MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Walimu wengi wenye maadili ni wale waliosoma vyuo vya certificate na diploma vya serikali kama Mpwapwa, Kigurunyembe nk. Katika ngazi ya degree walimu wanafundishwa madili kama lecture tu za masomo mengine ndo maana tunakua na walimu wa ajabu sana. Vyuo vya serikali vya dip tokea unaingia chuo wimbo mkuu ni Haiba, nidhamu mbele unanyooshwa hasa. unaenda field unapewa elf 13 maharage, mchele unga na sukari na unakata mwezi mzima tena field ya bush. Kijana aliyemaliza form 6 anaweza kua na miaka 21 mpaka 22, bado ana uchekibob wa ki teenager, anakwenda kusoma degree UDOM au UDSM ambapo ruksa kuingia darasani hata ukiwa umelewa, anaenda club, ana boom nk. Anamaliza chuo akiwa na miaka 25 unakwenda kumkabidhi malezi ya wanafunzi wetu kama wale wa Jangwani anakutana na mabinti wa form 2 mpaka four wapo kwenye adolescent Stage. anakutana na vijana wa kiume nao wapo katika umri huo. Yaani hapo ni majanga juu ya majanga
 
Walichokifanya ni sahihi maana kuna wanafunzi jeur na wakat mwingine hutaka kupigana na walim
Acha ujinga... Akili zako hazipo vizuri kwakweli we unadhani hata kama mwanafunzi alitaka kupigana na mwanafunzi hiyo ndio njia sahihi ya kuzuia?...

Yani shule za private kwani hakuna mwanafunzi wa aina hiyo.. Kama wapo huwa wanafanyiwa hivyo... Mkuu utakua hujasoma kayumba yani hilo tukio ni mfano tu yapo matukio mengi lakini hajafanikiea Ku rekodiwa like that.... So ilo liwe fundisho kwakweli.. Big up to you Ndalichako,


Apart from everything kuna walimu wazuri sana na wanamoyo mzuri sana hao hueshimika kwa wanafunzi bila shurti.
 
nimeshajibu hilo swali
Kama ni hapo ulipoandika wakatuvua na kuanza kutuchapa, sidhani kama umejibu. Sababu uliyotoa ya hao walimu kuwachapa ni kutovaa chupi, sasa walijuaje kwamba hamjavaa hadi wakaamua kuwavua nguo na kuwachapa mkiwa uchi?
 
Wadau,

Clip hii sijui ni shule gani lakini yaonekana ni hapa nchini kutokana na sauti ya dada inayosikika kwenye background.

Hata kama huyo kijana amekosa vipi si angepelekwa vyombo vya sheria?

Wana tofauti gani na wale wanakijiji walioua watafiti?

Sheria ifuate mkondo wake, inaumiza sana.

=======

UPDATE:

Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.

Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.

Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.

Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.

========

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.


Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video.

Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.

MWIGULU Nchemba, W MNN




MKUU WA MKOA WA MBEYA AZUNGUMZIA TUKIO HILO



​

Taarifa ya awali ya tukio la kupigwa mwanafunzi wa Mbeya Day ndg Sebastian Chingulu.

Tukio lilianza tarehe 26/9/2016 mwalimu Frank Msigwa mwanafunzi kwa vitendo toka chuo kikuu cha Dar Es salaam kutoa assignment ya soma la kingereza kwa wanafunzi wa kidate cha Tatu.

Baada ya kusahihisha aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya NA tarehe 28/9/2016 alikwenda darasani NA kutoa adhabu NA alianza kwa kuwapa adhabu ya push up, kupiga magoti NA baadae viboko 2 katika utekelezaji mwanafunzi Sebastian Chingulu alikataa kufanya kutokana NA kuumwa NA goti.

Baada ya kukataa adhabu mwl Frank Msigwa NA wenzake 2 John Deo NA sanke Gwamaka walimpeleka ofisini NA kuanza kumshambulia kwa kipigo NA baada ya tukio hilo walitoeka na wakati wanamshambulia mwalimu mwingine aliwasihi wasimpige NA alirekodi tukio hilo.

Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu NA mwalimu mkuu kwa mahojiano, kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu NA mwanafunzi aliyepigwa.

Nawahakikishia serikali itawasaka popote walipo walimu hawa waliofanya tukio hili NA kufikishwa ktk vyombo vya dola NA sheria.

Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa NA matibabu.

Hii Ni taarifa ya awali nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua.

Amos G Makalla
RC Mbeya

======

Walimu waliohusika wafukuzwa Chuo, kwa habari zaidi soma=>Waziri Ndalichako awatimua Chuo walimu wa Mafunzo waliompiga mwanafunzi shule ya Kutwa Mbeya

Hilo ni moja tu ya matukio ya walimu kupambana na wanafunzi ili kupunguza stress zao za maisha, matukio yote yangerekodiwa yote yangezua kizaazaa.
 
That is beyond humanity especially for someone put under ur supervision. Bora wameondoka mapema maana wangehitinu halafu ndio wako kikazi officially Inge kuwaje????? Jeeee?? Mzazi pole mama loooo uchungu jmn. Uuuwwwwiiiiii. Huyo mkuu wa shule tena mwanamke ukakaa kimya tu jmn??? Ohh my God tuhurumie. Kumbe kusoma kote huko ustaarabu wa paka kuketia mkia? Wanatofauti gani na wagogo wale w kijijini walioua researchers???? Nineumia vby sana. Pole kijana. Msamehe bure Mungu atakufungulia milango mtakutana akiwa choka mby halafu mpakize kwenye ndinga yako na hela ya mataptap pia umgee
 
Napita tu!!! Ila kama Serikali inafanya kaz kwa kutafta kick namna hii bsi tumekwishey!!!!!!
 
Kuna siku mtoto kaja shule saa3, kachelewa alafu hana hata wasiwasi, mwl akamuita akamuuliza kwann aje shule muda ule, akamjibu mwl, 'ticha fuata yako' mwl akamuuliza unasemaje? Akamjibu 'we mngese ukinigusa tu nakupasua' aisee walimu wote tukajikuta tumetaharuki, mwl akataka kumrukia akawahiwa na kushikwa.

Haya mambo nyie acheni tu.
 
Mbona hamsemi huyo mwanafunzi kumkaba koo mwalimu/mlezi wake. Endeleeni ni kulea tabia za Akina SCORPION mnasubir akue na tabia hizo mmtie kiberiti mtaani ndio mfurahie? Mwalimu wa Iringa Aliyerekodi wenzake hana maadili ya kazi. Pia naona shida kwa wanafunzi wa Iringa University kupata maeneo ya kufanya field.
 
umesahau kuwa kwa mazingira yalivyo kwenye ile
video ni wazi kuwa aliyerekodi
angefahamika tu iwe isiwe. Na ni
jambo ambalo halikwepeki. Binafsi
nilifikiria hilo lakini nikaona
wahusika wanajua tu kuwa walikua wanarekodiwa na mtu
fulani. Hilo la kwanza. La pili ni kwamba, huyo aliyekuwa
anarekodi naye anahusika na
tuhuma za tukio zima.
Ameshindwa kuchukua hatua za
kumsaidia mwanafunzi asipigwe
zaidi tu ya kusema kwa mdomo huku akiendelea kurekodi. Tafsiri
ni kwamba, dhamira yake haikua
inamaanisha alichokua anasema.
Alitamani lile tukio liendelee au
aliona linafaa au mwanafunzi
alistahili kilichomkuta. Chukulia mfano huyu mwanafunzi angefariki
kutokana na kupigwa kule,
ungemteteaje? Hivyo ni sahihi kabisa kusema na
yeye ni mtuhumiwa. Ni kumpa
namba tu kulingana na uhusika
wake kwenye tukio zima


Mkuu social media imekaa kichwani kwa watu sana skuizi.
Juzi kuna mtu kapigwa maeneo ya manzese kidogo afe.
Mtu kapata ajali baada ya kutoa msaada aanaanza kutoa kasim anapiga picha asee watu walimkunguta kisawasawa naamini umbea umbea saivi kauweka kando *****
 
Sometimes wanafunzi nao wawe wanaangalia na nyakati wanapotaka kufanya ujeuri, walimu wenyewe masela, unajua fika wapo field na edge mnalingana unaleta ujinga. Bora sie tulifundishwa na watu wazima, akina teacher Mwakalinde kila Siku alikuwa anatuonya kwa maneno sana, lkn leo hii hawa walimu wa mwendokasi hawana muda wa kukupa semina. anataka akupe mistari faster then nae hawahi uswazi kubet

Walimu watakaonipigia mwanangu hivi wahakiki kua wamemfanya asinisimulie kilichotokea kwa maana kesi itabadilika kua ya mauaji [emoji57]

(Cut off there tongues and put them in glass jar, chop off there heads mail them to there moms and put some roses with my home address (I ain't f**king waiting for long court hours to influence justice)
 
Mkuu social media imekaa kichwani kwa watu sana skuizi.
Juzi kuna mtu kapigwa maeneo ya manzese kidogo afe.
Mtu kapata ajali baada ya kutoa msaada aanaanza kutoa kasim anapiga picha asee watu walimkunguta kisawasawa naamini umbea umbea saivi kauweka kando *****
watu wanafikiria vya kupost mitandaoni tuu badala ya mambo ya msingi
 
ariyerekodi ni sawa tuu na yule anayerekodi magaidi wakichinja watu
 
Tumefurahi kwa hatua zilizochukuliwa na waheshimiwa mawaziri wetu,wananchi tunaomba hatua kali za kisheria,zichukuwe mkondo wake.
Hawa waalimu ni wauwaji,kipigo cha vipi,kumpiga kijana mdogo kama yule.Tumeumia sana,na tunasikitika sana.
Yaonyesha kuna matukio mengi unyanyasaji kwa waafunzi na watoto,kupitia kwa baadhi ya waalimu mashuleni.
 
Mwalimu wa wapi ww.shule gani afu f4 ulipata maths na physics alama zipi ww.
Ukifaulu maths na phy ndo huchapi au,achen ushamba,mtoto hata hakuumia chochote lakin maneno yamekuwa meng yasiyokuwa na maana
 
Kwa kweli kazi ipo,
Waalimu wana makosa sana huwezi kumpiga mtoto namna hiyo, lakini nao wanafunzi wa siku hizi jamani!!

Wazazi muanze kushirikiana na Waalimu kwenye maendeleo ya watoto wenu, sio mzigo wote mnawaachia wao hlf yakitokea kama haya ndio mnakua mstari wa mbele.
 
Tumefurahi kwa hatua zilizochukuliwa na waheshimiwa mawaziri wetu,wananchi tunaomba hatua kali za kisheria,zichukuwe mkondo wake.
Hawa waalimu ni wauwaji,kipigo cha vipi,kumpiga kijana mdogo kama yule.Tumeumia sana,na tunasikitika sana.
Yaonyesha kuna matukio mengi unyanyasaji kwa waafunzi na watoto,kupitia kwa baadhi ya waalimu mashuleni.

Huyo mtoto badae anaweza akawa jasusi au jangiri kabisa kutokana na vitendo vya ki fvcken hivi
 
Utajiskiaje kama huyu ni mwanao na wewe ndio mzazi unakuta wanamtendea huu ukatili..!?

KAMA NYUMBANI HANISUMBUI NITAKUA UOANDE WAKE ILA KAMA NYUMBANI HANA NIDHAMU SINA LAMKUSEMA ZAIDI YA KUOMBA WAREWIND
 
Kuna siku mtoto kaja shule saa3, kachelewa alafu hana hata wasiwasi, mwl akamuita akamuuliza kwann aje shule muda ule, akamjibu mwl, 'ticha fuata yako' mwl akamuuliza unasemaje? Akamjibu 'we mngese ukinigusa tu nakupasua' aisee walimu wote tukajikuta tumetaharuki, mwl akataka kumrukia akawahiwa na kushikwa.

Haya mambo nyie acheni tu.
Hii story yako ni ya uwongo na nina uhakika 99% niuwongo! Go to hell to relax!

Watoto wanaomaliza miaka hii ni watoto wadogo sana hawana jeuri hiyo ya kujibu fucken answer kama unavyo taka kutuaminisha hapa!!

Usipende kujitungia story za uwongo na kuziweka public

Huyo dogo alikuwa na haki ya kujitetea na kujieleza!

Walimu mna stress hamjalazimishwa kufundisha zipo kazi nyingine za kufanya

Kwani mlitumwa mfeli??
 
Back
Top Bottom