Erick_Otieno

JF-Expert Member
Mar 28, 2010
624
1,020
Blue Greyscale Volleyball Stats UAAP_NCAA Twitter Post.png

Wakuu salamu,

Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!
Kilimo Kwanza!


BAADHI YA WADAU WANAOHITAJI KUELEWA KILIMO HIKI
Wadau,

Napenda kufanya kilimo cha vitunguu ila sina data za kutosha kuhusu hili swala. Nimesikia kuna sehemu inaitwa mang`ola wanalima ila sijawahi fika,sehemu nyingine ni Iringa ila sasa nashindwa kujua ni wapi kati ya sehemu hizo mbili nimzuri na cheap.

Then: ingependa kujua mashamba yanakodishwa shiling ngapi? Mbegu kwa heka ni sh ngapi? Gharama ya kulima pamoja na kuweka matuta? Kupanda? Mtu wakulinda shamba ni sh ngapi?na vitu vingine ambavyo sivijuwi.

Wadau haya yote yametokana na hali mbaya ya wategemeawo mwisho wa mwezi.naombeni mawazo yenu wadau.

Naomba kuwakilisha hoja.
Wandugu nimeamua kuingia kwenye kilimo,ninawaza kuanza na kitunguu saumu,..naomba mnijuze wapi panafaa kulima?gharama ya kutunza hekari 1,muda mpaka kukomaa, . Pili nafikia pia maharage ya kijivu(ya mbeya) detail zake pia,, asanteni.
Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo.napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1


MICHANGO YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI
KILIMO BORA CHA KILIMO CHA VITUNGUU MAJI
Hapo awali kitungu kilikuwa ni zao lililokuwa linapatikana porini katika ukanda wa bahari ya Mediterania. Zao hili hulimwa katika nchi nyingi za magharibi, nchi za milima zilipo kaskazini mwa dunia, likwemo bara la Afrika. Vitunguu hustawi katika hali ya hewa ya jotoridi 13°C – 24°C, hali ya hewa inayofaa kwa kuotesha na kukuzia miche kwenye kitalu ni jotoridi 20°C – 25°C. Kwa kawaida vitunguu huhitaji kiasi cha joto nyuzi 20°C-25°C ili kuweza kustawi na kukua vizuri. Joto zaidi ya hapo hufanya vitunguu kudumaa na kutoweza kutengeneza viazi (bulbs).


Matumizi
Kitunguu hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula, na pia hutumika kama dawa ya kansa ya tumbo, vidonda na majipu.

Ustawi
Zao la vitunguu hustawi katika udongo wa tifu tifu wenye mbolea ya kutosha, ukiwa na uchachu wa udongo (PH) kiasi cha 6 – 6.8. Udongo wa mfinyanzi haufai kwa zao la vitunguu kwa kuwa hauruhusu viazi vya vitunguu (bulbs) kutanuka. Hivyo uwezekano wa kupata mazao ni mdogo. Pia udongo wa kichanga haufai kwa zao la kitunguu kwa kuwa hauna mbolea na hivyo vitunguu huwa vidogo sana, jambo ambalo ni vigumu kupata mazao yanayofaa kwa soko.

Zao la kitunguu huhitaji unyevu muda wote wa ukuaji wake. Zao hili lina mizizi mifupi hivyo linahitaji kumwagiliwa maji mara kwa mara.




Aina za vitunguu

Kuna aina mbili za vitunguu ambazo zimezoeleka
:
  • Vitunguu vya asili kama vile Singida, na Rujewa (aina hii ina rangi ya kahawia iliyopauka).

  • Chotara: Hii ni aina ya vitunguu inayojulikana kama vitunguu vya kisasa. Katika kundi hili kuna vitunguu kama Texas grano, Red creole, Bombay red, White granex, na Super rex.
Mgawanyiko
Zao la vitunguu limegawanyika katika makundi mawili. Hii inatokana na uhitaji wa mwanga na ukuaji wake. Aina ya kwanza inahitaji mwanga kwa saa 8-13 ili kuweza kuchanua na kutoa mbegu.

Aina ya pili inahitaji mwanga kwa saa 13-15 kuweza kuchanua na kutoa mbegu.


Kupanda
Vitunguu hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo husiwa kwenye vitalu. Kitalu kinaweza kuwa na upana wa mita 1, urefu unategemeana na ukubwa wa eneo ulilo nalo.

Unaweza kupanda vitunguu kwenye matuta mbonyeo (Sunken bed). Aina hii ya upandaji hutumika kwenye eneo lenye shida ya maji. Upana wa tuta uwe mita moja.

Kupanda kwenye matuta mwinuko (Raised bed) upandaji wa iana hii hutu mika sehemu yenye maji mengi au yanayotuama.

Tahadhari: Maji yakituama kwenye vitunguu hufanya vitunguu kuoza, hivyo kuathiri mavuno.

Nafasi
Vitunguu vipandwe kwa nafasi ya sentimita 7.5 kutoka mche hadi mche, sentimita 12.5 kutoka mstari mmoja hadi mwingine kwenye matuta.



Mbole ya kupandia
Unaweza kutumia mboji, au samadi iliyo oza vizuri kupandia. Baada ya hapo unaweza kuongeza mboji baada ya miezi miwili. Endapo unafanya kilimo kisichozingatia misingi ya kilimo hai, unaweza kupanda kwa kutumia mbolea aina ya NPK (20:10:10) baada ya mwezi na nusu, unaweka mbolea ya Urea.

Palizi
Vitunguu ni zao lenye uwezo mdogo sana wa kushinda na magugu. Hivyo, inabidi shamba liwe safi muda wote wa ukuaji hadi kuvuna.



Uvunaji
Kwa kawaida, vitunguu huchukua muda wa miezi 5-6 tangu kupandwa hadi kuvunwa. Unaweza kuanza kuvuna vitunguu baada ya asilimia 75 ya shingo za vitunguu kuvunjika. Baada ya kuvuna, unaweza kuweka kwenye madaraja (grades) kwa kufuata ukubwa, rangi na unene wa shingo ya kitunguu. Vitunguu vyenye shingo nyembamba hudumu zaidi, vyenye shingo nene huoza haraka.

Ukataji
Hakikisha kuwa shingo ya kitunguu inabaki kiasi cha sentimita 2. Hii husaidia kuzuia kuoza haraka.

Namna ya kuhifadhi vitunguu
Baada ya kuvuna, hifadhi vitunguu kwenye kichanja chini ya kivuli na uvitandaze vizuri. Unaweza kuhifadhi vitunguu kwa kufunga kwenye mafungu na kuvitundika. Vitunguu vikihifadhiwa vizuri vinaweza kukaa hadi miezi minne bila kuharibika, hii hutegemeana na aina ya uhifadhi.

Wadudu wanaoshambulia vitunguu
Kuna aina nyingi za wadudu wanaoweza kushambulia vitunguu. Hawa wafuatao ni baadhi ya wadudu waliozoeleka kwenye zao la vitunguu.



Thiripi (Thrips): Wadudu hawa hukaa kwenye jani sehemu inayokutana na shina. Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani ya vitunguu na kusababisha majani kuwa na doti nyeupe.

Madhara: Husababisha vitunguu kudumaa hivyo kuathiri ukuaji wake jambo ambalo huathiri mavuno pia.



Kimamba: Wadudu hawa hufyonza maji kwenye vitunguu, na kusambaza ugonjwa wa virusi. Husababisha kudumaa kwa vitunguu. Wadudu hawa ni hatari zaidi kwa kuwa husambaza virusi vinavyoingia hadi kwenye mbegu.

Minyoo fundo (Nematodes): Aina hii ya minyoo hushambulia mizizi ya vitunguu. Hali hii husababisha kudumaa kwa vitunguu kwa kuwa hushindwa kufyonza maji na chakula kutoka ardhini.

Vidomozi (Leaf minor): Hushambulia majani kwa kujipenyeza kwenye ngozi ya jani na kusababisha michoro ambayo huathiri utendaji wa majani.

Utitiri mwekundu (Red spider mites): Wadudu hawa hufyonza maji kwenye majani na kusababisha vitunguu kunyauka.

Funza wakatao miche: Funza hawa hutokana na wadudu wajulikanao kama Nondo, na hushambulia shina na kulikata kabisa.

Namna ya kukabiliana na wadudu hawa
Unaweza kukabiliana na wadudu hawa kwa kufanya kilimo cha mzunguko. Usioteshe vitunguu sehemu moja kwa muda mrefu, au kufuatanisha mazao jamii ya vitunguu kama vile leaks.

Tumia mbegu bora zilizothibitishwa kutoka kwenye kampuni zinatambuliwa kisheria na kibiashara. Kupanda kwa wakati unaotakiwa; vitunguu visipandwe wakati wa kiangazi. Vipandwe wakati wa majira ya baridi na kuvunwa wakati wa joto. Tumia dawa za asili za kuulia wadudu, au dawa nyinginezo zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo.


Magonjwa yanayoshambulia vitunguu

1. Purple blotch: Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Ugonjwa huu husababisha mabaka ya zambarau na meusi katika majani ya vitunguu. Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu unyevu mwingi.
Madhara: Ugonjwa huu hupunguza mavuno mpaka asilimia hamsini (50%).

2. Stemphylium leaf blight: Hukausha majani kuanzia kwenye ncha hadio kwenye shina.; Ugonjwa huu hutokea wakati wa unyevu na ukungu mwingi.
Madhara: Hupunguza mavuno hadi kwa asilimia sabini na tano (75%).

3. Magonjwa ya virusi (Onion yellow draft virus): Ugonjwa huu husababisha vitunguu kuwa na rangi iliyochanganyika, kijani na michirizi myeupe au njano. Vitunguu hudumaa kwa kiasi kikubwa;Ugonjwa huu husababishwa na kimamba.

Madhara: Huathiri mavuno kwa asilimia 80 mpaka asilimia 100%.

4. Kuoza kwa kiazi (Bulb rot): Husababishwa na fangasi. Ugonjwa huu hutokea vitunguu vikishakomaa, huku udongo ukiwa na maji maji. Vitunguu vikishakomaa visimwagiliwe tena.

Uharibifu wa vitunguu usiotokana na magonjwa
1. Kuchipua baada ya kuvunwa: Hali hii hutokea endapo vitunguu vitavunwa kabla ya muda wake. Endapo vitunguu havitakaushwa vizuri baada ya kuvunwa. Hali hii husababisha uharibifu mpaka asilimia themanini (80%). Sehemu ya kukaushia vitunguu iwe na hewa inayozunguka na mwanga wa kutosha. Vitunguu vikiwekwa gizani huchipua kwa urahisi.

2. Muozo laini (Soft rot): Ugonjwa huu hushambulia vitunguu baada ya kukomaa; husababishwa na vimelea (bacteria). Vitunguu hutoa harufu mbaya ya uozo. Kuepuka hilo vuna kwa wakati unaofaa, hifadhi sehemu yenye mwanga na hewa inayozunguka.



Virusi
Unaweza kuzuia vimamba ambao ndio wanaoeneza virusi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu.

Vitunguu vinalipa
“Vitunguu vinatofauti kidogo na mazao mengine ya mboga mboga kwa kuwa si rahisi kukosa soko, na endapo bei si nzuri unaweza kuhifadhi kwa muda ili kusubiri bei iwe nzuri.” Ni maneno ya mkulima Peniel Rodrick (pichani) ambaye amejikita zaidi katika kilimo cha vitunguu kibiashara.

Mkulima huyu kutoka kijiji cha Oloigeruno anasema pamoja na kwamba anazalisha pia mazao mengine, lakini ameamua kujikita zaidi kwenye vitunguu baada ya kugundua siri na namna ya kupata faida zaidi.

Toka aanze kilimo cha vitunguu miaka 12 iliyopita, ameweza kuendesha maisha yake vizuri, ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mingine kama ufugaji wa ng’ombe, kujenga nyumba ya kisasa na kuitunza familia yake ya watoto watatu ipasavyo. Pamoja na hayo anasema tatizo kubwa la vitunguu ni magonjwa na wadudu. Anasema si rahisi sana kugundua mara moja kuwa kuna ugonjwa unaoshambulia vitunguu, na mara unapogundua unakuwa umefikia kwenye hali mbaya.
KILIMO BORA CHA VITUNGUU SAUMU

UTANGULIZI
Vitunguu saumu ni jamii ya vitunguu maji asili yake ni nchi za Asia lakin pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA YA VITUNGUU SAUMU
Kitaalam bado aijafahamika kunaaina ngapi za vitunguu saumu lakini kuna aina mbili ambazo zinalimwa hapa nchini ni Kienyeji na kisasa.
Aina ya kisasa uzaa vitunguu vikubwa venye ngozi nyeupe napia aina ya kienyeji uzaa vitunguu vyekundu vyenye harufu kali sana na pia havia haribiki mapema ukilinganisha na vya kisasa vitunguu saumu havizai mbegu halisi kwa hyo uzalishwa kwa kutumia vikonyo vyake



TABIA YA MMEA

Tunguu la vitunguu saumu utokana na vikonyo na hiv vikonyo ndo vinatumika kama mbegu

HALI YA HEWA
Vitunguu saumu ulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

KUANDAA SHAMBA
Andaa shamba mapema lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutuengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda au wakati wa kupanda pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta

KUPANDA
Panda vikonyo vilivo anza kuchipua vilivo safi na visivyo na dalili ya ugonjwa kwa nafasi ya sm 5 kikonyo hadi kikonyo na sm 15 mstari hadi mstari.

PALIZI NA MATUMIZI YA MBOLEA
Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza weka mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi.

MAGONJWA
  • fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna
  • kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia
  • kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi
  • baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao
  • muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa
WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

KUVUNA
Vitunguu uvunwa vikifika miezi 6-7 baada ya kupanda majani na mashina unyesha dalii ya kukauka viache vitunguu shambani mpaka majani yanap kauka kabisa ngoa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu
ABC's ZA KILIMO CHA VITUNGUU
UTANGULIZI
Vitunguu saumu ni zao ambalo lipo katika jamii ya vitunguu na hufanana sana na vitunguu maji, zao hili linatumika sana duniani kama kiungo cha chakula na wengine hutumia kama dawa.

ASILI YAKE
Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na China, Asia lakini pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA ZA VITUNGUU SWAUMU
Vitunguu swaumu vipo vya aina mbalimbali nazo ni:=

i) Antichoke – Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea

ii) Soft neck – Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani

iii) Silver skin – Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

HALI YA HEWA & UDONGO
Vitunguu saumu hulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba linapaswa kutayarishwa mapema kabisa, lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda.

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Mbegu ya kitunguu swaumu ni ile punje (vikonyo) inayokuwa imebanguliwa kutoka kwenye kitunguu au tunguu iliyokomaa kabisa, kiasi cha kilo 300 – 500 hutumika kwa hekari moja na inatakiwa uchague mbegu isio na magonjwa au isio dhaifu.

UPANDAJI
Tabia ya mmea wa Vitunguu swaumu humea huanza kuota kipindi cha baridi ( miezi yenye baridi), kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August, Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 .
Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.

MBOLEA
Mbolea huwekwa baada ya palizi, tumia mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi.

UPALILIAJI
Kuwa na juhudi ya kupalilia ili kuipa uhuru mimea kumea vizuri na kulifanya shamba lako kuwa safi, Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza ndipo weka mbolea.

Unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi. Mmea unapoendelea kukua na kutoa maua yaache majani yarefuke mpaka yajikunje, ndipo utayakata ili kuongeza uzalishaji.

MAGONJWA & WADUDU
MAGONJWA

Vitunguu swaumu havishambuliwi sana na magonjo, ila magongwa yake ni kama:=

i) Fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna

ii) Kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia

iii) Kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi

iv) Baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao

v) Muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa.

WADUDU
Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

UVUNAJI
Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja.

SOKO
Soko lipo kwasababu Vitunguu Swaumu ni kiungo kinacho tumika na wengi, kwa bei ya shiling 3,000 – 3800 kwa kilo.
GHARAMA ZA KULIMA KITUNGUU KILOSA
Kwa Milioni moja?
Inategemea unalimia wapi?
Inategemea umwagiliaji kwa pampu au mifereji au mvua

Uzoefu wangu huku Kilosa huu:
Mbegu lita 7 kwa ekari @ 25,000/= jumla 175,000/=
Kuandaa kitalu 20,000/=
Kusia mbegu 10,000/=
kutunza kitalu 30,000/=
kukodi shamba 100,000/=
kufyeka shamba 48,000/=
kukatua udongo 64,000/=
kulainisha udongo 48,000/=
kutengeneza majaruba 25,000/=
kupandikiza 160,000/=
dawa ya kuua magugu 40,000/=
palizi mara mbili 100,000/=
Mbolea mifuko mitatu 210,000/=
Mtu wa kuweka mbolea mara mbili 10,000/=
madawa kuua wadudu na magonjwa 50,000/=
mpiga dawa wiki kumi 50,000/=
kung'oa 50,000/=
kukata vitunguu gunia mia 200,000/=
usafiri 100,000/=
chanja kukodi 100,0000
umwagiliaji petrol 2500 x lita 5 x wiki 10 = 125,000/=
mtu wa kumwagilia 5000 x wiki 10 = 50,000
JUMLA KUU = 1,855,000/=

Kwa wastani ni mil 2
GHARAMA ZA KULIMA KITUNGUU MBEYA
Mbeya
Kukod shamba 50000
Mbegu gram 400-500
Gram 100-25000
Kulima 50000
Vitalu kwa ajur ya kupanda 50000
Kupanda 100000
Dawa ya palizi 40000
Paluz 3
Mbolea 150000
Madawa tote 150000
Kuvuna 100000
Hapo unaweza kuvuna gunia had 90 hakuna migogoro ya maji yapo kubao unwagiria SAA yeyote ukitaka coll me 0759185832
KITUNGUU NI ZAO LENYE MANUFAA
Habari ndugu zangu,

Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.

Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.

Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.

Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.

Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com

Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.
UHUDUMIAJI WA KITUNGUU
Kwa kilimanjaro.

Kwanza mbegu kwa eka utatakiwa kusia kilo tatu mpaka nne. Ukinunua mbegu dukani hiyo ni 400,000
Kuandaa kitalu, kusia na kutunza mbegu kwa angalau mwezi mmoja na nusu lazima uwe na angalau 300,000
Kupandikiza ekari moja yenye majaruba yasiyopungua 330= 330,000
Utatakiwa ukishapandikiza uwe na mifuko angalau 12 ya mbolea kila mwezi utatia mbolea (yaani mifuko minne kwa eka) 45,000x12.

Utatakiwa kupiga dawa kila wiki ya kuua wadudu, buster, ya kuondoa baridi etc..dawa pekee itakugharimu si chini ya 80,000 kwa ekari moja kila wiki. Utatakliwa either kupiga dawa ya kuua mbegu za magugu yasiote ambayo ni tsh 17,000-27/ lita kwa ekar unaweza kuhitaji lita mbili. au kungolea majani angalau mara nne tangu kupandikiza mpaka kuvuna.

Kwa eka kila wiki utahitaji kumwagilia. Kwa ekari moja angalau uwe na lita 30 za dizeli/petroli kama pumb unayo.

NB: Omba Mungu utakapovuna Mang'ora au Ngage usiwe msimu wa kuvuna vitunguu maana utapata pressure. wengi wamepata hasara kubwa na wengine wamepoteza maisha. Bei kwa sasa kwa gunia la vitunguu haizidi elfu 60,000. Mimi binafsi nimelima na nimepata hasara isiyo kifani.

Kwa ekar kuanzia kusia mpaka kuvuna angalau uwe na tsh 3mil - 4mil. Lakini usitengee kuwa utavuna upate faida kama story zilivyo. Kama unapesa hivyo nakushauri uiwekeze kwa mambo mengine. Mzunguko wa pesa kwa sasa hakuna. Kitunguu hakilipi kwa sababu kinalimwa kila mahali Tanzania kwa sasa. Weka pesa zako hata fixed deposit.

Nazungumza kutokana na uzoefu. Nitumia zaidi ya mil13 kulima. Nilipovuna nikauza kila gunia kwa 40,000 nikapata hasara zaidi ya milion 10. Usisikie story. The truth is terrifying. Na usije ukachukua mkopo ukitegemea kilimo cha kitunguu kitakulipa.

Kabla benki hawajakufikia utakuwa umeshakufa kwa pressure. Nenda ngage, kileo, chekereni, mawala, na sehemu zingine za mkoa wa kilimanjaro utapata story za watu waliokufa kwa pressure mwaka huu kutokana na vitunguu kushuka bei na kutofikia hata gharama za uzalishaji.

unaweza kuja inbox kwa maelezo zaidi. lakini kwa sasa kilimo cha vitunguu is not ideal
 
Realtor,'

Kuna sehemu fulani inaitwa ruaha mbuyuni, hapo bwana kilimo hakitegemei mvua, kitunguu kinakubali sana hapo mpendwa, vilevile uzuri wa hapo ni kwamba unawezakulima vitunguu marambili kwa mwaka, ukitoa kitunguu unaweza kulima mahindi mara mbili na maharage mwaka huo huo mmoja. Yaani ardhi ya hapo inakubali karibu kila kitu na serikali imeshapaendeleza.

Ukiweza kupapata hapo utafaidika sana lkn bei sio zile za elfu 50 kwa hekari, bei hapo ni kubwa na ni vigumu kidogo kupata eneo maana tayari mabebari tumeshayakamata (kidding).

Ni-PM kama unataka maelezo ya zaidi naweza kukusaidia.
 
Last edited by a moderator:
cheusimangala

Seconded.

Kijiji kinaitwa msosa to be precise. ni tarafa ya mahenge i think Wilaya ya Kilolo. Au ukiwa unatokea Dar kwenda Iringa opposite aljazeera hotel on your left. Kuna mifereji kabisa ya umwagiliaji. Nilikuwa huko last month, it's terrific, we nenda utapata mashamba ya kukodi and it pays.

Good luck.
 
Last edited by a moderator:
Shukrani Cheusimangala...Hawa mabebari:smile-big: tutabanana nao!

Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema!

Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda, ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),

Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu,watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.

Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
 
Pia jatribu kwenda mkoa wa pwani. Ukivuka daraja la mto ruvu mbele kama 1 kilomita (nadhani zamani palikuwepo na ranch ya napco) pinda kulia - nenda kama kilometere kumi hivi/pia ulizia wakazi utakutana na wanakijiji amabao watakuelekeza wapi hasa pana mashamba ya kukodi au kununua. ila chunga matapeli.

Kila la kheri.
 
Pia jatribu kwenda mkoa wa pwani. Ukivuka daraja la mto ruvu mbele kama 1 kilomita (nadhani zamani palikuwepo na ranch ya napco) pinda kulia - nenda kama kilometere kumi hivi/pia ulizia wakazi utakutana na wanakijiji amabao watakuelekeza wapi hasa pana mashamba ya kukodi au kununua. ila chunga matapeli. kila la kheri

Well said bro (hapo pekundu)

Maeneo hayo ni hatari, kama hela zako ni za kuungaunga, yaani kama unanunua eneo kisha upate muda mwingine wa kutafuta uwezo wa kuliendeleza, utaishia kulia. Ruvu kwa sasa inatakiwa uwe na uwezo, unanunua na kuendeleza eneo lako mara moja.

Ila usiogope, ni ushauri tu.
 
Pia jatribu kwenda mkoa wa pwani. Ukivuka daraja la mto ruvu mbele kama 1 kilomita (nadhani zamani palikuwepo na ranch ya napco) pinda kulia - nenda kama kilometere kumi hivi/pia ulizia wakazi utakutana na wanakijiji amabao watakuelekeza wapi hasa pana mashamba ya kukodi au kununua. ila chunga matapeli. kila la kheri
Hii ya matapeli ni tatizo kubwa sana kwenye kununua ardhi. Nilishawahi kuuziwa heka 8 na serikali ya kijiji pale mlandizi ukienda ndani karibu na reli ya kati, baadae likawa na kesi kati ya vijiji viwili wanaligombania. Nashindwa kuelewa ni namna gani tunaweza kuudhibiti huu utapeli.
 
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema !!!!!!!

Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola)...

Malila unaweza kunipa mwanga kidogo kuhusu bei za hayo maeneo ya Ruaha na hayo mengine kama unafahamu. Nataka nikasurvey na angalau kabla sijaenda huko nijue bei ya kununua kwa eka au ya kukodi kwa eka.

Kilimo Kwanza!
 
Malila unaweza kunipa mwanga kidogo kuhusu bei za hayo maeneo ya Ruaha na hayo mengine kama unafahamu. Nataka nikasurvey na angalau kabla sijaenda huko nijue bei ya kununua kwa eka au ya kukodi kwa eka.

Kilimo Kwanza!

Kwa maeneo hayo sijapata kutafiti bei zikoje,ila naona dada Cheusi anaweza kukusaidia kupata bei hizo kwa maeneo yale. Mimi nitapita maeneo ya Ruaha,nitajaribu kuuliza bei zikoje.
 
Malila hongera kaka kwa juhudi zako Mungu atakusaidia ndugu yangu nakuombea lakheri nimekukubali nimtaftaji hakuna sehem usoijua na malezoyako niuwazi bilashaka mtuasipo kuelewa atkua namatatizo naham yakukuona hoja zako zimenipa faraja na kujiamini, nisikupendele sana kuna wengi manyusi, cheusimangala, Dick, nawshukuru sana nifaidika sana na ushauri wenu bila ya ninyi kujua mungu awalinde kwa afianjema muiwezeshe jamii.

Malila naomba mualiko katika vikao vyenu mkuu.

Mbarikiwe sana
 
Mkuu Malila naomba na mini nisiwe mchoyo wa kutoa shukrani zangu!

Kwa kweli nimekuwa nafurahia sana mchango wako na umekuwa muwazi sana, na hivi ndo wajasiriamali wa Tanzania tunatakiwa tuwe! big up saaaanaaaaa!
 
Last edited by a moderator:
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom