Mbona hata kuvuna mkaa kwenye maeneo mengine inaruhusiwa? Tatizo ni baadhi ya watu hawataki kwenda ofisi za maliasili kupata leseni na kulipia ushuru ili serikali ipate mapato yake. Misitu na mapori ni ya Watanzania wote sasa kama wewe Juma na John mnataka kwenda kuvuna mkaa basi kateni leseni, mlipe ushuru na muonyeshwe wapi muende kuvuna mkaa. Mkilipa ushuru ina maana watanzania wengine pia watafaidika na mapato ya Misitu yao. Msipolipa ushuru ina maana mnafaidika nyie tuu peke yenu wakati misitu ni ya wananchi wote.