Nashukuru kaka yako muelewa, yeye mambo ya kupiga magoti wala hapendi. Hao wengine nitaweka kichwa ngumu tu.
Pretty mpendwa nilitaka nifunge domo langu kwenye mada hii ila niliposoma hii nimeona bora nikueleze niliyofundishwa na mama yangu.
Kitu cha kwanza kabisa unatakiwa ujue msimamo wa mumeo (wa kiukweli sio wa mdomoni), je ni wale wanaosikiliza ndugu au ana msimamo wake? unaweza kujifanya kichwa ngumu mwenzio akakubadilikia ukashangaa.
Waheshimu ndugu zake wote hata watoto kwani ameishi nao kipindi kirefu kuliko alivyoishi na wewe, so wewe huwezi ukaja from nowhere ukaanza kumuonyesha ubaya wa ndugu zake. Hata kama ni wabaya mwache aseme mwenyewe na hata akisema nyamaza kimya kwani anaweza kuwa anakupima vilevile.
Hakuna binadamu asiye na maudhi, uvumilivu ni kitu cha muhimu sana, usiwape tu nafasi ya kukuudhi sana.
Hewala si utumwa, kwani ukipiga goti akafurahi wewe inakupunguzia nini? Unapaswa kukataa vitu tu ambavyo vinakudharaulisha. Sio vizuri kufanya vitu vinavyokufanya uonekane tofauti sana nao. Angalau wakuone kama mwenzao hata kwa asilimia fulani.
Ongea inapobidi, mama mkwe na wifi sio mashoga zako. Ongea kidogo sana sikiliza sana, wakisema mtu usitie neno. Sijui kama unajua kitu kinaitwa kucheka kichina, huku ni kusmile kumridhisha mtu. Mara nyingi wakiongea we cheka kichina, usi-support sana maongezi smile tu waone kama uko nao. Ishi maisha yako usitake sana ukaribu wa kuzidi, ni kusalimiana na kusaidiana.
Muhimu waheshimu, sio kuwa wewe ni mke basi wewe ni bora hapana. Mama ana nafasi yake kama mama na ndugu wana nafasi zao kama ndugu wewe huwezi kuzireplace na kila moja ina umuhimu wake. Muhimu usiwaruhusu tu kukuingilia katika mambo yako ya ndani ya ndoa, na usiwaambie kwa hasira ikitokea wakifanya hivyo, waambie tu kwa utaratibu na kwa heshima
Niamini watakuheshimu