Waziri Bashe kemea uhuni unaotaka kufanywa na TCJE, kuwanyima neema wakulima wanaolima kupitia vyama vya msingi mbolea ya ruzuku

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
10,146
21,477
Habari wakuu
Moja kwa moja kwenye mada
Bashe kupitia wizara yako ulituhaidi wakulima tunaolima kupitia vyama vya msingi kunufaika na mboleo ya ruzuku

Kweli mwaka huu tumepokea mbolea zilizo na vifungashio vyenye nembo ya ruzuku, tukakubali kwamba ahadi ya kumuinua mkulima kunufaika na ruzuku imetimia

Hizi siku mbili TCJE amekuwa akizitaka unioni (vyama vikuu vya upili ) kuwatoza vyama vya msingi bei ya mbolea isiyo na ruzuku kitu ambacho ni kinyume na makubaliano ya awali na ahadi ya serikali.

Tunakuomba mh. Bashe ulisemee hili na wakulima wa vyama vya msingi (hasa wakulima wa tumbaku) tutanufaika na mbolea ya ruzuku ama hapana

Maana TCJE amekuwa muhuni sana kwenye uagizaji wa pembejeo, analeta kwa kuchelewesha na bado anataka kuondoa ruzuku
 
Back
Top Bottom