Mauaji yaliyotokea Lemax Bar Sinza kwa Remmy yalikuwa yanaweza kuzuilika mapema

Suala siyo kijiwe chake wala mkewe, mara madeni mara kutisha watu. Kuwalaumu hao waliokimbilia vyumbani kuokoa maisha yao.

Si kila mtu anaweza kukabiliana na tukio la hatari tena lenye kuhusiana na silaha ya moto, hawapaswi kulaumiwa hata kidogo.
kaka kuokoa maisha yako ni wajibu wako wa kwanza kabisa, kwanza mie siwezi kukaa bar ambayo kuna jamaa kalewa afu anatoa chuma anakisafisha safisha pale mezani kisha kukirudisha kiuononi, hapo ni fastaa lipa bill sepa...

Pombe haina adabu naweza kuwawasha wote wote..dadadeq. ila kuokoa maisha ya wajinga niliowaacha pale ni lazima nipite Police niwatonye ili waje kumdaka.

Pombe imemfanyizia jamaa, sasa katuachia mkewe bado mbichi na bongo hii navyoiua - ha ha ha ha
 
Umeandika nini sasa? Yani hapa unakuja na nadharia za kiduanzi kweli. Hivi ni sheria gani inasema mtu akija kwenye bar yako akiwa ameshalewa usimuuzie pombe?

Sheria inakataza usiuze kwa underage tu. Hata haikatazi kunywa kupita kiasi, kuambiwa usinywe kupita kiasi ni unatahadharishwa tu wala sio katazo.
Sijui kwa Tanzania lakini Ulaya ukienda bar yoyote ukiwa umelewa chakari hakuna anayekuuzia pombe. Hata ukiwa bar na ukanywa kupitiliza na kuanza kusinzia au kuyumba yumba unatolewa nje fasta. Nchi nyingi ndivyo ilivyo. Tanzania inawezekana kusiwe na sheria lakini ni vizuri sana kutoamuuzia mtu aliyelewa kupindukia pombe. Hoja za mwanzisha thread zina mashiko kabisa. Hatua zilitakiwa kuchukuliwa mara alipoanza kutoa silaha mara kwa mara huku amelewa.
 
Mauaji yaliyotokea hivi karibui katika eneo la Sinza ndani ya Lemax Bar yaliyosababisha vijana wawili kupoteza maisha baada ya marehemu aliyekuwa anamiliki bastola huku akifanya mambo ambayo ni kinyume na kanuni na tataratibu wa umiliki mpaka kufikia kitendo cha kuua na kujiua

Kwanza nianze kwa kutoa uhalisia kuwa mimi sikwepo katika eneo la tukio ila naandika kwa kutumia shuhuda mbalimbali zilitolewa na watu
Una hoja nzuri sana japo kuna watu wanakebehi. Mmiliki/msimamizi wa Bar mwenye busara hatauza kilevi kwa mtu ambaye tayari yuko chakari. Na pia kama ulivyosema, hatua za kuita polisi zilitakiwa zichukuliwa mara alipoanza kutoa toa silaha yake huku amelewa.
 
Sijui kwa Tanzania lakini Ulaya ukienda bar yoyote ukiwa umelewa chakari hakuna anayekuuzia pombe. Hata ukiwa bar na ukanywa kupitiliza na kuanza kusinzia au kuyumba yumba unatolewa nje fasta. Nchi nyingi ndivyo ilivyo. Tanzania inawezekana kusiwe na sheria lakini ni vizuri sana kutoamuuzia mtu aliyelewa kupindukia pombe. Hoja za mwanzisha thread zina mashiko kabisa. Hatua zilitakiwa kuchukuliwa mara alipoanza kutoa silaha mara kwa mara huku amelewa.
Bora umenielewa mkuu , kuna walevi wabishi sana humu jamii forum
 
Mkewe ingetakiwa amu report anyang'anywe hyo bastola maana alikuwa anajulikana tabia yake ya ukorofi. Ona Sasa kaacha familia yatima na sisi wanawake ujasiri wa kuwa na wagonjwa wa akili huwa tunautoa wapi aisee
Mkuu nadhani wengi walikuwa wanafiria hawezi kupoteza network mpaka aue kirahisi namna hiyo. Unajua sasa hivi ni kwa sababu tukio limeshatokea ndiyo maana tunaona makosa kwa urahisi. Wengi walidhani ni ulevi tu na asingeweza kufika hatua ya kuua.
 
Yatupasa kuwalinda watu wanaokengeuka tusichukulie poa tu kwa kweli, bastola yataka mtu asiye na mihemko ya hovyo hovyo.
 
Mtoa mada una hoja nzuri, Mimi huwa nikihisi hatari yoyote maeneo nilipo cha kwanza ni kupotea hilo eneo mfano upo porini ukasikia harufu ya wali umeiva ujue ni nyoka anajiondoa gamba maeneo hayo sasa uendelee kukaa eneo hilo unatafuta nini na Mungu kakujalia milango ya fahamu ya kutambua hatari.
Kukaa eneo hatarishi ni ujinga wa kiwango cha lami.​
 
Haujanielewa nasema hivi , hawa jamaa tayari walishaona dalili za hatari walitakiwa kufanya juhudi za kutoa taarifa mapema katika mamlaka za usalama ili kumuweka marehemu katika mikono salama , kwa maana hiyo isingefikia hatua ya kukimbilia vyumbani....
Labda kama huwajui polisi wa tz
 
Umeandika nini sasa? Yani hapa unakuja na nadharia za kiduanzi kweli. Hivi ni sheria gani inasema mtu akija kwenye bar yako akiwa ameshalewa usimuuzie pombe?

Sheria inakataza usiuze kwa underage tu. Hata haikatazi kunywa kupita kiasi, kuambiwa usinywe kupita kiasi ni unatahadharishwa tu wala sio katazo.
Upo sahihi Tanzania hakuna kipimo cha mwisho katika kuuza pombe kwa mteja, ni hela yake tu. Kwanza huyu mhudumu angekataa kumuuzia pombe pengine angeanziwa yeye kupigwa risasi na wangefuatia wengine. Wakubebeshwa lawama ni wale waliopitisha uamuzi wa kumpa silaha bila kuchunguza kwa kina, mlevi kupewa silaha ina tofauti gani na kichaa kupewa rungu!​
 
Igp sirro Police kazi yao imejeuka ni kuiba kura na Kubambikiza kesi,.mengine hayo siyo kazi yao
 
Back
Top Bottom