Katavi: Wananchi watakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ya Wakulima na Wafugaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
f5fc9c1f-d643-4ca6-b609-60a1b58eaf33.jpeg

Mkaguzi wa Kata ya Kasansa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Elibariki Kateman amewataka wakulima na wafugaji wa kata hiyo kutokuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji katani humo.

Mkaguzi huyo ametoa kauli hiyo wakati akitoa elimu ya ushirikishwa Jamii ambapo amewaambia wananchi wa kata hiyo ambayo inajishughulisha na kilimo na ufugaji kufuata sheria za matumizi bora ya ardhi ili kujiepusha na migorogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Ameongeza kuwa migogoro hiyo inawarudisha nyuma kimaendeleo wananchi wa kata hiyo huku akisema atopenda kusikia kata yake inamigogoro ya wakulima na wafugaji.

Katemani amewaomba wananchi hao kuzingatia matumizi bora ya ardhi ili kuondoa changamoto hiyo katika kata ya Kasansa iliyopo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.

78e134b5-2125-4e17-8ffc-39303a785f05.jpeg

dbfa192b-0c37-4227-88ec-d179024353b9.jpeg

Pia amewambia wananchi hao kumekuwepo na tabia ya wananchi wa kata hiyo kutowapeleka watoto shule akiwasihi kuwa endapo watafanya hivyo watakuwa wanawanyima watoto haki yao ya Msingi ya kupata Elimu.

Mkaguzi Katemani amesema serikali imejenga shule kwa lengo la kuwapa watoto elimu ambapo amewaomba wananchi hao kuwapa elimu ili kupunguza wahalifu katika Jamii.

Sambamba na hayo amewaomba waendele kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za uhalifu na wahalifu ili kata hiyo iendelee kuwa shwari muda wote.
 
Back
Top Bottom