Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

Unapaswa kuweka flight mode ili laini za simu ziwe off.
Utaweka Ila shetani nae ana yake
Mara utapitiwa utatoa

Ni Jambo jema watu Wana app za Bible kwenye simu lakini sidhani Kama Ni sahihi Sana kutumia biblia ya kwenye simu kanisani,,
Kwa Nidhamu na kumuheshimu Mungu Ni vema ikatumika hardcopy
 
Kikawaida simu zetu tunazitumia kwenye mambo mengi maovu km kuangalia porn,kutext michepuko ,matusi nk na hata kama hufanyi hayo lakin utakuwa umewahi kupokea mawaidha maovu kwenye simu yako halafu unaitumia na kanisan kama kitabu kitakatifu sipingi sana ila kama unajua unafanya hayo nilyoyataja ni bora ukabeba Biblia kitabu not app asee
 
Bible app ni nzuri sana kama utaitumia vizuri na ukiamua kutulia na kujifunza,binafsi imenisaidia sana kukua kiroho, kuna app moja kwangu ni bonge la faida huwa namshukuru sana Mungu kwaajili ya hiyo app na Mungu azidi kuitunza na kuibariki,hiyo app kiasi kwamba hata nikipoteza simu huwa nakonda kabisa,app ya YOUVERSION ni bonge la Bible app,kwanza ina version mbalimbali na katika lugha mbalimbali karibu zote hata ukitaka the Bible yenyewe ya kiyahudi,hii imekuwa ikinisaidia sana kama sijaelewa mstari Fulani unamaanisha nini huwa na jaribu kusearch katika Version mbalimbali hadi napata maana kamili, pili imekuwa ikinisaidia sana kwa reference kama nahitaji maandiko mengine yafananayo na hayo,tatu imekuwa ikinisaidia sana kuupata mstari Fulani ninaouhitaji kwa haraka,kuna wakati unakumbuka maneno ila umesahau yako wapi ,NNE app hii ina masomo mbalimbali katika kila sekta ya hapa duniani utakuta Devotional mbalimbali kuna za mwaka mzima,wiki,mwezi,siku kadhaa n.k,kwahiyo huwa nafaidika sana na devotional hizo,mfano labda nataka kujua maswala fulani yahusuyo uponyaji nitasearch neno healing zitakuja devotional mbalimbali basi nitachagua ile niipendayo,kwa kweli sijutiii kuijua hii app.

Nije kwa kanisani huwa napenda kutumia Biblia ya kawaida offcoz kwasisi wazazi Biblia ya kawaida ni somo zuri sana kwa mtoto,ila kadri anavyokuwa ni vizuri kumfundisha pia mambo mazuri yaliyopo kwenye Bible app,yaani hii app ukiitumia vizuri kwakweli hata Insta utajikuta huna muda nayo,pia unapobeba Biblia yako inakutambulisha wewe ni mtu wa aina gani, pili kibongo bongo bado sana unapotumia Simu kanisani unaonekana mtu usiyejitambua hata Paulo alifundisha alipoenda kwa wenye hekima naye alikuwa mwenye hekima,alipoenda kwa wapumbavu naye alijifanya hivyo na alipoenda kwa watoto wadogo naye alijifanya ni mtoto mdogo,so si vizuri kuwa kwazo kwa watu wengine tumeamriwa tuheshimu mamlaka zilizopo,ole wake akwazikaye na aletaye makwazo, kwako inaweza kuwa fresh tu ila kuna jirani yako hapo unaweza kumpotezea concentration kabisa akatoka uweponi akabaki anakufikiria wewe na simu yako,ila wakati mwingine tunapokuwa Bible study sometime kunatokea kujifunza mbalimbali na mabishano labda kwahiyo nikitaka reference ya neno Fulani basi huwa nachomoa simu na kusearch fasta tu. Ila bado hivi vyote ni muhimu sana Biblia ya kawaida na App nakushauri uwe navyo vyote tu,hizi ni technology chochote chaweza tokea na shetani pia hapendi neno la Mungu lisambae kwa haraka Kwa watu wote na shetani tukumbuke hujifanya kama malaika wa nuru so humu humu anaweza kupita,kuna kipindi Fulani hata hizi za kawaida zilitoka na kiswahili kibaya kabisa wakaona bora waziondoe sokoni wazirudishe za zamani.

Ila sasa hasara kubwa ya kutumia Bible app ni Memory capacity inakufa kabisa yaani ule uwezo wa kukariri umepotea,najikuta maneno najua au habari Fulani naijua ila iko kitabu gani ni shida.
 
Mi nilishawishiwa nikaenda kawe kwa mwamposa. Eti kukanyaga mafuta.
Aisee!!!, Watu wanaselfika balaa. Yaan ni mwendo wa kutwanga photo. Hata nikasahau kilichonipeleka.
 
Mkuu hatusemi moja kWa moja bible app ina ubaya hapana.
Kuna mazingira Fulani inafaa sana kama hayo uliyosema.

Tunachokataa hapa ni kuingia Nayo kanisani.
Trust me kuna watu huwa wanakwazika kwa mtu mwingine kutumia simu kanisani hasa viongozi kitu ambacho unamsababishia atende dhambi muumini mwenzio akiwa ibadani..

Lakini pia watoto huwa hawaamini kama unasoma biblia wanachojua wao unachezea simu , wanaanza kuona kumbe hata ibada sio kitu cha serious kiviile.......hivyo UNYENYEKEVU mbele za Mungu unatoweka taratibu tangu wakiwa wadogo.

Ambao hawataki Bible App. Jibu swali hili rahisi


Kuna nchi ukionekana na Biblia ni jela ndeefu sana.

Kuna nyumba mtu anataka kusoma biblia lakini mazingira hayaruhussu .

watasomaje hawa watu ?

Kabla ya Kubuniwa karatasi wenzetu waliandika kwenye vitu vingine hameoni kama ni muendelezo wa ugunduzi wa teknolojia.

Je utakatifu upo kwenye kitabu su yalr maandishi, wapo watu wametengeneza lizra za kuvutia bangi karatasi laini za biblia.
 
Mabadiliko ni lazima, na hupaswi kuyakataa ila inabidi utafute nafasi yako ya kuishi ndani ya mabadiliko hayo, uliwengu wote unatoka kwenye hardcopies books unaenda kwenye matumizi ya softcopy, ambayo ni rahisi kubeba na kuwa accessible sehemu na wakati wowote, anayepinga matumizi ya bible app ni zwazwa wa technology na ni mpinga mabadiliko. Hata mauzo ya softcopy material yanazidi kuongezeka kuliko hardcopies materials, nilishaacha kubeba hardcopy bible mwaka wa nne huu sasa.


Wengine wanatoa sababu eti oooh zitaingia sms ukiwa kanisani, yes, tatizo liko wapi hapo? Mimi sms ikiingia naijibu vizuri tuu kwa kuwa sms hainizuii kwenda mbinguni, mbona kuna wakati Yesu alifuatwa na watu akiwa ktkt ya mahubiri na wakamwambia ndugu zako wapo nje wanakusubiri mfano huo unatofauti gani na sms iliyoingia katikati ya ibada?
 
Labda tu nikwambie kiufupi ...maswala ya roho usiyaweke kwenye teknolojia ... ROHO na teknolojia ni tofaut teknolojia inatumiwa na ibilis kwa asilimia nyingi hvo kitu chenye roho ya MUNGU mfano biblia hakitaweza kuwa na nguvu ikiwa kikiwekwa sehem ambayo ibilisi ametawala asilimia kubwa


SIMU Inaweza beba video za ngono
simu hio hio umetumia kusema uongo
af baadae uweke biblia my friend hautaielewa

KEY POINT
Ukitaka uone kama biblia ya kwenye simu haina maana ...katika ROHO
Fanya yafuatayo
Siku ukiona mtu amepandwa pepo chukua simu yako yenye biblia ndan kisha sogea karibu yake uanze kusema ushindwe kwa jina la yesu ..na mwingine ashike biblia kama kitabu uone nani atakaekabwa shati na kupasuliwa simu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ukisema suala la video za ngono kuwepo kwenye simu, au kuitumia simu kwa namna isiyo njema, inabidi pia ufahamu biblia kama kitabu hakina tofauti na kitabu kingine chochote, ila matumizi sahihi ya neno lililopo ndani ya biblia ndio yanayofanya mabadiliko kwenye maisha ya mtu, so haijalishi neno hilo umelisoma kwenye bible hardcopy au softcopy kama utafanya sawa sawa na linavyotaka utapata matokeo.

Pia kuwa na video za ngono kwenye simu haizuii matumizi ya simu kama biblia kwa kuwa kuna watu ni wazinzi na wanaingia kanisani na condom waende wakazini wakitoka, kuna wachungaji wanaongea uongo madhabahuni, kuna watu wanaingia kanisani wakiwa ni wasengenyaji na waongo... sasa hao na aliyebeba simu kama bible nani bora?

Lazima tukubali mabadiliko, ulimwengu wote unakwenda huko.
 
Ni bora aliyetunza uchafu kwenye simu kuliko aliyetunza uchafu moyoni, kwa hiyo kuna watu wanaingia wakiwa na hiyo hardcopy bible kanisani na kuanza kutamani wake au waume za watu ndani ya kanisa, au wanawaza uzinzi, usengenyaji unafiki n.k, so mimi sioni tatizo kabisa la kuingia na bible app kanisani
Shida siyo hiyo Bible app iliyopo kwenye simu...

Shida ni kwamba zaidi ya bible app kuna mautumbo na mauchafu kibao umetunza kwenye simu yako...

Katikati ya ibada mara notification hizo za mambo ya ajabu...


Cc: mahondaw
 
Tumieni manual bible bhana, achaneni na hivi vi app, maana unaweza ukawa church misa inaendelea unasoma mstari mzuri mara kanotification kanaingia "baby nijibu basi au nirudi" [emoji23][emoji23][emoji23] usipojibu hapo basi shetani atakuwa pekeyake motoni,
Ni bora hiyo sms uione ukiwa kanisani sababu itakupa kujitafakari tena kuhusu kiwango chako cha unafiki mbele ya Mungu, na huenda itakusaidia ukatubu
 
Mimi naona ni kushindana na wakati tu,watu wanasahau kuwa kuabudu ni imani haijalishi unatumia Biblia ya kawaida au ya Simu...
 
Mi nadhani kwa ushauri tu kama unaweza ukatumia Bible App bila matatizo ni vyema ukatumia kutokana na advantages zake nyingi tu. . .ila kwa wale wenye udhaifu au wanahisi si sawa waendelee kubeba vitabu hard copy. Kila mtu abaki kwenye safe zone yake bila kunyoosheana vidole.
Mimi nitaendelea kutumia Bible App kwasababu hainiletei shida wala usumbufu wowote ule. Tena ndio inanisaidia sana hata kujua mambo ya kimungu. (bibile app ninayotumia mimi huwa inakuwa na session za quiz ambayo huwa inanichallenge uelewa wangu), naweza kutake notes chapchap na kuzireview kwa urahisi)
 
Nakubaliana na Mtoa hoja. Makanisa yanapaswa kuliona hili na kubadilika. Ili huo uchakachuaji tunaohofia usitokee kwa kuweka version sahihi kwenye hizo App. Mfano Katoliki version ya vitabu 72. Lakini msingi mwingine ni Elimu kwa watumiaji. Mfano namna ya kuzuia simu kupata notifications ukiwa church. Mabadiliko ya teknolojia usipokubali kwenda nayo yatakubadilisha kwa lazima na hapo ndipo utajikuta yamekubadilisha vibaya. Tujikumbushe Musa alipokabidhiwa zile Amri kumi za Mungu ziliandikwa katika mawe. Lakini sasa tunazisoma katika makatatasi na sasa Apps. Those are changes due to technology advancement. Faida za simu inaweza kubeba kabati zima la vitabu into one simple gadget. But referencing and browsing chapter is easy than hard copies. Suala la namna ya kutumia ni dogo ambalo waumini wanaweza kufundishwa na wakafuata, lakini siyo kupingana na teknolojia.
 
Ukisema suala la video za ngono kuwepo kwenye simu, au kuitumia simu kwa namna isiyo njema, inabidi pia ufahamu biblia kama kitabu hakina tofauti na kitabu kingine chochote, ila matumizi sahihi ya neno lililopo ndani ya biblia ndio yanayofanya mabadiliko kwenye maisha ya mtu, so haijalishi neno hilo umelisoma kwenye bible hardcopy au softcopy kama utafanya sawa sawa na linavyotaka utapata matokeo.

Pia kuwa na video za ngono kwenye simu haizuii matumizi ya simu kama biblia kwa kuwa kuna watu ni wazinzi na wanaingia kanisani na condom waende wakazini wakitoka, kuna wachungaji wanaongea uongo madhabahuni, kuna watu wanaingia kanisani wakiwa ni wasengenyaji na waongo... sasa hao na aliyebeba simu kama bible nani bora?

Lazima tukubali mabadiliko, ulimwengu wote unakwenda huko.
biblia huwez ilinganisha na kitabu kingine cha kawaida jaribu kujenga hoja upya
 
Nilisikia mtumishi mmoja akisema hivi, mtu amesave mavitu ya ajabu alafu unafungua bible app ibadani! Likifunguka dude lako bahati mbaya [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂hii point ya msingi sana
 
Hako kashetani hakaji wakati unatumia bible app tu hata kama ipo mfukoni! Ni tabia tu!
Hiyo ni kweli ila kuna wanaoweza kutumia huo mwanya vibaya wakajidai kusoma bible kumbe mtu anachat na demu wake.
 
Kweli maana inawezekana dunia ya miaka 1000 ijayo haya makaratasi yasiwepo kabisa na yakapigwa marufuku kama mifuko ya plastiki! Wapunguze kutuchamba bana dah [emoji41][emoji41][emoji41]
Mwaka 1970 jamaa alitabiri ifikapo mwaka 2000 kutakuwa hakuna haja ya kutumia karatasi popote pale duniani lkn naona utabur wake umegonga mwamba ila matumiz ya karatasi yamepungua sana
 
Bibilia hardcopy inakuwa imebarikiwa.

Hiyo App haijabarikiwa.

Kubeba bibilia yako au misale ya waumini kwa masaa mawili ya week nzima sio mbaya.
 
Bibilia hardcopy inakuwa imebarikiwa.

Hiyo App haijabarikiwa.

Kubeba bibilia yako au misale ya waumini kwa masaa mawili ya week nzima sio mbaya.
Bonge la point hili.
 
Back
Top Bottom