Mbegu za Vitunguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbegu za Vitunguu

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by 1800, Dec 17, 2012.

 1. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wadau naomba kujuzwa juu ya upatikanaji wa mbegu za bora vitunguu mkoani Morogoro
   
 2. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 533
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Morogoro vitunguu bora vinapatikana kwenye maduka mengi sanaaa ya pembejeo mjini Morogoro. Hizo ni mbegu bora kwa vile ni officially certified. Mbegu hizi zinadosari kubwa mbili, kwanza huwa ghari sana kwa mtu anaetaka kulima eneo kubwa kibiashara mfano ekari moja na kwenda juu. Kwa hiyo gharama ya mbegu huwa kubwa ingawa kwa kweli huwa mara nyingi ni mbegu halisi! Tatizo la pili ni jinsi hali ya hewa ilivyoharibika Kitaifa kwamba kila biashara sasa kuna kitu-FEKI! Unanunua mbegu kwa bei mbaya inamhuri unaosomeka kabisa kuwa mbegu hiyo imekuwa packed January na wewe unainunua April unaisia inagoma kuota kabisa! Unahofia labda nimesia vibaya, unanunua nyingine tena matokeo yale yale haioti!

  Mfano iliwahi kunitokea mimi mwaka mmoja nilinunua mbegu ya Pilipili Hoho za kampuni maarufu ya Holand! Muhuri ulionyesha ni mbegu mpya kabisa ya hoho lakini haikuota!! Nimekuwa nikipata mbegu ya uhakika toka kampuni ya Mkulima Seeds hizo ndiyo zilikuwa zikiota, lakini tena tatizo likaja Mbegu za Mkulima seeds nazo ni mchanganyinko, hoho zingine zilikuwa ndefu sana na nyeupe (matunda)! Pia kuna Nyanya aina ya Tanya naijua vema tabia yake na tunda linavyokuwa, niliwahi kununua mbegu aina hiyo ya nyanya zinazozalishwa na East Africa Seed company zilipoanza kuiva ilikuwa ni uchafu tu hata wateja walisusia kununua! Ilikuwa ni mchanganyiko wa mbegu usioeleweka! Kwa ukweli usiamini mbegu yoyote eti mradi iko kwenye Kopo au pact yenye lebo nzuri ni wizi wizi tu! Mkakati wangu kwa hili ni kuzalisha mbegu mwenyewe watu hawaaminiki!

  Sehemu ya pili ya kupata mbegu Morogoro ni mbegu zinazozalishwa na wakulima. Morogoro kuna eneo maarufu kwa kilimo cha vitunguu linaitwa Lumuma, wilaya ya Kilosa huko kunawazalishaji wengi sana wa mbegu za vitunguu waliopata mafunzo rasmi ya uzalishaji bora wa mbegu za vitunguu. Mbegu za vitunguu toka kwa wakulima huuzwa kwa kupimwa kwa ujazo wa lita. Kutegemea mwaka lita huanzia sh 15,000/- hadi 30,000/- mwaka 2010 ilifikia bei ya lita moja 50,000/-! Mbegu huvunwa mwezi wa 10 huu ni muda mzuri kununua baada ya hapo bei hupanda juu. Mkulima anaetaka kulima eneo kubwa mbegu hii ndiyo inamfaa maana ni nafuu kuliko za kwenye makopo.

  Tatizo kubwa la mbegu za wakulima nalo ni ulaghai! Kwa kuitazama mbegu huwezi jua kama ni mbegu aina unayoitaka, wengi huwa wanadanganya ukijapanda baadae unabaki kulia kuwa umetapeliwa! Inabidi pia uwe unajua kuzipima kama zinaota au la, wenyeji wananjia mbalimbali wengine wanatumia maji wengine moto! Kitaalamu ni budi kuotesha sample kwanza kisha angalia uotaji wake kisha ukiridhika nunua kwa wingi kutoka kwa mkulima husika.

  Tatizo lingine kwenye mbegu za wakulima za vitunguu ni hili: kwa kawaida vitunguu vinatabia msimu wa kwanza havitakiwi vitoe mabomba ya maua bali vitoe vitunguu tu, msimu wa pili unapopandikiza kitunguu-mama ndiyo hutakiwa kitoe bomba, maua na hatimae mbegu. Sasa kwa wakulima laghai inapotokea kitunguu kikatoa mbegu isivyotarajiwa ule msimu wa kwanza huzivuna hizo mbegu na kuziuza! Ukinunua mbegu kama hizo matokeo yake ni kujikuta vitunguu asilimia kubwa shambani vimetoa mabomba ya maua! Na hii ni hasara kwani vitunguu vyako hukosa ubora sokoni yaani ni msiba kwako!

  Ili kuepuka hili unatakiwa uwahi kwa mkulima mzalishaji wa mbegu ukaone vitunguu vyake vikiwa bado shambani mwezi mmoja au miwili kabla hajavuna ili ujiridhishe kwamba ni aina halisi ya vitunguu unayotaka ili akivuna ununue kitu halisi. Vinginevyo tumia wakulima waaminifu ambao akikuambia ni red ni red kweli akisema khaki ni khaki kweli! Msimu wa mwisho nilimwamini kijana mmoja alikuwa akileta mbegu toka Singida, kumbe kule Singida alikuwa akizoa hizo mbegu nilizoeleza hapo juu, wanazoa zoa mashambani tu, matokeo yake nikaanza kuona vinajitokeza vitunguu vyeupe na vyekundu, baadae shamba zima lilichanua utadhani nimelima vitunguu vya mbegu!!

  Kuwa mwangalifu utakapokuwa unatafuta mbegu!

  Niwie radhi jamani maelezo yangu marefu saa zingine namimi nae mweeee!
   
 3. Madiba

  Madiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2013
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 330
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Kubota: Vipi kuhusu mbegu za maeneo ya Ruaha huko Iringa? Nina mpango wa kwenda kulima vitunguu huko
   
 4. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2013
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  kibota chukua like
   
 5. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 533
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Madiba kwa vile unaenda kulima huko huko Ruaha, ukifika huko ulizia wakulima wa mbegu mashuhuri. Nakuhakikishia utapata mbegu nzuri maana huko unakwenda jikoni kwenyewe. Fanya utafiti ili ujihakikishie kuwa atakayekuuzia ni mkulima wa mbegu mwenye jina na usijali hata kama anauza mbegu zake kwa bei kubwa kulinganisha na wengine, hiyo itakuwa ni shauri ya ubora, maana ubora unagharama zake. Nihivyo tu mkuu.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,356
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Hahaha Kubota umenichekesha. Kweli wewe kubota aisee. Big up.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Madiba

  Madiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2013
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 330
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nimekupata Kubota, ntafanya utafiti huo!!
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2013
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  mie natafuta mbegu ya vitunguu swaumu
   
 9. z

  zunya ishile Member

  #9
  Dec 28, 2013
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu Kubota,mimi ni graduate nina mpango wa kujikita kwa mara ya kwanza ktk kilimo cha vitunguu maji huko ruaha mbuyuni,nimeona changamoto nying hususan ktk masoko na hili la mbegu bora kiukwel umetoa darasa zuri..nitakapoanza nitaomba msaada wako zaid.shukran mkuu.
   
Loading...