Mbeya: Mwamba auza sehemu ya pori la akiba Rungwa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani humo kumsaka na kumtia nguvuni, Andrea Ngomeni, mkazi wa Kijiji cha Kambikatoto wilayani Chunya kwa tuhuma za kuuza eneo la pori la akiba la hifadhi ya msitu wa asili Rungwa.

Homera ametoa agizo hilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya baada ya kufika katika hifadhi na pori la Rungwa Two na kukuta sehemu ya hifadhi imefyekwa kwa ajili ya kilimo na mifugo na kujulishwa kuwa eneo hilo limeuzwa kwa wafugaji kutoka wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

"Nawaagiza polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kumsaka huyu bwana Andrea akamatwe ili hatua zichukuliwe, maana haiwezekani watu wanajifanyia wanavyotaka," amesema RC Homera
 
bwawa-rungwa.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mkoani humo kumsaka na kumtia nguvuni, Andrea Ngomeni, mkazi wa Kijiji cha Kambikatoto wilayani Chunya kwa tuhuma za kuuza eneo la pori la akiba la hifadhi ya msitu wa asili Rungwa.

Homera ametoa agizo hilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo baada ya kufika katika hifadhi na pori la Rungwa Two na kukuta sehemu ya hifadhi imefyekwa kwa ajili ya kilimo na mifugo na kujulishwa kuwa eneo hilo limeuzwa kwa wafugaji kutoka Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

"Nawaagiza polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kumsaka huyu bwana Andrea akamatwe ili hatua zichukuliwe, maana haiwezekani watu wanajifanyia wanavyotaka," amesema RC Homera.

Chanzo: Nipashe
 
Hizi nguvu zingetumika kuwasaka mafisadi huyo ndugu asingekuwa na muda wa kuuza pori la akiba. Maana kwa rasilimali hizi kila raia angekuwa millionaire kama si Bilionea.
Sasa misitu na mapori ya nini tena huku tunayo mengi na serikali imeshindwa kutumia kuondoa ufukara
 
Hapo Msukuma kashapelekwa chaka (katapeliwa) sasa sijui Homera atawasaidia hao Wasukuma au ndio imekula kwao
 
Back
Top Bottom