Mawaziri waghushi vyeti

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Mawaziri waghushi vyeti

• Wahaha kulinda siri isivuje

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KASHFA ya kughushi vyeti vya taaluma mbalimbali imeendelea kulitafuna taifa, baada ya kubainika uwepo wa mawaziri wanne wanaodaiwa kughushi vyeti vya elimu ya juu.

Kugundulika kwa mawaziri hao kunatokana na kuwapo kwa taarifa kuwa baadhi ya wasomi nchini wamepata taaluma hizo kupitia kwenye vyuo visivyotambulika kimataifa, hivyo elimu yao kutokuwa halali.

Aidha, kuna kundi linalodaiwa kughushi vyeti vya vyuo mbalimbali vya nje ambavyo havina umaarufu au sifa zinazotambulika kimataifa.

Miongoni mwa wasomi ambao wamo katika kundi la mawaziri ni wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, ambao wamepata shahada za falsafa (PhD) lakini zimebainika kupatikana kupitia katika tovuti mbalimbali za vyuo hivyo visivyo na sifa.

Kutokana na wahadhiri wao kutopata elimu hiyo kwenye vyuo vinavyotambulika, uongozi wa chuo hicho pamoja na Kamisheni ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu (TCU) imewataka wale wote waliopata elimu katika vyuo hivyo kusomea upya shahada zao katika vyuo vinavyotambulika kimataifa.

Habari ambazo zimeifikia Tanzania Daima Jumapili, zinadai kuwa mawaziri hao wanne (majina tumeyahifadhi), ambao ni madaktari wa fani mbalimbali hadi sasa hawajaweza kusomea upya shahada zao kama walivyoshauriwa na vyombo vya kitaaluma.

Hadi sasa mawaziri hao wamekuwa wakihaha kuhakikisha kuwa utata wa elimu yao hauwekwi hadharani ili kulinda heshima yao waliyojijengea ndani na nje ya nchi.

“Kuna mawaziri wanne ambao taaluma zao zina utata, hasa kutokana na wengine kughushi na wengine kusoma katika vyuo visivyotambulika kimataifa, uchunguzi wa walikozipata taaluma zao unaendelea,” kilidokeza chanzo chetu cha habari.


Mmoja wa mawaziri hao siku za hivi karibuni amekuwa akionekana zaidi katika vyombo vya habari, kwa msimamo wake wa kuitetea nchi ili isiingie katika mikataba na makubaliano na nchi nyingine bila kufanya tathmini ya kina.

Waziri mwingine anayedaiwa kuwemo kwenye mkumbo huo aliwahi kuingia katika malumbano na vyombo vya habari kutokana na kumuandika kuwa anatetea ufisadi, pamoja na kuwemo kwenye kundi la wanamtandao.

Kutokana na sakata hilo, mawaziri hao huenda wakalazimishwa kuachia nyadhifa walizonazo ndani na nje ya chama au kufukuzwa, iwapo suala lao litavaliwa njuga na viongozi wao au wananchi.

Kashfa hiyo ya mawaziri kughushi vyeti imekuja huku Baraza la Mitihani la Taifa NECTA likiandamwa kwa shutuma za uvujaji wa mitihani pamoja na uuzaji wa vyeti vya elimu ya sekondari.

Matukio ya kughushi vyeti yamekuwa yakiongezeka kila kukicha hapa nchini, jambo linalohatarisha mustakabali wa taifa katika nyanja ya elimu, hasa katika zama hizi za utandawazi, ambapo nchi kadhaa zimekuwa zikielekeza nguvu zaidi katika sekta ya elimu ili ziweze kuwa na wataalamu watakaozisaidia kuandaa mipango ya maendeleo.

Mmoja wa wabunge aliyewahi kukumbwa na kashfa ya kughushi vyeti vya elimu ya juu ni Ali Ramadhani Kihiyo, wa Jimbo la Temeke (CCM), ambaye alifunguliwa kesi na Chama cha NCCR-Mageuzi iliyosimamiwa na mwanasheria wake maarufu wakati huo, Masumbuko Lamwai.

Mbunge huyo alilazimika kuachia wadhifa huo baada ya kubainika kuwa hakuwa na elimu hiyo kama vyeti vyake vilivyokuwa vikionyesha na hatimaye kuachia ngazi na kuitishwa uchaguzi mwingine.


Mbali ya Kihiyo, Mbunge wa Buchosa, Samwel Chitalilo (CCM), amekumbwa na tuhuma za kughushi vyeti, lakini hadi sasa anaendelea na ubunge, licha ya kuwapo kwa kelele za baadhi ya watu wakimtaka aachie ngazi kutokana na kashfa hiyo.
 
Last edited:
sasa tutawavalia njuga vipi mpaka waachie madaraka wakati mnatuambia majina yamehifadhiwa

ama kweli hii ndio tanzania,tutafika lakini
 
Dr Nchimbi E
Dr Matayo David Matayo
Dr Mary Nagu
Dr Makongoro Mahanga
Dr Kamala D

Mbona wapo wengi is more than 4 waliofichwa majina hapo!!
 
Dr Nchimbi E
Dr Matayo David Matayo
Dr Mary Nagu
Dr Makongoro Mahanga
Dr Kamala D

Mbona wapo wengi is more than 4 waliofichwa majina hapo!!

Serikali ya kifisadi inatetea watenda maovu yote wakiwemo wakupuaji wa mabilioni ya walipa kodi wa Tanzania na hata waliogushi vyeti vya elimu yao. Watanyamaza kimya kama hawajui au kusikia juu ya kashfa hii nzito.
 
......kuna haja ya kuwataja majina na taratibu za kisheria kama zilivyofanywa na NCCR ili watuhumiwa waachie ngazi kwani hawa ndio chimbuko la uuzaji wa vyeti NECTA. Bila kuanza na hawa NECTA itaendelea kuuza vyeti. Chamsingi hapa ni kukata mizizi yote ya ufisadi wa kila aina
 
Kikwete, kazi kwako baba. Wewe kama amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumia dhamana uliyopewa na watanzania wote kulivalia njuga suala hili. Wewe kama Rais una "Executive Powers" ambazo unaweza kuzitumia kukomesha kero nyingi zinazotusumbua sisi tuliokuchagua, na sisi kama raia tumechoshwa na kigugumizi unachokionyesha katika kutumia u-executive wako tuliokupatia kama Rais wetu. Majuzi umetufukuzia DC wa Katerero... We are waiting to see you striking again your honour... This matter is more serious than lile la DC kuamuru walimu wachapwe viboko. Act accordingly ndugu Rais... Act NOW!!!!

Ni dhahiri kwamba viongozi wetu inabidi wawe mfano bora kwetu sisi wananchi wote. Sisi wananchi inabidi tujifunze kutoka kwao. Kwa mtindo huu wa kufoji vyeti, je, unataka sisi tuige wanavyofanya? Je, unaitakia future nzuri nchi yetu ya Tanzania kweli? Kama kila meneja, mkurugenzi, ama waziri akija kuwa na vyeti vya kufoji in the future je kwa kutumia uwezo wako wa kufikiri je unadhani Tanzania itafikia level gani kimaendeleo? Je, unataka history iku-judge vipi kama kiongozi kwenye kukomesha jambo hili?

Fukuza hawa watu na sisi tutaona kweli tuna Rais.
 
Last edited:
Dr Nchimbi E
Dr Matayo David Matayo
Dr Mary Nagu
Dr Makongoro Mahanga
Dr Kamala D

Mbona wapo wengi is more than 4 waliofichwa majina hapo!!

Aliyekua Waziri wa Sheria naye akawa anavunja sheria na kukubali kuitwa "Daktari wa falsafa" wakati akiwa na ufahamu kwamba hastahili kuitwa hivyo. Kitendo hiki kinastahili kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kwenda Jela kabisa. Nakichukulia kitendo hiki ni kama kuchezea utawala wa sheria. Huwezi kuwa waziri wa sheria halafu wewe ndio unakua mstari wa mbele kuvunja sheria, tena kiwaziwazi (in public). Tanzania ufisadi uko katika kila kona.. Mungu tusaidie.
 
Last edited:
Sidhani kama Rais Kikwete anajali. Alishasema "kelele za mlango hazimsumbui ......" kuhusu so-called mheshimiwa Chitalilo. Kwake naona bora siku iende tu.
 
Tanzania Daima nao, si wangewaelekeza wasomaji wake JF where we dare to talk openly?

Hawa jamaa tumekuwa tunawasema toka kule Business Times. Hakuna haja ya kuficha majina yao.

Sidhani kama serikali inalipa hili suala uzito. Hawa jamaa ilitakiwa waumbuliwe tokea 2000 na kuambiwa vyeti vyao vya Ph.D havitambuliwi.

Hivi kweli kuwa waziri unahitaji Ph.D? Wamejidhalilisha bure kwa kuongeza qualification ambayo haiwaongezei kitu.
 
Sidhani kama Rais Kikwete anajali. Alishasema "kelele za mlango hazimsumbui ......" kuhusu so-called mheshimiwa Chitalilo. Kwake naona bora siku iende tu.

Kama kweli "Kelele za mlango hazimsumbui", basi historia inaweza kuja kum-judge kama "THE WORST PRESIDENT EVER".... worse than Mkapa, maana Mkapa alikua fisadi, then yeye Kikwete kama Rais akashindwa kuuchukulia hatua huo ufisadi wa Mkapa na wenzake...

Let's wait and see.
 
Tanzania Daima nao, si wangewaelekeza wasomaji wake JF where we dare to talk openly?
Hata hivyo Source ni JF, hawatoi credit kwetu japo sisi tunasisitiza mara zote magazeti kupewa credit. Hata hivyo ni vema hoja hii hatimaye imeanza kusikika kwa jamii.
 
.........namkumbuka sana Mkuu sam na Pundit kwenye mada hizi.....sijui wamepotelea wapi hawa wakuu..........
 
...not so fast hapo,kuna tofauti kubwa kati ya forgery na unaccredited,sio kama natetea substandard yeyote katika credential za mtu lakini huwezi kushtaki mtu au kumwita ameghushi vyeti kwa sababu vimetolewa na unaccredited school,swala la kihiyo ni tofauti na hawa...najua politically kuna some price to pay kwa issue kama hizi,solution ni kuwaondolea doctorate zao tuu na kuwaambia hazitambuliki!
 
...not so fast hapo,kuna tofauti kubwa kati ya forgery na unaccredited,sio kama natetea substandard yeyote katika credential za mtu lakini huwezi kushtaki mtu au kumwita ameghushi vyeti kwa sababu vimetolewa na unaccredited school,swala la kihiyo ni tofauti na hawa...najua politically kuna some price to pay kwa issue kama hizi,solution ni kuwaondolea doctorate zao tuu na kuwaambia hazitambuliki!

Nakubaliana na wewe koba, lakini kama hawa Waheshimiwa wangekuwa na nia ya kweli basi wangetoa kauli hadharani kueleza hivyo na kukana hizo PhD zao na kuitwa Dr. Lakini wamekaa kimya miaka nenda miaka rudi bila kusema chochote kuhusiana na hizo Phd zao fake, hivyo kwa maana nyingine sasa hivi wanastahili kutambuliwa kama wamegushi hivyo vyeti.

Umejipatia cheti ambacho baadaye kinakuja kugundulika kwamba kina hitilafu na hizi habari zimeandikwa katika magazeti mbali mbali, pamoja na hayowahusika wamekaa kimya bila kusema chochote, ukimya wao unaashiria hawako tayari kuukubali ukweli wa hivyo vyeti vyao na hivyo kuudanganya umma wa Watanzania kwa wao kuendelea kukubali kuitwa Drs.
 
...not so fast hapo,kuna tofauti kubwa kati ya forgery na unaccredited,sio kama natetea substandard yeyote katika credential za mtu lakini huwezi kushtaki mtu au kumwita ameghushi vyeti kwa sababu vimetolewa na unaccredited school,swala la kihiyo ni tofauti na hawa...najua politically kuna some price to pay kwa issue kama hizi,solution ni kuwaondolea doctorate zao tuu na kuwaambia hazitambuliki!

sawa Mkuu lakini kama wewe unapenda future yako iwe nzuri kwanini usome kwenye chuo kisicho na sifa?

Kwa mfano Dr. Nagu ni mtu mkubwa sana sasa na anatumia title ya Dr. lakini chuo alichosoma PhD ni ashington International University. Maelezo ya wikipedia yako wazi kwa jila mtu na yanasema hivi:-

Washington International University is an unaccredited institution of higher education founded in 1994 and currently incorporated in the British Virgin Islands. It describes itself as a "university without borders", serving clients from around the world via distance education. The university website states that WIU's graduates have come from 112 countries. he university has not sought educational accreditation and does not have a campus.

The Oregon Office of Degree Authorization stated that "[WIU is] operating illegally in Pennsylvania according to PA Department of Education. WIU is forbidden to advertise or offer its programs in Australia".
 
Kwa mtaji huu tutegemee maendeleo? kama hatuna vetting mechanisms ya kuhakikisha anayeteuliwa kwa nafasi fulani anafaa kwa vigezo vyote tutarajie nini? Nilidhani Rais kabla hajateua waziri kuna vetting process ya aina fulani kumbe hakuna, ni kuangalia tu kujuana siyo? Nashangaa huyu Chitalilo anafanya nini mpaka sasa, hata uwezo wake wa kufikiri sijui.....
 
Verting ipo. Waziri Nagu aliipata hiyo Ph.D wakati tayari ni Waziri. Naomba tutenganishe Ph.D fake na zile toka un accredited universities.
Sifa za kuwa Mbunge ni elimu ya angalau kidato cha 4. Sifa ya kuwa rais ni elimu (angalau) ya chuo kikuu. Amani Karume ameukwaa urais bila elimu ya chuo kikuu. Msomi wa Ph.D ya ukweli Zanzibar, Dr. Gharib Bilali alifnyiwa zengwe. Dr. Salim alipogombea naye alipigwa zengwe.
Huu ni udhibitisho tuu kuwa accademic credentials za viongozi wetu sio issue ndio maana JK ametulia kimya.
Tufike wakati tujiulize GPA ya Mkulu ikoje?. Kwa nini hakufanya Masters. Majibu ya maswali hayo yatathibitisha kwamba shule nene sio issue, issue ni kuwa mpiga domo mzuri wa kuinadi ilani ya uchaguzi kwa wananchi na CCM itaendelea kutawala milele!.
 
Kuwa na PhD feki ni kosa lakini ni zaidi ya kosa kwa mtu aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza nchi yetu KUKURUPUKA na kuteua VIHIYO hao kuwa mawaziri wetu.Tukumbuke kwamba "Dr" Nchimbi na wenzake HAWAKUJITEUA KUWA MAWAZIRI bali WALITEULIWA NA Dr (wa heshima) Jakaya Kikwete.Najua two wrongs do not make a right na hapa sitetei hawa Vihiyo bali namlaumu huyo aliyewateua pasipo kuangalia rekodi zao sahihi.Leo tunafahamishwa kuwa tuna mawaziri wenye elimu feki,kesho tutasikia tuna mawaziri wenye uraia feki.Hii nchi ni kama inaning'inia kwenye utandu wa buibui....

By the way,hivi hakuna mamlaka inayomshauri Rais kuhusu anaotaka kuwateua (i mean kumshauri baada ya kuwafanyia sort of profiling...vetting)?
 
Back
Top Bottom