Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,914
Kama huyu Professor Nkunya ndio mhusika wa kutatua hili tatizo basi tumekwisha! Mzee haelewi tatizo.
Anasema Watanzania wanakuwa "trapped" na wauza shahada. Yani anamaanisha hawa walimu wa Mzumbe na mawaziri wenye u-professor Maji Majeru walikuwa hawajui kwamba nia yako ni kupata hivyo vyeti feki! Nkunya anaogopa kusema ukweli, au ni kilaza mwingine huyu?
Halafu, kukuonyesha zaidi kwamba Professor Nkyunya hajui kinachoendelea au si msema kweli, anatamka "wale wanaotaka kusoma nje ya nchi wawasiliane na sisi kwanza kwa ushauri..."
Mtu ambae anataka kupata shahada ya uongo uongo mtandaoni utategemeaje aje kwako kwa ushauri, au sijui ajipekele ubalozini, kwani ye mjinga akanyakwe? Yani Prof. Nkunya haelewi kwamba haya matatizo ni usanii wa kunuia, intentional chicaneries. Huyu Professor Nkunya ndio yuko in charge wa hili tatizo?
Alitakiwa aseme wazi wazi kwamba ukijipenyeza kwenye kazi ya mtu kwa vyeti feki feki hiyo inaweza kuwa ni fraud! Hakuna kubembelezana eti wamekuwa "trapped"! Bongo tumebarikiwa viongozi jamani jamani!
Ha, ha, ha, - unanikumbusha yule professor wa UDSM anayetoa ripoti yake na kudai kuwa performance ya Raisi Kikwete ni magnificent ila ya serikali yake ni deplorable. Alternatively wale wanaoamini kuwa CCM ni safi ila viongozi wake waliochaguliwa ndio MAFISADI. Halafu tunashangaa kwa nini hatuendelei..........