Siku ya kwanza ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, 01/05/2023 Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Fu8OPlTWAAI_ela.jpg



TAMWA WATOA NENO
Baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe amemkaribisha na kutoa neno la ukaribisho.

Anasema: Tunafahamu kuwa hali ya uhuru habari wa kujieleza kwa vyombo vya habari nchini umeimarika na tunaona jitihada zinazofanyika ili kuboresha zaidi.

Hivyo, tutumie siku hizi tatu kutafakari na kujadiliana mambo ambayo yatatuvusha hapa tulipo na kutupeleka kwenye fursa nzuri zaidi ambayo ni uhuru wa kuhariri, kutafuta habari, kuhoji na uhuru wa kujieleza, vyote viwe Mtanzania anapaswa kujivunia.

Pamoja na kutathmini hali ilivyo sasa tutumie jukwaa hili kujadili kwa undani changamoto ambazo bado ni kero katika sekta ya habari.

Changamoto hizo baadhi ni pamoja na hali ngumu ya vyombo vya habari ambayo inasababisha waandishi kufanya kazi katika mazingira magumu, masuala ya ulinzi na usalama kwa Wanahabari vikiwa shakani.
tAMWA.JPG

Tumeona pia mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Habari unachukua muda mrefu, jambo ambalo tunajiuliza nini sababu.

Changamoto nyingine ni usawa wa kijinsia katika vyombo vyetu vya habari, Wanawake wamekuwa wakiongezea katika tasnia hiyo katika kipindi hiki cha miaka 30 lakini bado nafasi za uongozi katika utawala, uhariri na nyanja za kisiasa uwakilishi wao ni mdogo.
Tamwaa.JPG

Aidha, baadhi ya vyombo vya habari havitendi haki vinapoandika kuhusu taarifa za kijinsia.

Tunafahamu kuwa hakuna uhuru usio na mipaka, waandishi wa habari tunapaswa kuzingatia misingi ya taaluma na maadili, tunatakiwa kulinda faragha za watu wakati tukitimiza majukumu yetu.

Pia tuepuke kulaumu pale tunapokumbushwa na mamlaka kuhusu majukumu yetu.
Tau.JPG

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Tabia Maulid Mwita (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Progamu wa JamiiForums, Glory Tausi, leo Mei Mosi, 2023 katika Siku ya Kwanza ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani linaloendelea Ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe.

MDAJALA UMEANZA
Wadau mbalimbali wanatoa maoni kuhusu tasnia ya habari, mjadala unaongozwa na mwanahabari mkongwe Ally Saleh.

SALIM SALIM: Ninaona fahari kuwa na Wanafunzi wengi wanahabari, wengi niliowafundisha miaka ya 1980 na 1990 ni tofauti na hawa wa leo. Vijana wa sasa ni wavivu wa kusoma, wanachojua zaidi ni Diamond kaimba nini lakini hawajui mambo yanayoendelea.

Hata hotuba aliyotoa Makamu wa Rais wa Tanzania alipokuwa Arusha hivi karibuni vijana wengi hawaijui lakini nilikuta waandishi wa Ivory Coast wakiisoma na kujua Makamu wa Rais wa Tanzania amesema nini.

Mfano inaweza kutokea Rais kapanda miti, waandishi wataripoti tukio lile na kusahau kufuatilia hiyo miti kama inatunzwa au la, pia Rais akitembelea hospitali kuzindua, Mwanahabari anatakiwa kujua je miundombinu iliyopo inafanya kazi kwa usahihi kama vile inawajali walemavu na watu wengie wenye uhitaji?

Wanahabari wakongwe hamtakiwi kuishia kulaumu tu bali tumieni uzoefu wenu kuwaelewesha wanaochipukia pindi wanapokosea.

Tufuatilie miradi ya Serikali, ubora uliotakiwa ndio ambao upo kwenye sehemu husika, wananchi wanasemaje na kuna uhalisia wa thamani ya fedha na miradi husika
Salim.JPG


ROSE HAJI: Wanahabari tunatakiwa kufuatilia maisha halisi yanayowakabili wananachi, kumekuwa na hofu ya kufichua uhalisia wa kinachoendelea, kama vile malalamiko ya barabara na mengine yanayohusu uwajibikaji.

WAZIRI TABIA MWITA:
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Tabia Maulid Mwita anazungumza:

Dunia hivi saa ina kabiliwa na changamoto ya uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, nimefurahi kuona moja kati ya mada ni kujadili changamoto ya mazingira, naamini mtakuja na mawazo mazuri ya kuleta njia ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

Serikali inaahidi kushirikiana na UNESCO, tunawapongeza TAMWA kwa kushirikiana na Idara ya MAELEZO katika maadhimisho haya.

Ningefurahi kuona maadhimisho haya yanaibua changamoto za kisera na maboresho ya mazingira.

Binafsi nafahamu Serikali ya Awamu ya Sita, inatekeleza miradi mingi ya manedeleo kwa manufaa ya wananchi wake.

Wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu miradi mbalimbali ya Serikali na jinsi Wananchi wanaweza kunufaika kwa kinachofanywa ili kukitokea kuna changamoto ya kukwama au kusita waweze kupaza sauti juu ya malalamiko yao mbalimbali.

Enao la miradi ya maendeleo ni pana, Wanahabari mnategemewa katika kutengeneza taswira chanya kwa faida ya maendeleo.
Waziri.JPG

Kuhusu Sheria mpya ya habari
Nimeona kuna ujumbe mbalimbali kuhusu umuhimu wa madai ya kupata sheria mpya ya habari husususani Zanzibar, mchakato umefika 80%.

Tumesikia mijadala na vilio kuhusu uwepo wa sheria hiyo, Serikali ya Awamu ya 8 ya Rais wa Zanzibar ni sikivu.
Ndio maana mchakato wa kukusanya maoni kwa Wadau wa Habari umefanyika mara kadhaa, changamoto kila hatua inapoenda mbele ikifika hatua ya mwisho, tunaambiwa turudishe tuipitie.

Kila hatua ya Serikali turudishe nyuma, michakato inayofanyika ni ileile, iaminini Serikali ili Muswada uingie kwenye Baraza na hatimaye tuweze kuwa na Sheria.

Naamini ni Sheria nzuri kwa Wanahabari wote, tusiwe na mashaka, kinachofanyika ni dhana kama vile Serikali haina wataalam, niwaambie tunaikamilisha na tupo katika hatua nzuri, tumrangalia Bara na mazingira yetu ya Zanzibar, hivyo tuna muundo mzuri.

Napongeza Wizara ya habari kwa kutengeneza mchakato wa kuwa na maafisa habari, kada ya habari itatambulika kama kada maalum.

Tutakuwa na Maafisa Habari wenye weledi na watakaokuwa wanatoa taarifa sashihi na wa kwa wakati.

NEEMA LUGANGIRA (Mbunge):
Katika Habari, Teknolojia ya kidigitali imeleta mabadiliko makubwa, hali hiyo imefanya kuwa na taarifa nyingi za kupotosha na kinachotokea vyombo vya habari vikubwa vinatumia taarifa za watu hao kama vyanzo vyao vya habari

"Mara nyingi tunashudia Vyombo vya Habari tunavyoamini vinachapisha habari lakini baada ya muda wanakuja kukanusha kwamba haikuwa ya kweli. Ipo haja kwa vyombo vya habari kutokupelekeshwa na teknolojia ili kujiepusha na utoaji wa taarifa za uongo kwenye jamii."

Mbunge Neema Lugangira anasema “Suala la ulinzi wa taarifa binafsi za Afya ni moja ya elimu muhimu ambayo inatakiwa kutolewa kwa Waandishi wa Habari ili tuisemee kwa pamoja kuleta mabadiliko chanya.”
Ameongeza “Unaweza kukuta unanunua kitu unafungiwa katika karatasi na unagundua kuwa kilichotumika ni taarifa za Afya za mtu fulani.”
Neema.JPG

MSIGWA:
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema “Ubunifu umepungua sana kwenye Tasnia ya Habari na ndio maana wachekeshaji wanachukua nafasi kwa kuwa wameona fursa, kuna watu wamekaa kwenye tasnia kwa miaka mingi na wamezuia vijana wapya kuingia.”

Ameongeza “Ndio maana vijana wamehama wameenda kwenye mitandao, hata kunapotokea wito kwa wanahabari, wale wa mtandaoni wanajali muda na wanafika kwa wingi kuliko wale wa kwenye vyombo vikubwa.

Amesisitiza “Tuongeze ubunifu, huwezi kuwalazimisha waje kwako unatakiwa kuwashawishi.”
Msig.JPG

GEAH HABIB:
Mwanahabari Geah Habub anasema “Ukikutana na Mtoto aliyebakwa na ukaruhusiwa umuone utaumia sana, ombi kwa Serikali ifanyike kampeni kubwa kuwafikishia ujumbe Watoto jinsi ya kujilinda na kutoa taarifa za ukatili.”

Anaongeza “Kuna matukio mengi ya ukatili na Watoto hawasemi kwa kuwa wanatishiwa kuwa wakisema watauliwa au watapigwa, tukiwapa elimu kuwa wakifanyiwa au wakiona dalili za ukatili watoe taarifa tutakuwa tumewaokoa wengi.”

Anasema “Inawezekana tukawatumia watu maarufu kama kina #DiamondPlatnumz au #FistonMayele kuwafikishia ujumbe muhimu kwa maisha yao.”
geah.JPG

MAKAMU MWENYEKITI MISA: JAMES MALENGA
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), James Marenga anasema “Wanaofanya upotoshaji mitandaoni kwa asilimia kubwa ni Wanahabari na si Waandishi wa Habari, kwa kuwa kuna tofauti kati yao, Mwandishi wa Habari anaelewa maadili ya taaluma yake."

Marenga anaongeza “Mfano mtu akiweka maudhui yake kwenye jukwaa la #JamiiForums lakini kama si suala la ukweli na lenye faida watalishusha haraka kwa kuwa wanajua athari zake ni zipi.”

Anasisitiza “Hii mitandao mingine ya Wanahabari ambao hawajui athari au Sheria ataacha, hiyo ni changamoto kubwa.”
Marenga.JPG

SALOME KITOMARI: WANAWAKE WANA HOFU KUMILIKI MITANDAO YA HABARI
Mwandishi Mwandamizi Salome Kitomari anasema “Asilimia kubwa ya wanaomilikiwa mitandao ya kijamii kama vile blog au tovuti na nyinginezo ni Wanaume, upande wa Wanawake bado wana hofu hali ambayo imetokana na makuzi ambayo ndiyo yameathiri uelewa wa wengi.”

Anaongeza “Katika Vyombo vya Habari pia Wanawake hasa wale wanaoanza kuingia katika tasnia wanakutana na changamoto za ukatili wa kingono ambao unachangia wanashindwa kusonga mbele.”
Salo.JPG

SALOME KITOMARI: WANAOFANYA UKATILI WANA VISINGIZIO VINGI
Akizungumzia kuhusu matukio ya ukatili Mwandishi Mwandamizi Salome Kitomari anasema “Matukio ya rushwa ya ngono au ubakaji yamekuwa na visingizio vingi, mara huyu kavaa hivi au vile lakini jiulize Mtoto wa miaka mitatu au Mtoto wa kiume amefanya nini mpaka akakushawishi kumfanyia ukatili.”

Anasema “Kuna visingizio vingi vinavyowekwa ili kumrudisha nyuma Mwanamke, hata katika mtandao ya kijamii watu wanautumia uhuru vibaya, wanaenda kutoa maoni ya ajabu kwenye kurasa za watu bila sababu za msingi.”
Salo 2.JPG


ZAMARADI KAWAWA: WACHEKESHAJI WANAOINGIZWA KWENYE TASNIA YA HABARI WAPELEKWE SHULE
Mwandishi wa Habari, Zamaradi Kawawa anasema “Kuna jambo ambalo naona linatendeka na ninaona lipo ndivyo sivyo, halitakiwi kulifumbia macho.”

Anaongeza “Kuna tabia imeanzishwa ya wachekeshaji kuwapa vipindi ambavyo ni ‘makini’ nadhani kama kuna ulazima huo kwa kuwa wanadai ndio wanaongeza mapato sokoni basi wapelekwe shule ili waelewe misingi ya taaluma.”

EILEEN MWALONGO: SERIKALI ITENGENEZE MFUMO WA UPATIKANAJI WA WANAHABARI KWENYE VYOMBO VYA HABARI
Afisa Program wa JamiiForums, Eileen Mwalongo anasema “Natoa wito kwa Serikali kushirikiana na Wadau ambao wapo kwenye taaluma ili kutengeneza njia sahihi na nzuri ili hao wanaoonekana ni wachekeshaji wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari watumike katika njia nzuri.”

Anaongeza “Tusikatae kuwa intaneti imekua tena kwa kasi kubwa, hakuna njia ya kuweza kukwepa, muhimu ni kutengenisha aina ya utendaji kazi ili kupunguza taarifa ‘feki’ na zile ambazo ni sahihi.”
ei.JPG


NYONZO: JUKWAA LA JAMIICHECK LINAENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI
Akizungumza katika siku ya kwanza ya Kongamano la Miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayofanyika, Zanzibar, afisa Program wa JamiiForums, Francis Nyonzo “Kuhusu Jukwaa la JamiiCheck linalopatikana kwenye tovuti ya JamiiForums.com lipo linaendelea kutoa taarifa ambazo ni sahihi na kufafanua zile ambazo si sahihi

Utaratibu huo umekuwa ukiendelea na umekuwa ukitoa mwangaa mzuri kuhusu taarifa ambazo si sahihi zinazosambaa kwenye jamii hasa mitandaoni
ny.JPG


NYONZO: MATUMIZI YA MTANDAO KWA WATOTO YADHIBITIWE SIO KUZUIA
Afisa Program wa JamiiForums, Francis Nyonzo anasema “Serikali imebainisha kuwa ina mpango maalum wa kuwawezesha Wanahabari katika elimu ya Teknolojia, hilo ni jambo zuri na ninalipongeza.”

Anaongeza “Tunapozungumzia matumizi ya mtandao nitoe mfano, tunawaandaaje Watoto na elimu ya digitali, tunawapa simu wakiwa wadogo kabisa, wakifika umri wa kutaka kifaa hicho tunawanyang’anya kwa kuweka Sheria lakini kumbuka huu ni ulimwengu wa digitali, ni vizuri kujua jinsi ya kudhibiti matumizi yasiyo sahihi na siyo kumzuia kutotumia kabisa.”
 
Back
Top Bottom