ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,115
- 49,833
Wakulima mna bahati sana awamu hii ya Rais Samia maana anawapeti peti Kwa Kila Hali Ili mnyanyuke.Rais Samia ndio Malkia wa Sheba wa Kizazi hiki.
1. Ruzuku ya mbolea na pembejeo zingine
2. Kilimo ni biashara na uhakika wa soko
3. Visima vya umwagiliaji Kwa wakulima wadogo
4. Riba nafuu kwenye mabenki isiyozidi Asilimia 9%
5.Kafuta ushuru/import duty kwenye zana za Kilimo kama matrekta
6.Uhakika wa Masoko
7.Anajenga Scheme za Umwagiliaji
8. Anawajengea Cold facilities
9. Anagawa vifaa vya umwagiliaji Kwa njia ya matone
10. Mradi wa BBT Kwa Vijana
11. Amerejesha 8/8 na kuifanya ya Kimataifa ambapo Vitalu vya mafunzo vitajengwa kwenye Viwanja vilovyoteuliwa.
12. Ameanzisha mnada wa Chai Tanzania,hakuna Kupeleka Mombasa.
13. Ameongeza Bajeti ya Kilimo Hadi kufikia Bilioni 970 ,hii ni Historia Kwa Tanzania.
Hayo ni Baadhi tuu kati ya mengi ambayo yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwenye sekta ya Kilimo.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Mweli pamoja na Dkt. Hussein Mohammed Omar Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya maafisa ugani, trekta kwa wakulima, vifaa vya kutengeneza Vihenge vya chuma kwa Vijana, bei elekezi za mbolea ya ruzuku, mradi wa uchimbaji wa visima pamoja na ugawaji wa vifaa vya mfumo wa umwagiliaji kwa matone katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.
My Take
Kiufupi Mama amenishawishi nimeingia kwenye Kilimo baada ya kuki damp awamu ya 5,Sasa hivi Kila zao utakalolima ni hela.