Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Wana jamvi habarini za wakati huu.

Jana majira ya saa sita usiku kuna mauaji yametokea yaliyosababishwa na watu wa maliasili.

Tukio hilo limetokea Mkoa wa Pwani, wilaya ya Kibaha (V), tarafa ya Ruvu, Kata ya Kwala, kijiji cha Kwala! ambapo watu wa kubeba mkaa maarufu kama booster wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wa maliasili walipokuwa wakisafirisha mkaa majira ya usiku na kupita maeneo walipokuwa wameweka mtego maliasili.

Watu hao walipigwa risasi na mmoja wao akapoteza maisha hapo hapo, mwingine alifariki akiwa anapelekwa hospital leo saa sita mchana mara baada ya askari wa mlandizi kufika eneo la tukio, mtu huyo mmoja alishindwa kupata msaada wa kwanza kwa muda wa masaa zaidi ya 12 sababu kuu ikiwa ni zuio kutoka kwa watu wa maliasili huku akizidi kupoteza damu nyingi zaidi.

Maoni yangu

Hawa watu ni watafutaji kama watafutaji wengine, wameacha familia zao wakienda kutafuta maisha katika kipindi hiki kigumu tunachopitia watanzania wengi,

Hivyo basi, ni vyema maliasili kuongozwa na utu wakati wa kufanya kazi zenu, silaha ya moto itumike pale penye ulazima tena baada ya kuchukua precautions kama sheria inavyotaka.

Wanajukwaa tupaze sauti ili haki intendeke kwa ndugu wa marehemu, uchunguzi katika hili ninmuhimu sana, maana mauaji yamekuwa yakichukuliwa kama kawaida na hawa wanaojiita watu wa maliasili.
"Hawa watu ni watafutaji kama watafutaji wengine, wameacha familia zao wakienda kutafuta", kwa neno lako hili napendekeza uwe rais wetu rais anayejali watu kujitafutia.
 
Tuendelee kujenga tabia hii ambayo itatufanya na sisi tuwe violence national, police hawaruhusiwi kutumia deadly force, unless maisha ya raia au ya kwake yakiwa hatarini, police state in the making, kulalama humu hakusaidii chochote ni push back ndio lugha hawa kenges watakayo isikia
Niamini nikikwambia, hautofanya chochote, mostly sababu watanzania ni waoga na hiki ulichokisema hakimake any sense.
 
Ongeza na wale wa mbuga za wanyama, hawa watu wanaojiita wa mali asili ni wanyama kuliko wanyama, hawa wanaolinda miti na wanyama wanajiona wapo juu ya sheria wanaweza kumua mtu wanayehisi ana deal na misitu na wanyama pori watamfanya asusa na hawatashitakiwa. Kwa nini wasiwe wanawakamata na kuwapeleka mahakamani kama wanaona misitu yao na wanyamapori wao wanaharibiwa? Ya nini kuua binadamu mwenzako?
 
Tuendelee kujenga tabia hii ambayo itatufanya na sisi tuwe violence national, police hawaruhusiwi kutumia deadly force, unless maisha ya raia au ya kwake yakiwa hatarini, police state in the making, kulalama humu hakusaidii chochote ni push back ndio lugha hawa kenges watakayo isikia
Nakuunga mkono asilimia 100 violence ndio njia pekee ya kuleta usawa nchi flani.hakuna blablaa,wacha waue kisha tukichoka wote ndio tutaheshimiamana
 
Wamejitakia, kwa nini ufanye biashara ya mkaa bila kufuata sheria?
Kwahiyo kufuata sheria kwa watumishi wa serikali ni kumpiga risasi mkata mkaa?
Hawa wangekutwa hifadhini wangetudanganya wamefyatuliana risasi, lakini ni wakata mkaa.
Sheria inawataka askari wawashambulie kwa risasi?
Siku zote askari wa maliasiri hawana utu moyoni, kwao wanyama au miti vina thamani kuliko utu wa mtu.
 
Adhabu ya kufanya biashara ya mkaa bila kufuata sheriani kuuawa? Wewe ni shetani mkuu na ulaaniwe, ufikwe na msiba kama hao unaofurahia kuuawa.
bahati mbaya mtaani matukio huripotiwa tofauti sana.

hawa watu hushambulia askari mara kwa mara kwa mapanga,moja ya case iliyosababisha mambo ya kibiti ni hii.
watu kujiona wana haki sana na hawapaswi kuguswa ktk hilo.

tutakuwa wendawazimu kuamini askari anaweza akaamka tu ameshiba akaanza kurusha risasi kuua watu,halafu tunaendelea na yaliyo kinyume na sheria.
 
Back
Top Bottom