Kuna umuhimu wa mtoto kumiliki simu mapema?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,961
Reaction score
67,517
Nakumbuka mm nilianza kutumia simu yangu ya kwanza baada ya kumaliza kidato cha nne na sio kununuliwa na mzazi nilinunua mwenyewe

Ila now naona watoto wapo shule ya msingi mzazi kamnunulia mtoto simu wengine wana diliki hadi kuwa promise mwezi ujao nakununulia simu

Kuna umuhimu huo au ni ulimbukeni wa wazazi kwamba watoto wao waonekane wakishua sana au?

Impact kuna mtoto shule ime funguliwa mda mrefu yupo form 2 lkin mpaka sasa mtoto hajaenda shule na nyumabn hayupo lakni simu yake yupo on na ana wasiliana kama kawaida wazazi nao hawajali wapo bise na kazi wana amin mtoto kafika shule

Au tusi washauri kila mtu amlee mtoto vile ana weza kwa upande wake sio?
 
Haina umuhimu na ki sayansi haina tija kwa watoto.

Wenzetu wazungu wameshaweka restrictions kabisa.

Shida ya sisi wabongo huwa tunaiga kila kitu bila kufuata ushauri wa kitaalamu.
Wataalam gani kijana ,
Wewe pia ni mbongo unaesubiri wataalam wa kizung waje wakushauri.
Maana huwez kujishauri
 
Haina umuhimu na ki sayansi haina tija kwa watoto.

Wenzetu wazungu wameshaweka restrictions kabisa.

Shida ya sisi wabongo huwa tunaiga kila kitu bila kufuata ushauri wa kitaalamu.

Elimu inatakiwa kwa wazazi mm sikubaligi na usem wao wanasema maisha nilio pitia mimi sitak mwanangu apite hana sahau maisha hayo alio pitia ndio yame mfanya kuwa bora na jasiri kwa kiasi fulan mpaka watu waka mpenda na kumpa nafasi zaidi ya kupambana
 
Kwasabb una jua effect zake
Kwanza mimi wanangu husoma day kwa hiyo niko nao muda wote.
Nikisafiri kuna simukwa ajili ya mawasiliano,, kuna laptop ya kazi za shule wanafanya na baba yao hiyo laptop alishapiga kufuli baadhi ya mitandao.

Sasa si kwamba najua madhara pia hata sioni sababu ya kuwapa simu hizo kabla ya muda niliopanga.
 
Elimu inatakiwa kwa wazazi mm sikubaligi na usem wao wanasema maisha nilio pitia mimi sitak mwanangu apite hana sahau maisha hayo alio pitia ndio yame mfanya kuwa bora na jasiri kwa kiasi fulan mpaka watu waka mpenda na kumpa nafasi zaidi ya kupambana

Mbongo akishashika pesa, humuambii kitu!

Kumbe hatujui tunaharibu vizazi vijavyo kwa ulimbukeni!

Kwanza mimi wanangu husoma day kwa hiyo niko nao muda wote.
Nikisafiri kuna simukwa ajili ya mawasiliano,, kuna laptop ya kazi za shule wanafanya na baba yao hiyo laptop alishapiga kufuli baadhi ya mitandao.

Sasa si kwamba najua madhara pia hata sioni sababu ya kuwapa simu hizo kabla ya muda niliopanga.
Mama bora wa Kitanganyika.
 
Kila mtu alee mtoto wake.
Lakini binafsi mimi wanangu huwa wanaanza kumiliki simu baada ya kumaliza form six chini ya hapo atatumia yangu.
Huyo unayesema alee mtoto wake ajuavyo, ndiye mkweo siku si nyingi!

Mwisho wa siku mwanao anakuja kupata mume/mke wa ajabuuu.

Kwanza mimi wanangu husoma day kwa hiyo niko nao muda wote.
Nikisafiri kuna simukwa ajili ya mawasiliano,, kuna laptop ya kazi za shule wanafanya na baba yao hiyo laptop alishapiga kufuli baadhi ya mitandao.

Sasa si kwamba najua madhara pia hata sioni sababu ya kuwapa simu hizo kabla ya muda niliopanga.

Wamepata wazazi wazuri
 
Back
Top Bottom