Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Ringo Edmund na wengine, nawaombeni sana tuepuke political sentiments kwenye huu msiba ili tusiugeuze kuwa ni mtaji wa kisiasa!.

Ukianza hizi comments za Chadema hivi mara Chadema vile, usituprovoke hapa tukakushishia nondo na data mpaka percentage za viongozi wa Chadema ni kina nani na concetration ni kabila gani?!.

Naomba tuache siasa tumzike kwa amani mpendwa wetu Regia! Haya mengine tuyalete baada ya msiba ndipo tukadilane Chadema ni chama cha kitaifa kwa kiwango gani!?

Rip Regia!.
Pasco bana! Tulia wewe, na ushukuru Mungu.
 
Umoja wa wanawake wabunge wote wanatoa salamu zao.

Zinatolewa na Mhe Susan Lyimo.
 
Nilikuwa nimetoka nimerudi kwa ajili ya huyo kipenzi chetu .lala pumziko salama la milele
 
jaman jana nimepata habari kuwa gari la marehemu limesukumwa zaidi ya kilometa kumi na uku wananchi wakilia na kudai uchaguzi ufanyike mapema sana kwa sababu walio wengi wanajua aliyekuwa mbunge wao ni regia mtema na awamtambui mbunge wao wa ccm hakika ni machungu sana na hatuna jinsi juu ya hili ni kumuachia Mungu ndiye muweza yote
 
Mkuu, unasikia rahaaa kuongozana na JK.....hahahahaaa!!! wewe bana!!!
hajui muda huyo, si unajua jamaa zetu hawa? wewe usingehangaika kutoka Dar alfajiri!! Safari njema mkuu, angalieni barabara mbaya hiyo, kona na madaraja kibao tu!
:focus:
Birigita usilete siasa kwenye msiba wetu!.
Jamaa zako walilala moro na hiki kibaridi baridi na vimvua vua, walijihimu sana kuachia yale mablangeti mapema!.
 
Poleni sana na Mungu awape moyo wa uvumilivu na mumlaze Dada Regia Salama.
R.I.P dada Regia!
 
Mengi tutasikia lakin ukweli unasimama pale pale kuwa Regia ameshatutoka na kazi ya Mola haina makosa.

Ni vizuri kwa sasa kumuombea kwa Mola mambo yake yawe mepesi aweze faulu..
 
Umoja wa wabunge wa Morogoro,unatolewa na Mhe Dr Mponda.waziri wa Afya.
 
Dada Regia katuonyesha njia na kutupa hari,ni muda sasa wa wana Morogoro kuamka na kupigania Moro yetu na Tanganyika yetu kwa ujumla ili tuache sifa na historia nzuri kwa nchi hii kua wana Moro pia twaweza na si wazembe!Moro stand up na tumuenzi vilivyo dada Reggy
 
Salamu za serikali zinatolewa na Mhe Hawa Ghasia.
 
Nenda Mpiganaji Regia Mtema, nenda upeleke Salamu zetu kwa Nyerere mwambie Tanzania imegeuka shamba la bibi, tena wale alio waamini ndio wanalipeleka taifa kubaya, wala rushwa na mafisadi waliokubuhu ndio viongozi wa CCM na serikali na wengne bila haya wanafanya mikakati ya kwenda ikulu. Nenda mpiganaji, nenda kakutane na Amina Chifupa mwambie vijana wamehamasika sana katika siasa na sasa wako wengi bungeni kuliko kipindi chochote cha historia ya nchi, mwambie wauza madawa wa kulevya bado wako matumbo joto na wanakamatwa kila kukicha.

Nenda mpiganaji wetu, peleka salamu zetu kwa Rasta,kamanda na Mpambanaji Chacha Wangwe mwambie harakati za kupigania maslahi ya wachimbaji wadogo wadogo yanaendelea japo jimbo lake la Tarime CCM wamelitwaa tena ila wapambanaji hawajachoka watalitwaa tena, nenda mpambanaji kakutane na kiongozi wa mashambulizi kanda ya ziwa na magharibi kamanda Philipi Shelembi mwambie chaguzi ndogo kata yake imeendelea kuwa chini ya wana mageuzi ila mpaka sasa matokea halisi ya jimbo la Shinyanga mjini hayajawekwa sawa kama alishndwa kwa kura moja au asilimia moja. Nenda kakutane na Silima mwambie jimbo lake la Uzini bado chaguzi ndogo ila umepangwa mwezi ujao wapiga kura wake watawakilishwa vyema asipate hofu.

Nenda Regia kakutane na Edward Sokoine mwambie njozi zake za kilimo leo wanaita KILIMO KWANZA ila kiutendaji ni KILIO KWANZA, mwambie kuna fisadi mmoja anajifananisha nae kama mtaji wa kisiasa, Nenda kutana na Simba wa Vita Kawawa, mwambie hakuna vita tuliyoishinda wala dalili za ushindi hazipo, umaskini unaongezeka kila kukicha, pengo la maskini na tajiri linaongezeka, ujinga unashamiri kwani wanafunzi wako sekondari hawajui kusoma wala kuandika na maradhi yanashamiri hata net za mmbu tunapewa msaada toka nje! Nenda mpambanaji nenda kamanda ona mamilioni ya watu wanavyokusindikiza na kulilia huu ni uthibitisho kuwa ni kipenzi chetu sote na sio kwa watu wa Ifakara tu.


Kamanda usiache kukutana na wasomi wapiganaji, kakutane na Prof Haroub Othumani, Prof Chachage Chachage, Prof Mushi na Prof Shayo, waambie tuna wamiss sana katika mchakato wa KATIBA MPYA kwani wanataaluma wengi leo wanachumia tumbo na hawasimamii maadili na miiko ya taaluma zao


Mpinaji huwa tunasema kazi na dawa! Ili mazungumzo yasichoshe Gwiji wa muziki Mbaraka Mwinshehe na TX Moshi William watawaburudisha, ila kabla Mtoto wa Dandu hajapanda stejini mwambie Tanzania Music Awards imechuliwa na wajanja wanaipeleka kiujanja ujanja tu na sio kama malengo ya uanzishwaji wake, usiache kumualika Mr Ebbo aliyeona ufahari mkubwa kwa umasaai na utanzania wake mwambie uzalendo wake kwa taifa utaenziwa na apige kibao cha mi mmasai bana ili Sokoine akisikie, kamanda usiache kuwa alika Complex na Vivie kuja kutoa support kwa wanamuziki. Usiache kuwa kuwasemea vyema wasanii wa maigizo na filamu mchukue mzee Kipara kama mshauri wako mkuu pia akusaidie kuwaona hao wazee kwani alicheza nao ktk ujana wake


Mpiganaji ungana na hao ndg, jamaa, rafiki na viongozi wetu. Waambie kwa ujumla wenu ni waungwana sana na mmepata bahati sana hapa Tanzania na hata duniani ya kupendwa, kuaminika na kuheshimika. Kikubwa zaidi ni siku zenu za mwisho mmesindikizwa na wapendwa wenu ktk familia, mmezikwa na washirika wenu na katika mazishi yenu pakuweka mguu hakuna wakati kuna wengne wamekwenda kwa kuzikwa na watu wachache kuliko ilivyodhaniwa, wengne wamezikwa kana kwamba hawana thamani duniani, hawana ndg wala washirika! Pumzikeni kwa Amani mmebahatika kusindikizwa kwa heshima.


Amani iwe juu yenu, nafsi ziwe kwatu kwa kuwa tutayasimamia vyema yote mema mliyo yaanzisha na mtakuwa mfano mwema kwetu, tutarekebisha mlipokesea! Mwambie Nyerere aendelee kupumzika kwa kuwa maadui wa taifa letu tumewajua na CCM yake wamewajua na Gamba watavuliwa, kama kwenye chama wakishndwa hukumu ya wananchi 2015 itakuwepo. Mwambie wa Tz sasa wameamka kuliko kipindi chake na gharama yoyote watatea ardhi zao na utu wao, dhuluma na unyang'anyi utafika mwisho. Mwambie Simba wa Vita mzee Kawawa asipate hofu anawakilishwa vyema na watoto zake bungeni tena Zainabu ni shujaa kama yeye, kamanda mwambie Sokoine ashushe morali uliopanda kwa kuwa mpaka leo tuna amini ndio waziri mkuu bora kuliko wote, njozi zake leo ndio zinatimizwa na binti yake Namelok anamwakilisha vyema. Kamanda waambie wapambanaji na makamanda Wangwe na Shelembi wasiwe na hofu kwani mapambano yanafika mwisho na makamanda wanaelekea kushinda 2015 hii inadhibitishwa na w/mkuu Pinda aliposema bungeni makamanda wanawanyima muda wa kufanya kazi, inathibitika kwa kuwa toka uchaguzi uishe makamanda ndio ajenda midomoni mwa watu, ugumu wa maisha umeongezeka na wananchi watahitaji mbadala. Mpambanaji mwambie Amina Chifu nawe msiwe na hofu pumzikeni kwa amani kwani vijana 2015 watakuwa wengi bungeni na kuandika historia mpya, mwambie vita ya madawa ya kulevya vijana tunaiendeleza kwa nguvu zote. Mwambie mtoto wa Dandu atulie kamanda Sugu ameanzisha harakati za kupambana na wanyonyaji wa kazi za wasanii akimaliza ataikomboa Tanzania Music Awards na kuirudishia heshima yake. Kamanda usiache kuwaambia Mbaraka Mwishehe, TX Moshi, Ebbo,Complex na Vivie kuwa muziki sasa unalipa zaidi na unawatoa wasanii kimaisha ila kazi zao wao hazijawahi chuja na zinapendwa na rika zote. Kamanda Regia Mtema ukimaliza kuwafikishia salamu zetu nawe upumzike kwa amani kwani tutakuenzi daima
 
poleni mliotuwakilisha
tunaomba picha za matukio tafadhali,dada josephine kamara imeissha chaji?
 
Hawa ghasia anatoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali,jk bado hajawasil hapa japo inasemekana atashiriki.
 
Mengi tutasikia lakin ukweli unasimama pale pale kuwa Regia ameshatutoka na kazi ya Mola haina makosa.

Ni vizuri kwa sasa kumuombea kwa Mola mambo yake yawe mepesi aweze faulu..

Taratibu sheikh,

Kwamba Regia ametutoka hilo ni dhahiri, kinachofanyika hapo ni katika kukamilisha zoezi la kuupumzisha mwili wake katika nyumba yake ya milele.

Na hayo mengine mengi unayosema tutayasikia ndio ukweli wenyewe, kwamba yatasemwa na yameshaanza kusemwa.
 
Asante kwa updates, i wish ningekuwepo hapo japo nitoe salamu zangu za mwisho. R.I.P Regia!
 
Back
Top Bottom