Nilivyokutana na Mlokole kwa mara ya pili

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
13,910
Reaction score
28,202
Screenshot_20260905-100410_Google.jpg

Nipo zangu mgahawani napata chakula cha mchana,pale mezani nakutana na dada mtu mzima kiasi

Wote tunakula ugali na dagaa,mboga ya majani na ndondo,yes maharage

Sorry to say this in case wewe ni mlokole, hawa watu huwa lazima tu wajitambulishe kuwa ni walokole kwa namna yoyote ile, hupenda tuwajue kuwa ni watu wa Mungu,sasa sisi wengine sijui ni watu wa nani?

Anyways, akaanza kunipa lecture juu ya yeye kuchaguliwa na Mungu,kwa kawaida huwa nimejifunza kuwa na adabu ya kumsikiliza mtu kwa asilimia 100

Basi nikampa full attention kama nipo chachi vile,akaniambia amehifadhi vifungu 68 vya biblia,ni kweli kabisa,akaanza kusoma kifungu kimoja baada ya kingine,kiufupi yupo vizuri

Baada ya kumaliza msosi tukaagana nikasepa,wakati naondoka dada wa mgahawani akaniambia "naona umekutana na mama mchungaji leo hahah"

Nikamjibu ndio alikuwa ananipa mistari,basi siku ikaisha kwa stahili hiyo

Jana nikajisogeza zangu mgahawani mida ya 1936hrs hivi, nikamkuta bwana,alisahau kama tulishawahi kukutana last time na alinipa mistari ile ile tena,lakini this time alisema kitu kimoja

Kwamba alienda chachi flani hivi,akamkuta pasta wa hapo ana vifungu au mistari michache tu ya biblia ambayo hutamba nayo,so alipopewa nafasi akatiririka mistari au vifungu vyote 68 huku watu wanafuatilia kwenye Biblia

Akaniambia alifukuzwa pale chachi kwa kuonekana kuwa ni mchawi,kwamba inakuwaje ahifadhi vifungu vyote vile

Swali la kujiuliza kama alionekana ni mchawi kwanini hakuombewa atolewe huo uchawi?

Lakini kitu kinachoingia akilini ni kwamba viongozi wa lile kanisa la kilokole,waliona wivu kwa yule dada kuwa na vifungu vile vya Biblia kichwani,angali wao hawana zawadi hiyo,ndio maana walimfedhehesha yule dada na asionekane tena pale chachi

Ila kwa kadri nilivyo msoma yule dada pia ana arrogance/kiburi flani hivi,huenda kwakuwa amehifadhi vile vifungu basi anajiona the chosen one

Ila walokole bwana mdada wa watu kahifadhi verses 68 za Bible imekuwa shida je,waislamu wanao hifadhi verses 6,000 na kitu?

Moral of the story: Hata ukiwa umebarikiwa kipawa kiasi gani usiwe na kiburi,hata uwe na vibration au aura au energy fulani be humble,wacha hivyo vipawa vijidhihirishe vyenyewe naturally ila usiwe loud mbele ya watu,hakika watataka kukuangusha tu

Have a nice day

Ni hayo tu!
 
Sijawahi kusikia Mkristo anajivunia idadi ya vifungu alivyokariri, labda watoto wanaojifunza kusoma!

Sounds like something a Muslim would make up, maybe she's an ex Muslim? ? ?

Nimesearch saa hizi
Biblia ina vifungu 31,000+
Ya wakatoliki inaenda hadi vifungu 36,000+
Ya Ethiopian Orthodox itakuwa nyingi zaidi labda 40,000+

Vifungu 68 kati ya 31000 ni asilimia 0.2! ! !
 
To me, walokole wote wana changamoto ya afya ya akili. Kwa sababu
1. Unawezaje kukubalinkusali kanisa ambalo mpo ndani wachache lakini mnawepa mispika mikubwa ambayo inakuwa kero hata kwa majirani.
2. Unapata wapi akili ya kuhubiri barabarani huku wapita njia wakiwa hawana time na wewe.
 
View attachment 3663713

Nipo zangu mgahawani napata chakula cha mchana,pale mezani nakutana na dada mtu mzima kiasi

Wote tunakula ugali na dagaa,mboga ya majani na ndondo,yes maharage

Sorry to say this in case wewe ni mlokole, hawa watu huwa lazima tu wajitambulishe kuwa ni walokole kwa namna yoyote ile, hupenda tuwajue kuwa ni watu wa Mungu,sasa sisi wengine sijui ni watu wa nani?

Anyways, akaanza kunipa lecture juu ya yeye kuchaguliwa na Mungu,kwa kawaida huwa nimejifunza kuwa na adabu ya kumsikiliza mtu kwa asilimia 100

Basi nikampa full attention kama nipo chachi vile,akaniambia amehifadhi vifungu 68 vya biblia,ni kweli kabisa,akaanza kusoma kifungu kimoja baada ya kingine,kiufupi yupo vizuri

Baada ya kumaliza msosi tukaagana nikasepa,wakati naondoka dada wa mgahawani akaniambia "naona umekutana na mama mchungaji leo hahah"

Nikamjibu ndio alikuwa ananipa mistari,basi siku ikaisha kwa stahili hiyo

Jana nikajisogeza zangu mgahawani mida ya 1936hrs hivi, nikamkuta bwana,alisahau kama tulishawahi kukutana last time na alinipa mistari ile ile tena,lakini this time alisema kitu kimoja

Kwamba alienda chachi flani hivi,akamkuta pasta wa hapo ana vifungu au mistari michache tu ya biblia ambayo hutamba nayo,so alipopewa nafasi akatiririka mistari au vifungu vyote 68 huku watu wanafuatilia kwenye Biblia

Akaniambia alifukuzwa pale chachi kwa kuonekana kuwa ni mchawi,kwamba inakuwaje ahifadhi vifungu vyote vile

Swali la kujiuliza kama alionekana ni mchawi kwanini hakuombewa atolewe huo uchawi?

Lakini kitu kinachoingia akilini ni kwamba viongozi wa lile kanisa la kilokole,waliona wivu kwa yule dada kuwa na vifungu vile vya Biblia kichwani,angali wao hawana zawadi hiyo,ndio maana walimfedhehesha yule dada na asionekane tena pale chachi

Ila kwa kadri nilivyo msoma yule dada pia ana arrogance/kiburi flani hivi,huenda kwakuwa amehifadhi vile vifungu basi anajiona the chosen one

Ila walokole bwana mdada wa watu kahifadhi verses 68 za Bible imekuwa shida je,waislamu wanao hifadhi verses 6,000 na kitu?

Moral of the story: Hata ukiwa umebarikiwa kipawa kiasi gani usiwe na kiburi,hata uwe na vibration au aura au energy fulani be humble,wacha hivyo vipawa vijidhihirishe vyenyewe naturally ila usiwe loud mbele ya watu,hakika watataka kukuangusha tu

Have a nice day

Ni hayo tu!
Mimi nikajua Kuna kula kimasiara aiseee😀😂

Natania TU in dudubaya voice
 
Ila hao wanaohubiri mitaani ni kama huwa wana changamoto ya akili. Huwa nawasikiliza tu (pale inapobidi) cha muhimu ni neno la Mungu, hayo mengine watajuana na Mungu wao.
 
Sijawahi kusikia Mkristo anajivunia idadi ya vifungu alivyokariri, labda watoto wanaojifunza kusoma!

Sounds like something a Muslim would make up, maybe she's an ex Muslim? ? ?

Nimesearch saa hizi
Biblia ina vifungu 31,000+
Ya wakatoliki inaenda hadi vifungu 36,000+
Ya Ethiopian Orthodox itakuwa nyingi zaidi labda 40,000+

Vifungu 68 kati ya 31000 ni asilimia 0.2! ! !
Ishu hapa ni kwamba amehifadhi kichwani vyote kwa usahihi mkubwa,yani ukiwa na biblia na yeye akitoa kichwani ni mule mule neno kwa neno,inaweza isiwe big ishu lakini anastahili kongole

Quran ni rahisi kukaririka kwakuwa ipo kwenye mfumo kama wa mashair na imefanywa rahisi kuhifadhi na Allah mwenyewe
 
Ila hao wanaohubiri mitaani ni kama huwa wana changamoto ya akili. Huwa nawasikiliza tu (pale inapobidi) cha muhimu ni neno la Mungu, hayo mengine watajuana na Mungu wao.
Halafu siku hizi wapo wengi sana,kuna mmoja ni mama pale kawe stand ya Tanganyika pekazi,sometime anahubir mwenyewe bila watu kuwa around

Unaweza hisi hawa watu wamechanganyikiwa

Lakini hata nabii Nuhu wakati anatengeneza Safina alionekana chizi kutengeneza jahazi nchi kavu,lakini mwisho wa siku walijua hawajui

So leo huenda tunawaona kituko ila mwisho wa siku itajulikana
 
Seems ana mental disorder,

Muulize maisha mengine vp, atakuwa anashida somewhere anatumia dini kujiona yuko sawa
Alinipa background yake pia,ni mtoto yatima,huenda changamoto hiyo nayo imemsumbua sana,aliniambia just imagine hujui ndugu zako,hujui kama una Shangazi

Inasikitisha kwakweli
 
Halafu siku hizi wapo wengi sana,kuna mmoja ni mama pale kawe stand ya Tanganyika pekazi,sometime anahubir mwenyewe bila watu kuwa around

Unaweza hisi hawa watu wamechanganyikiwa

Lakini hata nabii Nuhu wakati anatengeneza Safina alionekana chizi kutengeneza jahazi nchi kavu,lakini mwisho wa siku walijua hawajui

So leo huenda tunawaona kituko ila mwisho wa siku itajulikana
Enendeni mkawafanye watu wote kuwa watumishi wangu sio?
Tatizo mmegoma kwenda kanisani, ni kuwasakanya tu kila mahali mlipo hadi kieleweke.
 
Back
Top Bottom