BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
"Wananchi kuuawa na kuporwa mali zao katika siku za karibuni imekuwa ni jambo la kawaida, wananchi kuuawa na kuporwa mali zao kwa visingizio vya kusimamia sheria za uhifadhi, mfano katika maeneo irani na hifadhi kunaripotiwa taarifa za wafugaji kuuawa, wanawake kuuawa wakiwa wanakusanya kuni kwenye misitu ya hifadhi, wengine mifugo yao kutaifishwa na kuuzwa kiholela na Serikali na hata wakishinda kesi Mahakamani mifugo yao hawarejeshewi, haya ni maonevu na dhuluma iliyopitiliza kwa wananchi wetu na ni kinyume kabisa na malengo ya Uhuru na Mapinduzi" -Mpina
Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) amezungumza hayo alipokutana na Wanahabari kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka Sitini (60) ya Mapinduzi ya Zanzibar