Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Mauaji ya wabeba mkaa maarufu 'booster'

Watu hao walipigwa risasi na mmoja wao akapoteza maisha hapo hapo, mwingine alifariki akiwa anapelekwa hospital leo saa sita mchana mara baada ya askari wa mlandizi kufika eneo la tukio, mtu huyo mmoja alishindwa kupata msaada wa kwanza kwa muda wa masaa zaidi ya 12 sababu kuu ikiwa ni zuio kutoka kwa watu wa maliasili huku akizidi kupoteza damu nyingi zaidi.

Maoni yangu

Hawa watu ni watafutaji kama watafutaji wengine, wameacha familia zao wakienda kutafuta maisha katika kipindi hiki kigumu tunachopitia watanzania wengi,
Alaaniwe aliyejimilikisha gas na genge lake aliloliita wawekezaji
 
Huwa najiuliza hawa jamaa wanapata wapi amri ya kuuwa watu hivyo
Sio mara ya kwanza wanatajwa kwa kuuwa na kutesa
Hawa wakikumata na nyama utaila mbichi mpaka iishe, ukikamatwa na asali utainywa mpaka ufe
Hawa naona ni death squad waliopewa kazi maalum maana haiwezekani hakuna kiongozi anaelia na haya mauwaji
Stop the killing stop the dying
 
Unakumbuka yule dogo mpambanaji aliyeibiwa na polisi hela zake za madini mtwara hadi wakamchoma na sindano ya sumu. Na dogo kwenda kudai haki yake kabla ya kumuua yani walivyomtreat utadhani jambazi wakamfungia nakumkalisha chini. Ndugu zake kufuatilia nao vitisho kutaka kubambikiziwa kesi. Mungu akasaidia maza kuingilia kati sijui kesi imefika wapi? Nachukia hawa watu watatu WAONEVU, WASALITI NA WADHULUMATI.
 
Mvua zisiponyesha, mabwawa yakose maji Umeme uwe wa mgao mnailaumu serikali. Maji yakipungua huko Mto Ruvu ambao ndio unalisha Dar mnailaumu serikali..

Tukubali kufata tu sheria, mapori tengefu yasiyoruhusiwa kuvunwa miti yaachwe..
 
Askari kuua wamekosea sana wanastahili kushtakiwa

Ila pia kumbukeni misitu inaisha jamani Tanzania

Tabianchi Tanzania kwa kiwango kikubwa na shughuli za mkaa

Serkali ingepunguza gharama za gesi ili hata sisi wa chini tuweze kumudu
 
African we are not yet a complete human being .

So Fanya self-investment ili uwe civilized enough.

Then Anza kutafuta Certification and acceptance

Tafuta kibali kwa Mungu certifaction na tafuta kukubalika kea Mungu acceptance.

Kwa kushukuru Sana bila kulalamika , kuishi katika wewe na kuwa wewe authentic.

Kugusa Sana watu kwa kutotegema kulipwa na uliyemgusa.

Zingatia this formula

Source = God
Giver =
Taker

So be a giver in this life

Don't complain about anything embrace Love, Affection , kindness , humbleness, goodness .

Practice more gratitude .
So sad brother
 
Back
Top Bottom