Mawifi jamani, hivi wana nini?

Mawifi jamani, hivi wana nini?

jamani wadada na JF tukubali kuwa sometimes sisi waolewaji ndo huwa tunakuwa na matatizo, mambo ya kwenda umejiandaa kuidhibiti familia ya mume. unajua sio familia zote ambazo ni ngumu kuishi nazo ila kwa vile tunatoka kwetu tukiwa tumejiandaa jinzi ya kuwadibiti mama mkwe na mawifi ndo inakuwa balaa. wakati mwingine wifi au mama mkwe anaweza akakosea kitu kidogo, kibinadamu, ambapo hata mama au mdogo wako anaweza akafanya kitu kama hicho lakini sababu kafanya wifi/mama mkwe inakuwa balaa.
tujitahidi na sisi kuchukulia familia za waume zetu kama familia zetu, labda haya mzogo yatapungua


hii point mwanakwetu, sasa unakuta dada zako na mama yako mzazi wakija kwako heshima mkononi na wewe unawaheshimu lakini wakija mawifi ni kunyanya paa tu kwa kwenda mbele, mara akuamrishe mara akufokee, ukifanya kizuri akutoe kasoro...kuna wengine aah hawana shida na mtu kwa kwelli hao hata kuwachukulia kama dada inakuwa rahisi lakini kuna wengine balaa kweli kweli

mimi nakumbuka kuna shangazi yangu alikuwa kila akija nyumbani lazima aondoke na kitu, mama analalama weee lakini kumwambia hathubutu eti kwa vile ni wifi yake..
 
Nyamayao kama wanawake wote wangekuwa na ujasiri huu matatizo ya mawifi na wakwe yangepungua sana, tatizo wengine hawapendi halafu eti hawasemi wanayaweka tu moyoni huku ndoa zao zinaingia migogoro...


mie ctaki kabisa, wakati mwingine mr akutibue huku familia yake nayo ikutibue, nimegoma mie, lakini hizi mila/desturi zinatubana sana wanawake jamani, nikikaa na ma frnds zangu kwenye kilaji kilio cha kila mmoja ni mama mkwe/wifi, na neno "vumulia" hata ukienda kumweleza mamako mzazi shida unazoletewa ndio jibu utakalopewa....sasa hivi napumua ndugu yangu na wananijua mie sio wa masihara kabisa....
 
unajiandaaje sasa? kama mie mama mkwe/wifi nilikuwa naelewa nao mwanzoni, baadae wakanibadilikia, kwanini na mie nicbadilike?...halafu hawa watu hawafanyagi ishu za kikawada ambazo hata mamangu anaweza kufanya, mamangu hawezi kufanya kitu cha kuniumiza roho hata kidogo lakini hawa watu malengo yao yote ni kuumiza tu...

Nyamayao, nadhani hujanielewa vizuri. Mimi na wewe tunajua kwamba kuna watu wanapotaka kuolewa wanapanga kabisa mbinu za kwenda kuishi na wakwe..... ndo hayo kwamba "mimi ndo wasinibabaishe kabisa, kama kuolewa nimeshaolewa". lakini kuna wengine (I guess) kama wewe ambao wanaenda tu, na mambo yanabadilika ukiwa ndani. Mimi nakusifu sana kama una courage ya kuongea na mama mkwe/wifi yako maana wengi hawana hiyo courage.
hawa watu huwa wanahitaji tu kukumbushwa kuwa wewe pale ni part of the family, sio externality
 
Jamani maswala ya ndoa yanachanganya sana navyo wasoma hapa kama vile nisioe vile niwe namega tu maana yanachanganya haswa mala hiki mala unapendelea kule kha!


ndoa ina utamu wake Fidel, ina makashkash kibao, na cjui kama kuna mtu anaweza sema ndoa yake tambarare 100%, kama yupo imebarikiwa hiyo, na kumbuka ndoa sio wewe na mkeo tu ni familia mbila sasa mzozo ukitokea hapo ujue unahusu familia zote mbili, mfano ndio kama huu hapa sasa wifi/mama wakwe mara nyingi tafrani zinaanzia hapo....ingia ingia luv, hivi vijimambo humu ndani vickutishe.
 
wewe wacha jeuri yako mkung'utie wifi yako magoti umeanza jeuri mapema minaona..sasa baadae bwana nae atakuambia anataka uchume ile mboga utakataa pia hehe kaazi
 
Chrispin said:
Lol! Jifagilie mamii. Hivi MJ1 yupo? Hapa lazima tungetungiwa na kashairi. Si unakumbuka limjamaa lake lilikuwa linampeleka spidi? Sijui kama lilikuwa mawifi zake walikuwa upande upi.


walaaa, nazungumzia hali halic Chriss.
 
Lol! Jifagilie mamii. Hivi MJ1 yupo? Hapa lazima tungetungiwa na kashairi. Si unakumbuka limjamaa lake lilikuwa linampeleka spidi? Sijui kama lilikuwa mawifi zake walikuwa upande upi.

We nawe umefurahiiiiii! Mwone vile.

Mie wifi zangu nilikuwa nao watano nashukuru MUNGU wananipenda mpaka leo.
 
We nawe umefurahiiiiii! Mwone vile.

Mie wifi zangu nilikuwa nao watano nashukuru MUNGU wananipenda mpaka leo.

Sasa kwa nini hawakukusaidia kulikong'oli lile limjamaa? Manake samtaimz mawifi wanaokoaga jahazi.
 
Sasa kwa nini hawakukusaidia kulikong'oli lile limjamaa? Manake samtaimz mawifi wanaokoaga jahazi.

We naye sasa hata wangeingilia kati kuna faida gani kujua kuwa unaishi na mtu kwa vile dada zake wamemlazimisha?.
 
Hiyo ndio raha ya wachaga, hawamind mambo ya magoti. Huku ninakoenda magoti hao wanaona kama ndio heshima kwa msichana.
Sasa si bora magoti,je ungeenda kwa wale wenzetu salamu ni saluti na gwaride kama upo kambi ya jeshi,ingekuwaje?
 
Hiyo ndio raha ya wachaga, hawamind mambo ya magoti. Huku ninakoenda magoti hao wanaona kama ndio heshima kwa msichana.
Sasa kama unaona wachaga ni poa badili muelekeo uone kama hujageuzwa punda,coz bila kazi kwa mchaga hamna heshima,ni kazi kuanzia asubuhi mpaka lukwiri,tena ni manual works tuu,ukitoka ofisini dukani au kukamua ng'ombe,lazima uchakae!!
 
Sasa kama unaona wachaga ni poa badili muelekeo uone kama hujageuzwa punda,coz bila kazi kwa mchaga hamna heshima,ni kazi kuanzia asubuhi mpaka lukwiri,tena ni manual works tuu,ukitoka ofisini dukani au kukamua ng'ombe,lazima uchakae!!


wewe unazungumzia wachaga wa miaka ipi....1905?...
 
Hiyo ndio raha ya wachaga, hawamind mambo ya magoti. Huku ninakoenda magoti hao wanaona kama ndio heshima kwa msichana.
Jifikirie mara mbili kama kweli unampenda huyo mchumba wako,jibu likiwa kweli unampenda basi magoti sio tatizo,hata ukiambiwa kuwa unatakiwa uchapwe viboko ndio salamu ya kwao,upendo utakulinda tuu!!lakini kama upo after some thing lazima utaje dhambi mpaka za babu zako kaburini,yaani utaona ni mateso mno!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom