The FaMa
Senior Member
- Oct 6, 2011
- 125
- 27
Umati huu wa watu toka kila kona nchi unadhihirisha jinsi dada Regia alivyokua kipenzi cha watu!
Kwa kweli nafarijika sana kuona ni namna gani Dada Regia aligusa maisha ya watu. Tangu taarifa ya kifo chake kutolewa, wananchi wengi sana wamejitokeza kumtakia pumziko la amani. Naamini hata familia yake inafarijika kwa maisha ya binti yao, kwani kwa umati unaojitokeza kumsindikiza tangu kule Tabata, Karimjee na sasa huko Ifakara, ni wazi kuwa Regia alikuwa ni kipenzi cha wengi. Huenda hata huko alikopumzika haamini anayoyaona huku duniani jinsi watu walivyompenda.
Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani na kumpatia raha ya milele. Amevipiga vita vilivyo vema na kuvimaliza, anastahili pumziko.
Ulale vema Dada Regia, tutakukumbuka.