Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,757
Ubora wa Katiba yetu ya mwaka 1977 na yaitwayo madaraka makubwa ya Rais.
Funzo kwa wenzetu nchi ya haiti na kumpunguzia rais wao madaraka.
Je, watungaji (constitutional framers) wa katiba ya 1977 ya JMT walikosea kumpa rais wetu madaraka makubwa?
Kufuatia mauaji ya rais wa nchi ya Haiti Jovenel Moise kumetokea funzo kubwa hasa kwa Chadema na wote wanaotaka katiba mpya hapa nchini, kwa kigezo cha kumpunguzia rais madaraka yake makubwa.
July 5, hayati Rais wa Haiti Jovenel Moise alimteua waziri mkuu mpya baada ya kumuondoa waziri wake mkuu aliyekuwepo kipindi chote cha uongozi wake.
Bunge lilivunjwa na waziri mkuu mteule alikuwa bado kuapishwa.
Mgogoro mkubwa wa kikatiba.
Kwa katiba ya haiti, bunge ndilo lenye mamlaka ya kusimamia nchi pale ambapo rais atafariki ama kuondolewa madarakani kwa sababu tofauti.
Bunge halipo baada ya kuvunjwa na rais ameuawa baadaye.
Hali hiyo imepelekea kwa mawaziri wakuu wawili (aliyeondolewa na mteule ambaye hajaapishwa) kugombea madaraka ya kuwa rais.
Kufikia leo jioni, waziri mkuu aliyeondolewa madarakani amekichukua kiti cha urais (acting president) na kuzua sintofahamu kubwa kupita kiasi.
Kwetu Tanzania
Kwa funzo hili, nawapa kongole waliotuandikia katiba yetu ya 1977 kwa kule kumpa nguvu kubwa rais wa nchi, kwa kuzifikiria tabia zetu wanadamu.Tabia zetu Waafrika, za kuweza kuyagombea madaraka kwa uchu mkubwa kupelekea kuibua mgogoro mkubwa na kuitia nchi katika mizozo, vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Binafsi nitaendelea kuwasifu waliotunga Katiba yetu bora kwa kutuepushia na matatizo yaliyowapata haiti na baadhi ya nchi nyingine.
Kiukweli kwetu tanzania wala hakuna haja ya kufanya makosa eti tumpunguzie rais wetu madaraka.
Wako watu wasioliona hili ima kwa kutokujua hatari hiyo ama kufanya kusudi ili kutuondolea utulivu wa nchi na kutuchafulia sifa njema ya amani tuliyonayo na inayopigiwa mfano afrika nzima na dunia kwa ujumla.
N.B: Shime tumuunge mkono rais wetu Mh. SSH katika kuujenga uchumi wetu kipindi hiki cha mtanziko wa corona na kuzikataa hila zote za wapenda chokochoko na ukosefu wa utulivu wa kinchi.
#KatibaMpyaSiHitajiLaWatanzaniaWote
#KatibaIliyopoNiBora
#UchumiKwanza
#KaziIendelee
#UchumiKwanza
#DieHardFanOfCCM