Nimeambiwa hatimaye Kamala kafanikiwa kupata Ph.D inayotambulika kutoka Hull university.
Sina uhakika sana ila inaelekea baada ya scandal kuanza akajiandikisha kimya kimya na ameonekana akitembelea hicho hicho mara nyingi.
Wenye taarifa zaidi mnaweza kutujulisha. Kule bungeni bado hajaweka hiyo taarifa. Labda anasubiri watu wamshambulie ndio atoe ushahidi wake, au anasubiri 2010 wapinzani wake wakija na tuhuma ndio ataoe ushahidi wake.
Itaidi Kamala atuombe radhi kwanza kwa kutuletea Ph.D feki (aliyosomea kwa miezi mitatu) ambayo ilikuwa msingi wa uteuzi wake mbalimbali. Huo ni udanganyifu ambao unaadhibika chini ya sheria za nchi.