Ajaye
JF-Expert Member
- Sep 25, 2020
- 319
- 595
Wana jamvi habarini za wakati huu.
Jana majira ya saa sita usiku kuna mauaji yametokea yaliyosababishwa na watu wa maliasili.
Tukio hilo limetokea Mkoa wa Pwani, wilaya ya Kibaha (V), tarafa ya Ruvu, Kata ya Kwala, kijiji cha Kwala! ambapo watu wa kubeba mkaa maarufu kama booster wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wa maliasili walipokuwa wakisafirisha mkaa majira ya usiku na kupita maeneo walipokuwa wameweka mtego maliasili.
Watu hao walipigwa risasi na mmoja wao akapoteza maisha hapo hapo, mwingine alifariki akiwa anapelekwa hospital leo saa sita mchana mara baada ya askari wa mlandizi kufika eneo la tukio, mtu huyo mmoja alishindwa kupata msaada wa kwanza kwa muda wa masaa zaidi ya 12 sababu kuu ikiwa ni zuio kutoka kwa watu wa maliasili huku akizidi kupoteza damu nyingi zaidi.
Maoni yangu
Hawa watu ni watafutaji kama watafutaji wengine, wameacha familia zao wakienda kutafuta maisha katika kipindi hiki kigumu tunachopitia watanzania wengi,
Hivyo basi, ni vyema maliasili kuongozwa na utu wakati wa kufanya kazi zenu, silaha ya moto itumike pale penye ulazima tena baada ya kuchukua precautions kama sheria inavyotaka.
Wanajukwaa tupaze sauti ili haki intendeke kwa ndugu wa marehemu, uchunguzi katika hili ninmuhimu sana, maana mauaji yamekuwa yakichukuliwa kama kawaida na hawa wanaojiita watu wa maliasili.