MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

FukuuuuZa mbwaa haao na wafungwe kwa kosa jalibio la kuua, aseee ewee mwalimu gusa mtoto wangu uone doso nitakalokuja kukupa na extra drills za kutosha had nikumalize
[emoji123][emoji109][emoji109][emoji109][emoji109]
 
Amefanya watu wapoteze kazi!!

I heard kua walimu wote wa pale wamefukuzwa!
Sina hakika lakini
Huyu mkuu inabidi akawd secretary ubalozi wowote nje ya nchi.
Hebu wakuu mfikirieni huyu dada mana maisha yake hayapo salama .
Kwnza inabidi akaishi kituo cha polisi kama usalama wake uwe hai
 
Mwaka jana mtoto wa Aunt (wa kike) alienda pale 77 kwenye maonyesho alafu akapotea kwa siku 4 tulienda hadi polisi siku ya 4 kajirudisha home nikaitwa kutoa adhabu duh nilimfumua yule binti akagoma kusema ikabidi nimburuze mpaka shule maana walikua na taarifa duh acheni jamani walimu wa digitali mafundi jamani walimpa kisago kama jeshini nusu saa tu kataja hadi jina la basha ake wale walimu wakamuibukia dowezi pande za Temeke wakatoa kipondo kwa wote alafu wakawasogeza ubaoni kwa polisi ikabidi tukae pale Pile Bar tuchambe koo na walimu kupoza mwili mpaka mida mibovu kwa ujumla watoto wanafumuliwa sana tu uko mashuleni ila ndio bahati ya kuona hatupati kama hili la Mbeya day ila kama kuna walimu umu hawashangai maana wanawafumua sana tu watoto wetu na hii ni toka kitambo shikamoo mwalimu Victor popote ulipo bado nakumbuka visago vyako vya kinyang'au mpaka kundi lote likaacha bangi.
 
UPDATES: Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amewafukuza chuo walimu waliohusika na kumpiga mwanafunzi wa kidato cha 3, Mbeya Day Sec. School

Baada ya kusambaa kwa video inayowaonesha walimu takriban watano wakimpiga bila huruma mwanafunzi wa shule ya kutwa ya Mbeya, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amechukua hatua.
x14026642_245715935822573_429135586_n.jpg.pagespeed.ic.fjBouvdYDP.jpg

Kupitia Instagram, Mwigulu amesema kuwa polisi Mbeya wanaendelea kuuhoji uongozi wa shule hiyo.

Haya ni maelezo yake:

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile.

Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. MWIGULU Nchemba, W MNN

Kitendo hicho kimesababisha hasira kali kwa wananchi wanaotaka kuwepo adhabu kali kwa walimu hao.


Una maoni gani mwanajamii juu ya hili sakata la udhalilishaji?
 
Huu udhalilishaji hata miaka ya nyuma ulikuwepo tatizo whatsapp na mitandao mingine ya kijamii ilikuwa bado haija improve ili kusambaza taarifa kama hizi.
 
Mwanafunzi alitenda kosa kwa kutokamilisha zoezi la somo. Mwalimu alipaswa kumhoji kirafiki kabka ya kumhukumu. Huenda alikuwa na sababu ya msingi, mf. hakupata nafasi baada ya kurejea nyumbani.

Adhabu inayojenga ingemfaa sana mwanafunzi kuliko kuchapwa kofi na mwalimu. Unajua katika umri wa majimoto (adolescence period) ni aibu kijana kupigwa kofi mbele ya wanafunzi wenzake hususani jinsia tofauti.

Nafikiri mbadala wa adhabu ile ungekuwa kumsimamia huyo mwanafunzi afanye zoezi au kumuongezea maswali zaidi.
 
Ingekua mm uwiiii huyo mwalim ni wa kiume ila angezaa manina zake
 
Hawa ni walimu au ni [HASHTAG]#Teamscorpion[/HASHTAG].
 
Hiyo adhabu kwakweli ni nzito, ila hawa watoto jamani acheni tu, tunakutana na mengi sana, wazazi wenyewe washawashindwa, ni manunda yaliyokubuhu, alafu hayaogopi wala hawamuheshimu mtu.

Emagine we mzazi mwanao anakosea unamuhoji then anakutukana,utamfanya nini mtoto huyo??
Walimu nao ni binadamu jamani na wana nyongo.
Mwanafunzi alikuwa anaumwa na magoti halafu mwalimu anamwambia apige magotii ungekuwaww ungekubalii siokulaumu
 
Hawa vijana hawakujifunza saikolojia? walipaswa kuwaelewa vizuri wanafuzi wao tabia zao ili kuwaongoza vizuri
 
Mwanafunzi alitenda kosa kwa kutokamilisha zoezi la somo. Mwalimu alipaswa kumhoji kirafiki kabka ya kumhukumu. Huenda alikuwa na sababu ya msingi, mf. hakupata nafasi baada ya kurejea nyumbani.

Adhabu inayojenga ingemfaa sana mwanafunzi kuliko kuchapwa kofi na mwalimu. Unajua katika umri wa majimoto (adolescence period) ni aibu kijana kupigwa kofi mbele ya wanafunzi wenzake hususani jinsia tofauti.

Nafikiri mbadala wa adhabu ile ungekuwa kumsimamia huyo mwanafunzi afanye zoezi au kumuongezea maswali zaidi.
Asante, pia kuna disciplinary procedures za shule zipo na ukifuata huna cha kupoteza. Mwanafunzi atakukumbuka maisha yake yote na wewe utaitwa mwalimu mwenye hekima.
 
Khaa ni mwanafunzi huyo wanampiga namna hiyo. They are really muderers

Dah, hata mimi nashindwa kuamini kama ki;pigo hicho ni kutokana na mwanafunzi huyo kukataa adhabu aliyopewa...Waalimu wa aina hii nadhani wamepotea profession....hawa nadhani wanaweza hata kuvaa mabomu kiunoni na kulipua watu...yaani hawana huruma....ni sadists hawa....
 
Wabongo bwana! Mara hii wameshamsahau scorpion mtoboa macho wa buguruni.... Afu wanalilia justice kwa mwanafunz aliepigwa vijibao kadhaa na mwalimu. Wengi wetu tusingekuwepo hapa tulipo with white collar jobs bila kupata adhabu nzito kama hizo pindi tulipokuwa tukifanya upuuzi. Kazi nzuri walimu! (Ukinizingua nakutibua!!)
TANZANIA NI TAIFA LA WANAFIKI MKUU... MIMI NILIVYOPOKEA KICHAPO O LEVEL HAIELEZEKI... HUYU DENTI KWANZA MLA BANGI TU.

UNAANZAJE MKWIDA TICHA. I COULD NEVER HANDLE IT.
 
Duuu pole sana kijana Mwenyezi akujalie nafuu mapema But nna mashaka na malezi ya hawa walimu binadamu aliyelelewa kwa upendo hawezi fanya haya
 
Sometimes wanafunzi nao wawe wanaangalia na nyakati wanapotaka kufanya ujeuri, walimu wenyewe masela, unajua fika wapo field na edge mnalingana unaleta ujinga. Bora sie tulifundishwa na watu wazima, akina teacher Mwakalinde kila Siku alikuwa anatuonya kwa maneno sana, lkn leo hii hawa walimu wa mwendokasi hawana muda wa kukupa semina. anataka akupe mistari faster then nae hawahi uswazi kubet
 
Back
Top Bottom