Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Wana jamvi habarini za wakati huu.

Jana majira ya saa sita usiku kuna mauaji yametokea yaliyosababishwa na watu wa maliasili.

Tukio hilo limetokea Mkoa wa Pwani, wilaya ya Kibaha (V), tarafa ya Ruvu, Kata ya Kwala, kijiji cha Kwala! ambapo watu wa kubeba mkaa maarufu kama booster wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wa maliasili walipokuwa wakisafirisha mkaa majira ya usiku na kupita maeneo walipokuwa wameweka mtego maliasili.

Watu hao walipigwa risasi na mmoja wao akapoteza maisha hapo hapo, mwingine alifariki akiwa anapelekwa hospital leo saa sita mchana mara baada ya askari wa mlandizi kufika eneo la tukio, mtu huyo mmoja alishindwa kupata msaada wa kwanza kwa muda wa masaa zaidi ya 12 sababu kuu ikiwa ni zuio kutoka kwa watu wa maliasili huku akizidi kupoteza damu nyingi zaidi.

Maoni yangu

Hawa watu ni watafutaji kama watafutaji wengine, wameacha familia zao wakienda kutafuta maisha katika kipindi hiki kigumu tunachopitia watanzania wengi,

Hivyo basi, ni vyema maliasili kuongozwa na utu wakati wa kufanya kazi zenu, silaha ya moto itumike pale penye ulazima tena baada ya kuchukua precautions kama sheria inavyotaka.

Wanajukwaa tupaze sauti ili haki intendeke kwa ndugu wa marehemu, uchunguzi katika hili ninmuhimu sana, maana mauaji yamekuwa yakichukuliwa kama kawaida na hawa wanaojiita watu wa maliasili.
Aisee huu ni ukatili uliopitiliza
 
Bwana Misitu kama walivyojulikana zamani walikuwa na jukumu la kulinda na kuzuia uchomaji moto misitu uliokuwa unafanywa na wawindaji na wavuna asali, wafugaji walikuwa wanapeleka mifugo kulisha misituni na wafugaji walikuwa wakiwashambulia Mabwana Misitu kwa kuwajeruhi na kuwaua.
Kuweks mambo sawa serikali ikaamua Mabwana Misitu wawe askari misitu kwa kuwapa mafunzo ya uaskari ili waweze kuwadhibiti na kakabiliana na wanaoharibu misitu.
Shida ikaanzia hapo, kuna wale wanaodai wanajitafutia kipato ili wazilishe familia zao iwe haki yao! Hawa ili wapate haki zao wakaanza kujihami kwa kupambana askari wa misitu.
 
Mvua zisiponyesha, mabwawa yakose maji Umeme uwe wa mgao mnailaumu serikali. Maji yakipungua huko Mto Ruvu ambao ndio unalisha Dar mnailaumu serikali..

Tukubali kufata tu sheria, mapori tengefu yasiyoruhusiwa kuvunwa miti yaachwe..
Yanachwa lakini sio kwa kuua mtu mwenye Boda na Mkaa juu ukiona umeona.Ni mfumo tu wa Umaskini wa Akili na Mali.Hayo mapori tengefu ndiyo hayo yanavunwa kimya kimya ndani kwa ndani na hao hao jamaa kwa kuweka washikaji zao.
Bongo hapa Askari akiwa tu na bunduki kaa chonjo hata kama unapiga naye story tu 😁 😁 😁
 
Yote haya ni kwa sababu ya CCM...

Raia wanafanya kazi au shughuli kama hizi kwa sababu ya ugumu wa maisha, hapo unakuta mtu alishajaribu kuuza bidhaa nyinhine mgambo wakatembea nazo...
 
bahati mbaya mtaani matukio huripotiwa tofauti sana.

hawa watu hushambulia askari mara kwa mara kwa mapanga,moja ya case iliyosababisha mambo ya kibiti ni hii.
watu kujiona wana haki sana na hawapaswi kuguswa ktk hilo.

tutakuwa wendawazimu kuamini askari anaweza akaamka tu ameshiba akaanza kurusha risasi kuua watu,halafu tunaendelea na yaliyo kinyume na sheria.
Ndugu yangu unadanganya mchana kweupe? Wewe ni mmoja wa hao askari wauaji? Tanzania mara ngapi tumeona cold blooded killings za polisi kwa wahalifu wasio tishio au hata kwa raia wema? Ni mara ngapi tumeona askari wanaua raia wema ili wachukuwe mali au fedha walizonazo? Kama hili tukio limeripotiwa tofauti, hebu wewe tuambie ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom