Mauaji yaliyotokea Lemax Bar Sinza kwa Remmy yalikuwa yanaweza kuzuilika mapema

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Mauaji yaliyotokea hivi karibui katika eneo la Sinza ndani ya Lemax Bar yaliyosababisha vijana wawili kupoteza maisha baada ya marehemu aliyekuwa anamiliki bastola huku akifanya mambo ambayo ni kinyume na kanuni na tataratibu wa umiliki mpaka kufikia kitendo cha kuua na kujiua

Kwanza nianze kwa kutoa uhalisia kuwa mimi sikwepo katika eneo la tukio ila naandika kwa kutumia shuhuda mbalimbali zilitolewa na watu mbalimbali juu ya scenerio ya tukio zima

Kwanza nianze tu kwa kusema hata kama ni biashara yaani kupata pesa ilikuwa siyo vyema kumuuzia pombe kwa mtu ambaye amekunywa usiku mzima nje ya eneo lako kisha kuja katika bar nyingine akiwa amelewa alafu wewe mmiliki wa bar bado unaendelea kumuuzia wakati unaona huyu binadamu ameishalewa hili nalo ni jambo lakini pia ni chanzo cha mauaji mwenye bar ahojiwe vizuri ili next time awe na akili juu ya biashara yake

Pili ni kwa watu wengine waliokuwa hapo bar wakiendelea kunywa katika mazingira hatarishi , nao walikuwa na uwezo wa kuzia hayo mauaji, kwa mfano marehemu mmiliki wa bastola pale alipoanza kutoa bastola yake huku akiwa na wenge la kilevi basi wale jamaa wengine kwa haraka walitakiwa kutoa taarifa polisi ili waje kumkamata na kumaliza jambo nasema wale waliokimbilia vyumbani hawakutakiwa kukimbia ila walitakiwa kutoa taarifa mapema tu ili jambo liishe mapema

Tatu ni kwa huyu afisa wa serikali ambaye inasemekana ni usalama wa taifa sijui ni wa kikosi gani huyu jamaa mana sijamuelewa, binafsi naona huyu usalama nae ni feki tu, tunaposema usalama maana yake ni amani

Sasa tujiulize ni afisa gani wa usalama unaeona sehemu uliyopo haina usalama alafu upo upo tu kama vile haujui majukumu yako? Hata kama yeye majukumu yake hayausiki kukamata mtu wa namna hiyo alishindwa nini kutoa taarifa kwa mamlaka zingine zikaja kumkamata?

Tunalaumu tukio kutokea lakini tunamlaumu marehemu ila hata wale wote waliokuwepo katika tukio nao ni sehemu mauaji hayo.

Mwisho

Pia soma:
 
Mauaji kutokea hivi karibuni katika eneo la Sinza ndani ya Lemax Bar na kusababisha vijana wawili kupoteza maisha baada ya marehemu aliyekuwa anamiliki bastola, huku akifanya mambo ambayo ni kinyume na kanuni na taratibu wa umiliki mpaka kufikia kitendo cha kuua na kujiua.

Kwanza nianze kwa kutoa uhalisia kuwa mimi sikwepo katika eneo la tukio ila naandika kwa kutumia shuhuda mbalimbali zilitolewa na watu mbalimbali juu ya scenerio ya tukio zima , niseme hata kama ni biashara yaani kupata pesa ilikuwa siyo vyema kumuuzia pombe, mtu ambaye amekunywa usiku mzima nje ya eneo lako kisha kuja katika bar nyingine akiwa amelewa alafu wewe mmiliki wa bar bado unaendelea kumuuzia wakati unaona huyu binadamu ameishalewa, hili nalo ni jambo.

Lakini pia ni chanzo cha mauaji mwenye bar ahojiwe vizuri ili next time awe na akili juu ya biashara yake , pili ni kwa watu wengine waliokuwa hapo bar wakiendelea kunywa katika mazingira hatarishi , nao walikuwa na uwezo wa kuzia hayo mauaji.Mfano marehemu mmiliki wa bastola pale alipoanza kutoa bastola yake huku akiwa na wenge la kilevi, basi wale jamaa wengine kwa haraka walitakiwa kutoa taarifa polisi ili waje kumkamata.

Na kumaliza jambo nasema wale waliokimbilia vyumbani hawakutakiwa kukimbia ila walitakiwa kutoa taarifa mapema tu ili jambo liishe mapema , tatu ni kwa huyu afisa wa serikali ambaye inasemekana ni usalama wa taifa sijui ni wa kikosi gani huyu jamaa mana sijamuelewa , binafsi naona huyu usalama nae ni feki tu , tunaposema usalama maana yake ni amani , sasa tujiulize ni afisa gani wa usalama unaeona sehemu uliyopo haina usalama alafu upo upo tu kama vile haujui majukumu yako? hata kama yeye majukumu yake hayahusiki kukamata mtu wa namna hiyo alishindwa nini kutoa taarifa kwa mamlaka zingine zikaja kumkamata ?

Tunalaumu tukio kutokea lakini tunamlaumu marehemu ila hata wale wote waliokuwepo katika tukio nao ni sehemu mauaji hayo.

Mwisho.
 
Kwamba hawakutakiwa kukimbia? Haya huyo aliyekufa kwa kujaribu kuzuia unaona walikufa wachache kwahiyo ni heri wangeuawa hata kumi si ndio?
Haujanielewa nasema hivi, hawa jamaa tayari walishaona dalili za hatari walitakiwa kufanya juhudi za kutoa taarifa mapema katika mamlaka za usalama ili kumuweka marehemu katika mikono salama, kwa maana hiyo isingefikia hatua ya kukimbilia vyumbani.
 
Kwamba wale waliokimbilia vyumbani hawakupaswa kukimbia! Akili yako ina ushirikiano mdogo sana na mwili wako.

Mlevi katoa silaha ya moto na anapiga risasi hovyo unawalaumu waliokimbia kunusuru maisha yao? Unadhani kila mmoja ana uwezo wa kukabiliana au kuthubutu kumsogelea mtu mwenye silaha ya moto? Ulitaka wafe watu 40 ili uwaone mashujaa au vipi.

Hebu tumia mitishamba kutengeneza mahusiano ya mwili wako na akili.
 
Yule jamaa kifo alikitaka mwenyewe sifa za kijinga jamaa muoga balaa - kama mwanaume kweli wa shoka kwa nini kajiua baada ya kuua kama si woga.

Afu nasikia ana mke bomba mbaya, ngoja tuanze kumtafuta shemeji yetu kumpa pole huu msina ni mzito mno!
 
Umeandika nini sasa? Yani hapa unakuja na nadharia za kiduanzi kweli. Hivi ni sheria gani inasema mtu akija kwenye bar yako akiwa ameshalewa usimuuzie pombe?

Sheria inakataza usiuze kwa underage tu. Hata haikatazi kunywa kupita kiasi, kuambiwa usinywe kupita kiasi ni unatahadharishwa tu wala sio katazo.
 
Kwamba wale waliokimbilia vyumbani hawakupaswa kukimbia! Akili yako ina ushirikiano mdogo sana na mwili wako.
Wanasemsa kijiwe hicho ndiyo cha jamaa, so wengi wanamjua mzee wa misifa sifa.

Alikuwa anadaiwa laki sita ya ulevi wakamdai hadi mkewe akaja kulipa, jamaa akamaindi nani kamdai mkewe? ndiyo akaenda na chuma kusafisha jina

So wamgeona jamaa hayupo sawa wangemtonya mkewe aje kumchukua au police maana jamaa katishatisha watu muda mwingi tu.
 
Wanasems kijiwe hicho ndiyo cha jamaa, so wengi wanamjua mzee wa misifa sifa.

Alikuwa anadaiwa laki sita ya ulevi wakamdai hadi mkewe akaja kulipa.
Suala siyo kijiwe chake wala mkewe, mara madeni mara kutisha watu. Kuwalaumu hao waliokimbilia vyumbani kuokoa maisha yao.

Si kila mtu anaweza kukabiliana na tukio la hatari tena lenye kuhusiana na silaha ya moto, hawapaswi kulaumiwa hata kidogo.
 
Umeandika nini sasa? Yani hapa unakuja na nadharia za kiduanzi kweli. Hivi ni sheria gani inasema mtu akija kwenye bar yako akiwa ameshalewa usimuuzie pombe?

Sheria inakataza usiuze kwa underage tu. Hata haikatazi kunywa kupita kiasi, kuambiwa usinywe kupita kiasi ni unatahadharishwa tu wala sio katazo.
Huyu jamaa nimegundua mapema kukosekana kwa ushirikiano kati ya akili na mwili.
 
Wanasemsa kijiwe hicho ndiyo cha jamaa...so wengi wanamjua mzee wa misifa sifa.

Alikuwa anadaiwa laki sita ya ulevi wakamdai hadi mkewe akaja kulipa.
Wewe umenielewa vizuri sana hachana na huyo anaejiita Mbao za Mawe akili yake ni ngumu kuchanganua mambo.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
kwani kwenye mabaa siku hizi hakuna kukaguliwa wakati wa kuingia ndani.
Inabidi tujifunze tuache masiala katika maisha lakini pia tushukuru mungu Tanzania haina uadui na vikundi vya kigaidi otherwise tungekuwa tunakufa kama kuku , sisi watanzania washamba sana sijui kwanini.... kule moto unapowaka sisi ndio tunakimbilia huko....
 
Hasingekufa mtu usingepata wazo la kundika nyuzi yako. limetokea na yatatokea mengi tu, kila kitu kinasababu. Hatuwezi kuzuia ajali ila tunaweza kupunguza
 
Back
Top Bottom