenzetu Waarabu, vipi 15% itunyanyase 85%?

Mbona amri ya kukamatwa imetolewa na Mahakama baada ya Mbowe kuamuwa kuvunja sheria!! Polisi na CCM wanahusikaje? Wahusika ni Mbowe mwenyewe na Mahakama wanaoonyeshana ubabe!
 
Heche usilete balaa nyingine hapa... Tatizo si la Mbowe na polisi. Polisi hawajamkamata ili wamuhoji au kuna tatizo na mbowe ila anakamatwa kama kutimiza matakwa ya Mahakama. Heche usisahau kuwa kuna nguzo tatu - Mahakama, Bunge na Dola. Mahakama imeamuru dola kutekeleza wajibu fulani na dola inatekeleza ila kama kuna udhuru dola inautoa kama ilivyotokea kwa mgombea binafsi. Serikali ilikata rufaa. Dola haijaona kosa kumkamata mbowe hivyo wametekeleza wajibu wao. Anne Makinda pia anao wajibu wa kumtetea Mbowe lakini labda ameshatoa kibari cha polisi kumsomba .....who knows?

Tusubiri uamuzi wa Mahakama bila kuweka mashinikizo. Hakimu atamwacha huru tu kwani hiko wazi kuwa waliomba ruksa na mdhamini wake alikuwa mgonjwa hakuja so no problem to Mbowe.........
 
Mbona amri ya kukamatwa imetolewa na Mahakama baada ya Mbowe kuamuwa kuvunja sheria!! Polisi na CCM wanahusikaje? Wahusika ni Mbowe mwenyewe na Mahakama wanaoonyeshana ubabe!

Kwa nini wamkamate weekend???inahusuika vipi hii taratibu??kwa nini wasingesubiria mpaka siku za kazi???fikiria kwanza......
 
Back
Top Bottom