Mbarali: Ng'ombe zaidi ya 400 ambao ni mali ya Wananchi kupigwa mnada leo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,420
Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kwamba ng'ombe hao wa wananchi wa Mbarali ambao idadi kamili ni 433, wanaodaiwa kukamatwa na Askari wa Wanyamapori kwenye hifadhi wanapigwa mnada leo 14/11/2022

Bali kampuni iliyopewa tenda ya kupiga mnada ng'ombe hao wa Wananchi inaitwa MBARALI HIGHLAND AUCTION MART LTD, Inayomilikiwa na Mbunge wa zamani wa CCM aliyetajwa kwa jina moja la Haroon , ambaye pia ndiye aliyeuziwa Mashamba ya Wananchi hao kwenye utawala wa awamu ya 4, yaani mtu aliyepora mashamba ya wananchi ndiye aliyepewa tenda ya kuuza mifugo yao.

Lakini Kanuni ya Mungu ile ya KILA UBAYA UTALIPWA ingali bado inafanya kazi.

Mungu wabariki wananchi wa Mbarali .

==
LEO, ng’ombe 433 waliokamatwa katika eneo la ardhi oevu ya Bonde la Ihefu, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wilayani Mbarali wanatazamiwa kupigwa mnada mkoani Mbeya.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kufanya oparesheni ili kuondoa zaidi ya mifugo 200,000 iliyovamia eneo hilo.

Mbali na kuhatarisha ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mifugo inahatarisha pia Mto Ruaha Mkuu.

Akitoa taarifa ya uvamizi wa bonde hilo la Ihefu, Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Godwell Ole Meng’ataki anasema katika kipindi cha miaka miwili wamekamata mifugo 12,758 katika hifadhi hiyo.

Anasema licha ya kuwatoza faini wafugaji kiasi cha kukusanya zaidi ya Sh bilioni 1.2 katika kipindi hicho, wafugaji wameendelea kurejesha mifugo ndani ya hifadhi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune anasema eneo lililotengwa kwa ajili ya mifugo katika wilaya hiyo linatosheleza mifugo isiyozidi 60,000, lakini wilaya hiyo ina mifugo zaidi ya 200,000.

Tatizo la mifugo kuvamia maeneo ya misitu haliko Ihefu pekee bali pia maeneo mengi, hasa katika mkoa wa Lindi, Pwani na Morogoro ambayo ina mito muhimu kwa ajili ya kutoa maji ya kunywa na hata mabwawa ya kuzalisha umeme.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, aliwahi kueleza namna misitu mingi ya mkoa wake inavyovamiwa na wafugaji, akisema baadhi ya wafugaji walioko Lindi wanazungumza lafudhi sawa na waliomaliza misitu mkoani Shinyanga ambako aliwahi kuhudumu pia kama mkuu wa mkoa.

Telack ambaye wasifu wake ni pamoja kusomea shahada ya uzamili katika maendeleo ya vijiji, Chuo Kkiku cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anasema kilimo tunachosema ni uti wa mgongo kitashindikana kama hatutakuwa na misitu kwa sababu kilimo chetu kinategemea mvua na misitu ina nafasi kubwa ya kuvuta mvua na kulinda vyanzo vya maji.

Faida nyingine ya misitu kwa mwanadamu na viumbe hai wengine ni kunyonya hewa ukaa na kutoa hewa safi, kuwa makazi ya viumbe mbalimbali na kutoa miti-dawa.

Misitu huwezesha pia ufugaji wa nyuki, kutoa mbao za aina mbalimbali na nishati za kupikia kama mkaa na kuni na hasa kama vitu hivyo vitavunwa kwa njia endelevu.

Pamoja na kwamba Watanzania wanahitaji mifugo kwa ajili ya nyama na maziwa na pia kutoa ajira, ni wakati wa kuhakikisha wafugaji wanafuga kisasa, wanatumia maeneo waliyopangiwa, wanapunguza idadi ya mifugo na kulima malisho kwa ajili ya mifugo yao. Lazima wabadilike, ‘wahifadhi’ mifugo na si ‘kuichunga’.

Ni muhimu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na viongozi wa mikoa mbalimbali kuboresha hali ya ufugaji ili kupunguza pia migogoro ya ardhi. Wahusika wasione kigugumizi kupiga mnada kila mahala ng’ombe walikovamia.

Chanzo: Habari Leo
 
Naona unyan'ganyi na uporaji, serikali inachangia pakubwa sana kukuza umaskini kwa wananchi wake, kuanzia tozo kila sehemu mpaka kuwanyan'ganya mifugo yao, kwangu faini ingekuwa adhabu ya haki kwa hao wafugaji, unless wakirudia tena, ndio wachukue sehemu ya mifugo yao, na sio yote.
 
Ufugaji wa kuhama hama hauna nafasi tena kwenye Karne hii ya 21. Kama mtu hawezi kufuga kwa kutulia auze tu ng'ombe wake wote. Tukiwachekea wafugaji siku si nyingi nchi hii itageuka jangwa
Naona unyan'ganyi na uporaji, serikali inachangia pakubwa sana kukuza umaskini kwa wananchi wake, kuanzia tozo kila sehemu mpaka kuwanyan'ganya mifugo yao, kwangu faini ingekuwa adhabu ya haki kwa hao wafugaji, unless wakirudia tena, ndio wachukue sehemu ya mifugo yao, na sio yote.
 
Naona unyan'ganyi na uporaji, serikali inachangia pakubwa sana kukuza umaskini kwa wananchi wake, kuanzia tozo kila sehemu mpaka kuwanyan'ganya mifugo yao, kwangu faini ingekuwa adhabu ya haki kwa hao wafugaji, unless wakirudia tena, ndio wachukue sehemu ya mifugo yao, na sio yote.
Umetembelea mikoa ya wafugaji umeona kulivo kukame? Unataka tuharibu na mikoa yenye asili ya kilimo kisha tutaishi vipi? Mkuu lazima tubadilike na hakuna mabadiliko yasiyo na maumivu. Mifugo hiyo ipigwe mnada kama wanaweza watanunua wao wenyewe na wasipoheshimu sheria watanyang'anywa tena. Mazingira lazima tuyalinde kwa nguvu zote kwa kuwa hayo ni muhimu kwa wanadamu na viumbe wengine.
 
Natamani ukame utawale kwa miaka kumi hadi ishirini mfululizo ili tuweze jifunza kwa vitendo kama wakenya na wasomali wanavyo pambana na ukame...

Baada ya hapo ndio tutaelewa nini maana na umuhimu wa kutunza mazingira... kwa maendeleo endelevu
 
Umetembelea mikoa ya wafugaji umeona kulivo kukame? Unataka tuharibu na mikoa yenye asili ya kilimo kisha tutaishi vipi? Mkuu lazima tubadilike na hakuna mabadiliko yasiyo na maumivu. Mifugo hiyo ipigwe mnada kama wanaweza watanunua wao wenyewe na wasipoheshimu sheria watanyang'anywa tena. Mazingira lazima tuyalinde kwa nguvu zote kwa kuwa hayo ni muhimu kwa wanadamu na viumbe wengine.
Ukame una wachapaga huko monduli longido na maeneo mengine simanjiro nk

Mifugo ina pukutika kama kuku wa mdondo
 
22967C11-6388-44F6-A7DE-2E14406524A0.jpeg

9FDF5F66-185D-401C-8244-02F6DEC220FF.jpeg

7CC208AF-D224-4A77-B99C-F1B3913A81E6.jpeg

510ACF3F-9CE2-47F7-B8A6-6834542CAB06.jpeg
9A31D1CB-91B6-47A9-B484-E4639A1D41FF.jpeg
 
Attachments

  • 5E7EE854-C214-41D0-8AF7-E729B4BDA66D.jpeg
    5E7EE854-C214-41D0-8AF7-E729B4BDA66D.jpeg
    40.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom