Kuwa na PhD feki ni kosa lakini ni zaidi ya kosa kwa mtu aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza nchi yetu KUKURUPUKA na kuteua VIHIYO hao kuwa mawaziri wetu.Tukumbuke kwamba "Dr" Nchimbi na wenzake HAWAKUJITEUA KUWA MAWAZIRI bali WALITEULIWA NA Dr (wa heshima) Jakaya Kikwete.Najua two wrongs do not make a right na hapa sitetei hawa Vihiyo bali namlaumu huyo aliyewateua pasipo kuangalia rekodi zao sahihi.Leo tunafahamishwa kuwa tuna mawaziri wenye elimu feki,kesho tutasikia tuna mawaziri wenye uraia feki.Hii nchi ni kama inaning'inia kwenye utandu wa buibui....
By the way,hivi hakuna mamlaka inayomshauri Rais kuhusu anaotaka kuwateua (i mean kumshauri baada ya kuwafanyia sort of profiling...vetting)?
.....Mlalahoi....ukisikia jinsi SIASA inavyochukua uzito kuhusiana na hizi teuzi.....unaweza kuichukia siasa ya Tanzania maisha yako yote.......wee si umemsikia Kingunge anasema MASLAHI YA CHAMA KWANZA.......kwi kwi kwi kwi kwi......na teuzi zinakuwa hivyo hivyo MASLAHI YA CHAMA KWANZA............