Mbeya: Rais Samia azindua mpango wa ruzuku kukabiliana na bei ya mbolea kwa wakulima

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
3,135
2,471
Rais Samia Suluhu Hassani amezindua rasmi mpango wa ruzuku ili kukabiliana na bei ya mbolea nchini ambao baada ya ruzuku hiyo, mkulima atanunua kwa bei ya chini kama inavyoonekana ktk jedwali.✊🏿

Tangu aingie madarakani, Rais Samia amefanya jitihada kadhaa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inaleta tija kubwa nchini huku akishughulika zaidi ktk maeneo ya utafiti, pembejeo na kilimo cha umwagiliaji.

Kwa mujibu wa takwimu za kiuchumi; asilimia kubwa ya watanzania wanategemea sekta ya kilimo kujikwamua kiuchumi.
20220808_115349.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametuwezesha sana wakulima msimu huu wakulima tunaramba asali
 
Wakulima wanapaswa wasome vizuri utaratibu, wasije kuanza kutukana kama walimu walivyofanya kutokuelewa 23.3

Hizi bei sio kwamba ukienda tu dukani utakuta hivyo, hapana. Kuna utaratibu wa wakulima kusajiliwa kwenye mfumo na kupata hizo mbolea kwa bei hiyo.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametuwezesha sana wakulima msimu huu wakulima tunaramba asali
Kushukuru hadi utekelezaji ufanyike.

Vinginevyo waweza sema ahsante na ukaishia kunawa.

Maneno maneno na upigagi usiojali utu ndiyo maisha yetu tuliyonayo hivi sasa waTz.
 
Back
Top Bottom