Thanks JamiiForums members!

MR MONEY08

Member
Oct 21, 2022
61
26
Habari zenu jamii forum members, aisee nilikuwa nikifuatilia jamii forum Kwa muda mrefu tangia mwaka 2012 , yaani miaka 12 iliyopita, japo am new member here.

NIMEJIFUNZA MAMBO MENGI. Na nimeona wasomi wa humu au labda, wakishua au watu wakawaida tu, wako fair katika kutoa mawazo, na michango mbalimbali ya mawazo.

Kama ni wasomi watoao mawazo na michango humu, wale waliopo kwenye nyadhifa mbalimbali na waajiriwa wenye nyadhifa kubwakubwa za uongozi kwanini wasiwe kama Hawa?

Kupitia jf, nimeweza kutimiza baadhi ya mambo kama vile kutravel nje ya Tanzania kwa kufuata miongozo Yao, pia nilipata kazi maana nilisota mda mrefu bila kupata kazi, na Sasa naona mwanga kwa mbali wa kutimiza malengo yangu, na ninaamini yatatimia. Nafuata miongozo wa ushauri uliotolewa na member Fulani humu aliesema kosomee hotel, then nenda dubai.

Thanks Jamiiforums
 
Back
Top Bottom