Kwa malalamiko ninayoyasikia kutoka kwa huyo dada,ni wazi huyo kijana hakustahili adhabu hiyo,labda kutokana na umri,hata kama hakuwa mwanafunzi wa hapo.
Wabongo tujifunze kufuata sheria.Kama ni kijana wa mtaani si wangempeleka Polisi?Na kama ni mwanafunzi kwanini wampige hivyo?Ukatili wa aina hii haumjengi kijana mdogo kama huyo,unambomoa.
Mwisho,ninashauri ungeanzishwa utaratibu masuala ya adhabu na kesi za wanafunzi mashuleni wangechaguliwa waalimu maalum kudeal nayo na kigezo kikubwa cha kuwachagua waalimu hao iwe ni umri,above 35.Najua siku hizi waalimu wa umri huo ni wachache,hii iwe changamoto kwa serikali kujiuliza ni kwa nini watu wa umri huo hawavutiki sana kuendelea na kazi ya ualimu but what I see ni kwamba mambo ya ajabu mashuleni yanazidi kuongezeka kwa kadri umri wa waalimu unavyozidi kuwa mdogo.
Mtoto halelewi na mtoto mwenzie,kijana halelewi na kijana mwenzie.Tutafute namna ya kuwapata hawa walimu seniors wawepo baadhi kila shule kuwasimamia hawa watoto wetu wanaofundisha watoto wenzao.