SoC03 Mbinu zipi zitumike kuongeza watumiaji wa mtandao wa Jamii forums Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Afrocentric view

JF-Expert Member
Jun 19, 2022
1,373
2,267
Tangia Jamii forum ianze miaka 17 iliyopita, mpaka leo bado ina watumiaji laki 6 na kidogo tu. Hii idadi ni ndogo sana kulinganisha na idadi ya watanzania wenye uwezo wa kumiliki simu janja.

Hii ni hasara kwa jamii kwakuwa hatuzivuni faida nyingi za watu kuwa katika huu mtandao kuliko mitandao mingine kama facebook,instagram,tiktok nk.

Kazi kuu nne za mitandao ya kijamii ni kuunganisha watu, kuhabarisha, kuburudisha na kufunza.

Mitandao mingine inafaulu sana kwenye kuunganisha watu na kuburudisha lakini inapungua sana kwenye kuhabarisha na kufunza. Jf pia inafaulu kwenye kuunganisha watu na kuburudisha lakini hapa kwenye kuhabarisha na kufunza ndipo inapofaulu zaidi na kujitofautisha na mitandao mingine.

Zipo sababu nyingi lakini nadhani kuu mbili zinazoifanya jf iwe juu ya platform nyingine ni;

1. Jf imejikita kwenye mada na sio watu wanaopost mada kama mitandao mingine: Ukifungua mitandao mingine unakutana na mada/post za watu uliowafollow au za aina hiyo, lakini ukifungua Jf utakutana na mada mbalimbali zinazojadiliwa na watu tofauti na unakuwa na access ya kuona post ya mtu yeyote. hii inafaida zifuatazo;

a)Wigo: Uwanja wa vitu utakavyovipata Jf ni mkubwa kuliko mitandao mingine kwasababu
mtumiaji haubanwi kuona vitu vya watu uliowafollow pekee, mfano instagram kama umefollow page za udaku, basi utaona udaku pekee. Lakini Jf unapata content za watu wote kutoka majukwaa mbalimbali ya siasa,elimu,sayansi,teknolojia,biashara,michezo,nk.

b)Ukuzaji (Promotion): Kwasababu msisitizo ni mada kuliko watu huku jf, basi hata watu wenyewe wanaoanzisha mada wanajaribu kuiuza mada zaidi kuliko kujiuza wenyewe. Kujiuza mwenyewe namaanisha ile mtu anapost picha ili aonekane yeye, vitu vyake, watu wake au maisha yake ili aongeze umaarufu wake lakini kimsingi haimnufaishi kwa lolote mtazamaji. Kuuza mada ni ile mtu anapost kitu kuongelea mada na ideas general(hata kama akitumia maisha yake kama mfano) ambazo jamii inaweza kujifunza au kuburudika kwazo. Members wa jf wakiongelea maisha yao hawaishii kutuhabarisha tu, bali inabidi waongeneze maelezo ambayo wachangiaji watavuna mafunzo/burudani kwayo.

c) Uchujaji: kwasababu mada ni kipaumbele basi mada nzuri ndizo hutrend, hivyo ukiingia Jf unakuwa na uhakika wa kukutana na mada nzuri nyingi kuliko mitandao mingine. Watu maarufu unaowafollow instagram hata wakiandika pumba itakulazimu uzione, lakini jf mtu anaweza kuwa hajulikani na hujamfollow lakini akaandika mada nzuri ukaiona.

d) Access/Reach: Mtu yeyote anaweza kuanzisha mada Jf na kuwa na uhakika wa kuifikisha kwa watu wengi bila kuhitaji yeye kujulikana (kama unavyonisoma hapa). Mfano ili ufikishe ujumbe kwa watu 10,000 instagram inabidi uwe na wafuasi 10,000 lakini jf unaweza kufikisha ujumbe kwa hao watu bila kuwa na mfuasi hata mmoja.

2. Faragha na kutojulikana kwa watumiaji (Privacy and anonymity)
Ni ngumu kwa mtu kufuatilia na kujua maisha binafsi ya watumiaji wa Jf. Hii inasaidia kuongeza

a) Uhuru wa maoni: Kwasababu maisha binafsi ya watumiaji hayajulikani imeongeza uhuru wa watu kuhabarishana,kuanzisha au kuchangia mada yoyoye ile bila kuwa na aibu,hofu ya mamlaka, au hofu ya kupata madhara yoyote kwenye maisha yao binafsi kutokana na michango mtandaoni. Vyombo vya habari vinaweza kununulika visiwe huru lakini Jf kuna uhuru.
Watu huongelea mawazo yao ya kisiasa,mahusiano,michepuko,dini,nk. ambayo wasingeweza kuyaongea kama utambulisho wao ungejulikana kama mitandao mingine.
Ofcourse wazee wa chai na propaganda hawakosi, lakini atleast huku kuna uwezekano mkubwa wa kupata mawazo ya watu ambayo hayajachakachuliwa na kuchujwa kwa kuhofia jamii itanichukuliaje.

b): Taarifa nyeti(Exclusive content & Whistleblowing): kutokana na hizo sababu juu, Jf ndipo jukwaa pekee ambapo unaweza kukuta taarifa nyeti ambazo huwezi kuzipata sehemu nyingine.


Hivyo Jf ni mtandao wa kipekee uliochongwa vizuri kuongeza maarifa na elimu ya vitu mbalimbali kwa jamii.

Watu wanaotumia jf huonekana magenius mtaani. Na wao pia huona kama jamii kubwa ya watanzania bado ipo gizani. Utakuta mada inatrend Jf kuhusu mambo ya msingi yenye maslahi mapana ya taifa, watu huijadili kwa mabishano ya hoja za uweledi, lakini ukienda mtaani unakuta mada inayotrend ni zilezile za Soka tu au maisha ya watu maarufu. Watu hawana habari yoyote kuhusu vitu vya msingi kwa taifa lao. Jiulize, ni vipi asilimia hata 50% ya watanzania wangekuwa Jf ingekuwaje?

Najua kuna raha unajisikia ukienda kijiweni na kuonekana mwamba unajua vingi, lakini hilo sio jambo la kufurahia kwasababu kiupana zaidi inadhihirisha kiasi gani jamii kubwa ipo gizani na inahitaji kuamshwa.

Kuna umuhimu mkubwa kwa Wahusika wote wa Jf kuhakikisha tunaipromote kwa kadri ya uwezo wetu ili kuiamsha jamii.

Baadhi ya mbinu zinazoweza kutumika

1. Kufanya watu wengi zaidi waujue umuhimu na faida za jamii forum: Hii ni kama nilivyofanya hapo juu.

2.Kupromote nyuzi zinazotrend:
Najua hii inaenda kinyume na mawazo ya wengi wanaosema kuwa ni bora kupromote majukwaa, kwakuwa jamii inapenda mada za kijinga hivyo ukipromote trending basi mada za kijinga ndio zitakuwa zinaonekana tu, Na hilo linaweza kuwa kweli lakini tujaribu kuangalia hii kutoka angle nyingine.
Kwakuwa mada itakayotrend ni mada inayopendwa na wengi,basi hii ni njia pekee ya kuleta watu wapya hapa Jf maana watafuata zile mada wanazopenda hata kama ni za kijinga. Wakishafika jf na kuburudika na mada hizo, ndipo watapata access ya kuona mada zingine kutoka majukwaa mengine ambazo wasingeziona bila kwanza kuvutiwa na mada za kijinga na kujiunga Jf. Hongera kwa uongozi wa Jf Hili limeshafanyika

2. Promotion na matangazo: Uongozi wa Jf waongeze kuutangaza mtandao kupitia magazeti, majarida, mitandao ya kijamii, media mbalimbali na page za watu maarufu ili kuongeza idadi ya watumiaji.

3. Kuanzisha/Kuendeleza events,sherehe na mikutano mbalimbali ya hadhara kuongeza utambuzi (awareness) ya jamii kuhusu mtandao huu.

4. Watumiaji tuongeze bidii ya kuutangaza mtandao huu kwa jamii inayotuzunguka kwa kuwaunganisha ndugu,jamaa na marafiki wetu kwenye huu mtandao. Jf waboreshe muonekano, mtumjaji aweze kuitumia kwa wazi bila kuhofia ID yake ya jf kujulikana ili tuache tabia ya kutumia jf kwa kujificha.
Pia Jf wanaweza kutoa zawadi kama hamasa kwa watu watakaotuma link ya kuleta members wengi zaidi.

5. Kusaidia kampeni ya kuongeza idadi ya watumiaji wa simu janja hapa nchini.
Sikuhizi kuna simu za mikopo, tusaidie jamii kutambua hili na kuhakikisha watu wengi zaidi wanamiliki simu janja.

Mdau mwenzangu unadhani ni mbinu gani zingine zinaweza kusaidia kuongeza watumiaji wa jamii forums Tanzania?
 
haka kamtandao kangewaacha watu huru ingekuwa ni bonge la mtandao.eti ukimtukana mjinga anaenda kukusemea unapewa ban🤣🤣
 
Jeiefu yenyewe ina account mitandao yote inayooperate hapa Nchini, na Haimasishi Watu kujiunga nayo, sisi ni nani tushupaze shingo kuwatafutia Mkate hawa Jeiefu.
 
Jeiefu yenyewe ina account mitandao yote inayooperate hapa Nchini, na Haimasishi Watu kujiunga nayo, sisi ni nani tushupaze shingo kuwatafutia Mkate hawa Jeiefu.
Hili ndilo linatakiwa libadilike
Sio sifa eti jf kuwa mtandao wa watu wachache
We unadhan hata nusu tu ya watanzania wangekuwa huku.
Mapinduzi gani yangefanyika kwenye siasa,elimu,uchumi na biashara?
 
Ofcourse wazee wa chai na propaganda hawakosi
images (3).jpeg

☕Kama☕
 
Back
Top Bottom