Jamani, jamani, jamani, why waste time discussing on these issues?
hawa phd holders wawe waasajiriwa ikifika muda fulani let say miaka 2, kama hatuoni contribution yake katika society, anaporwa hiyo phd yake, regardless alichukua oxford au PWU!
Tumeishia kusema tu lakini in reality, hizi zote ni standard na walioweka ni watu, private employers let say, wanahiari wa kuikubali phd yake au la! ili mradi ana deliver. au hakuna tena informer education? au mtu kujiita phd mnauma nini kuna watu kibao wanaitwa madocta, wengine viongozi- kama Karume! wengine wachungaji wote hao ni Drs!
kama kweli hii bodi yetu iko serious, hawa jamaa wafuatiliwe mchango wao ktk jamii, na wawe na uwezo wa kumvua hiyo phd, wapewe mamlaka ya kupiga marufuku matumizi ya title Dr kwa wasiostahili!
kupigishana kelele kuhusu hawa jamaa, wakati wale waliosoma hizo degree mnazoziita bora, hatuoni wanafanya nini, ili hali nchi yetu inaongoza kwa umaskini, huku tuna wataalamu kila kona, nalo linazua maswali.
tukiwawekea standard/task/laws watatakiwa wawe wanafanya kila mwaka, ili wazilinde title zao nadhani tutapiga hatua. haya majadiliano ya nani kasoma wapi hayamsaidii mtanzania wa kawaida na hasa taifa letu!.
NB. hili wengi huwa hampendi kuambiwa- PhD bora kabisa ni ile unayofanyia kwenye taifa lenu! sio utumwa huu wa kuvumbua kitu Japan, wala hutumii elimu yake TZ, PhD nyingi zilizofanyika nje ya nchi hazijalenga kulisaidia taifa letu, haya angalieni wanafanya nini! kwa ordinary person kwa sababu mmekosa kazi mnaanza kunyoosheana vidole nani kasoma wapi-ILI IWE NINI, TUKIWAJADILI HAWA THEN, TUNAENDELEA??
Kama JF ni kisima cha hekima, naomba dongo hili walipokee wote wenye PhD zilizopatikana kwenye vyuo bora kabisa! na wale wanaojadili mambo bila kutauta mzizi wa tatizo!
Maghembe upo? , Mkandala mlimani upo?
Maprofesa wa umeme UDSM mpo?-giza jamani
Maprofesa wa uchumi popote pale mpo?
maprofesa wa uongozi mpo?
na je tukiambiwa walioharibu nchi hii niwasomi wazuri kabisa waliosoma kabla vyuo feki kuzaliwa tutakataa??
are we weak? no, are we inferior? absolute no,
Tujadili jinsi ya kuwabana hawa wote wenye Phd nchini, hawa feki watandoka wenyewe.
tukianza hawa tutakuja na wote wenye bachelor! tuulizane je kazi unayofanya ni ya mtu wa degree? au naweza nikamtrain mtu wa kidato cha nne na akafanya? au degree ni kuwa customer care voda?
tukiweka mtindo wa kudeliver na kusajiliwa, basi feki degrees zote zitaosha.
haya mambo ya mtu akiwa na Phd basi amemaliza kazi! then nani asiyetaka mteremko?