Matumizi ya neno KUWEZA kwenye vyombo vya habari yamekaaje?

raslimali

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,344
1,012
Ukisikiliza vyombo vya habari vikiripoti matukio ya vifo au majeruhi utasikia Kwa mfano " watu wawili wameweza kupoteza maisha" au " mtu mmoja aliweza kujeruhiwa". Haya ni matumizi sahihi ya kitenzi hiki?

Nimejifunza lugha za mataifa mengine na msaada mkubwa kwenye kujifunza ilikuwa kusikiliza vyombo vyao vya habari Kwa mfano wajerumani wanayo Deutsche Welle (DW) na taarifa zao za habari wanaziweka kwenye section ya mafunzo ya lugha ya kijerumani ila zinasomwa polepole ili mwanafunzi aelewe.

Sasa najiuliza kama vyombo vyetu vya habari tukivitumia kama kisaidizi Cha wageni kujifunza Kiswahili itakuwaje?

Maana matumizi ya lugha ni shida! Sijui kama Kwa kiingereza ningesema " two people could lose their life in that accident" ," one woman was able to be injured" n.k .

Maoni yenu tafadhali na pia nipo tayari kusahihishwa.
 
Back
Top Bottom