Hivi watumiaji wa mtandao wa JamiiForums ni Maroboti ama Alliens?

Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,742
4,932
Huwa najiuliza sana hili swali.

Hivi nyie wakuu huwa mnatumia wapi mtandao huu pedwa ni huwa mnajificha ama? Walahi sijawahi kushuhudia mtumiaji yeyote yule akiperuzi waziwazi huu mtandao. Nimeshuhudia raia wakiperuzi waziwazi mitandao ya kijamii kama vile Instagram, WhatsApp, Facebook nakadhalika ila sio huu wa JF.

Mpaka huwa nabaki na maswali mengi sana, ama nyie ni maroboti au alliens? Ama ni vile huu mtandao bado haujajulikana sana kama mitandao mingine? Lakini hapa hapana watumiaji wa mtandao huu ni wengi sana Tanzania hii, sasa wakuu mbona huwa siwagumii kabisa mkitumia huu mtandao?

Wakuu huwa mnatumia huu mtandao mkiwa wapi? Maana katika mtandao nina uraibu nao ni huu wa JF ni unashika namba moja kabisa. Au wakuu sisi watumiaji wa JF tuko sayari nyingine kabisa?
 
Asilimia kubwa ya watumiaji wa huu mtandao ni magenius na wako smart sana kiujumla, kwahiyo sio rahisi mtu mwenye sifa kama hizo kujionyesha onyesha eti akiperuzi mara huku mara kule. Huwa nashangaa sana mtu yuko kwenye kadamnasi ya watu ni ana peruzi tu mitandao ya kijamii.

Binafsi yangu huwa napenda kutumia mitandao ya kijamii nikiwa peke yangu nimetulia mahala, sio kila sehemu nitoe simu nitumie, hapana kabisa.
 
Huwa najiuliza sana hili swali.

Hivi nyie wakuu huwa mnatumia wapi mtandao huu pedwa ni huwa mnajificha ama? Walahi sijawahi kushuhudia mtumiaji yeyote yule akiperuzi waziwazi huu mtandao...
Tuko kwenye ofisi zetu, tunakaa peke yetu, tunaenda kwenye magari yetu tuko peke yetu, kisha tunaenda nyumbani. Hapa hatutumii JF hadi labda mpenzi alale.
 
Huwa najiuliza sana hili swali.

Hivi nyie wakuu huwa mnatumia wapi mtandao huu pedwa ni huwa mnajificha ama? Walahi sijawahi kushuhudia mtumiaji yeyote yule akiperuzi waziwazi huu mtandao. Nimeshuhudia raia wakiperuzi waziwazi mitandao ya kijamii kama vile Instagram, WhatsApp, Facebook nakadhalika ila sio huu wa JF.

Mpaka huwa nabaki na maswali mengi sana, ama nyie ni maroboti au alliens? Ama ni vile huu mtandao bado haujajulikana sana kama mitandao mingine? Lakini hapa hapana watumiaji wa mtandao huu ni wengi sana Tanzania hii, sasa wakuu mbona huwa siwagumii kabisa mkitumia huu mtandao?

Wakuu huwa mnatumia huu mtandao mkiwa wapi? Maana katika mtandao nina uraibu nao ni huu wa JF ni unashika namba moja kabisa. Au wakuu sisi watumiaji wa JF tuko sayari nyingine kabisa?
Unataka kututeka?
 
Huku ndani Kuna members kibao tu ambao Ni waheshimiwa wa kuu wa wilaya, mikoa na mawaziri mama Samia mwenyewe yupo humu sema kitu kinatunyanya tusiogopane ni vile tunatumia majina feki.

Kuna kipindi nilikutana na Mh mmoja kwenye kikao katika story za hapa na pale akanipa simu nimuandikie namba yangu kidogo notification ya Jf ikaingia hapo ndo nilipoanza ogopa kujibu watu vibaya humu
 
Mtandao unawatumiaji laki 6.5..Tanzania inawatu Million 60+ watumiaji wa simu ni Mil 30 katika hao..wenye access na internet ni Mil 21 kwa mujibu wa TCRA.

Katika hao 21M kuna watu laki 6 tu ambao ni sawa na 0.5% sasa hao robot au watu wakukutana nao wanaotumia JF ni mtihani labda Mungu tu aamue kuwakutanisha
 
Sasa kama mume tuu hajui kama mimi ni member huku...ndo ujue tuna dumisha neno Privacy..and anonymity zetu.. 😆 😆 mimi namwambia tuu naipenda sana JF kuperuzi ila hajui kama nina ID huku.

Nisingekua huru kuchangia..yani hata marfk wa karibu najua wana ID huku ila kila mtu anakwambia hana...
 
Back
Top Bottom